AINA YA MAGONJWA YA AKILI Unyogovu (Depression ) ni mojawapo ya ugonjwa wa akili ambao unahusishwa na hisia za huzuni, kukosa matumaini, na kupoteza furaha au shauku katika shughuli za kila siku. Huu si tu hisia ya huzuni iliyokatisha tamaa, bali ni hali sugu inayoweza kuathiri mabadiliko ya mwili, mawazo, na tabia ya mtu. Unyogovu unaweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kemikali katika ubongo, maumbile, mazingira, na matukio mbali mbali katika maisha ambayo kupelekea mgonjwa kuwa hivyo.