image

Jifunze zaidi mzunguko wa mfumo wa damu kwa binadamu

Posti hii inahusu zaidi mfumo wa mwili ambao huhusika na kusafirisha damu ,virutubisho na takamwili.mfumo huu unajumuisha damu,mishipa ya damu na moyo.moyo husukuma damu kupitia mishipa ya damu na kufika maeneo yote ya mwili.

Maana ya mfumo wa mzunguko wa damu wa binadamu.ni mfumo wa mwili ambao huhusika nankusafirisha damu,virutubisho nantakamwili.mfumo huu unajumuisha damu,mishipa ya damu na moyo.moyo usukuma damu kupitia mishipa ya damu na kufika maeneo yote ya mwili.

 

  sehemu za mfumo wa mzunguko wa damu wa binadamu.

Sehemu zinazofanya mfumo wa mzunguko wa damu ni damu,moyo na mishipa ya damu.kila sehemu ya damu na kufika maeneo yote ya mwili.

 

 Pia damu no tishu iliyo katika halo ya kumiminina inayoundwa na plizima au uzegili,seli hai nyekundu ,seli hai nyeupe na chembe sahani.sehemu kubwa  ya damu ina zaidi ya asilimia 55 iliyoundwa na plazima.

 

plazima(uzegili):plazima ni kimimimiko cha damu kinachojumuisha kiwango kikubwa cha maji na vitu vingine kama protini,globulikinga na elektroliti.kazi kubwa ya plazima ni kumpokea takamwili na kurekebisha halijoto mwilini.protini zilizopo kwenye plazima huzuia kuvuja kwa damu kutoka kwenye mishipa na kugandisha damu kwenye jeraha.pia plazima ina globulikinga ambazo husaidia mwili kupambana na vimelea vya magonjwa.

 

        seli nyekundu za damu:seli nyekundu za damu zina umbile la suara iliyobonyea katika Kati .seli hizi hubeba kampaundi ya damu yenye rangi nyekundu hazina nyukiliasi na utengenezwa kwenye iroto wa mifupa.seli hizi hudumu kwabzaidi ya miezi 4 na bahada ya apo huvunjwa vunjwa na ini ili kuondoa ayani ilizobeba .kazi ya seli nyekundu za damu ni kusafirisha gesi ya oksijeni na kabondayoksaidi mwilini.

 

     seli nyeupe za damu:seli nyeupe hazina umbo maalumu na zialna uwezo wa kubadilika kuwa katika maumbo mbalimbali .seli hizi zina nyukiliasi na huzengenezwa katika iroto wa mifupa na kwenye matezi ya limfu kazi kubwa ya seli nyeupe ni kulinda mwili kwa kupambana na vimelea vyaagonjwa.

 

     Chembe sahani:hizi ni seli ndogo za damu zisizo na nyukiliasi .seli hizi hazina umbo maalumu na huzengenezwa kwenye iroto wa mifupa .kazi ya chembe sahani ni kugandisha damu hasa katika jeraha.

 

         moyo.​​moyo ni organi inayopatikana ndani ya kifua na umeegemea upande wa kushoto wa mwili wa binadamu.kazi kubwa ya moyo ni kusukuma damu kutoka kwenye moyo kwenda sehemu zingine za mwili .pia hivo hivo moyo umegawanyika katika sehemu kuu mbili. Yaani kulia na kushoto .kila upande una vyumba viwili ,chumba cha juu na chumba cha chini hivyo kufanya jumla .vyumba vinne.

 

  Majina ya vyumba hivyo ni atriamu ya kulia,atriamu ya kushoto,ventrikali ya kulia na ventrikali ya kushoto.sehemu ya juu ya moyo ni pana zaidi kuliko ya chini.

 

   Hata hivyo vyumba vya chini yaani ventrikali ni vikubwa zaidi kuliko vyumba vya juu yaani atriamu .Kati ya atriamu na ventrikali za kila pande kuna vali.vali zingine mbili zipo sehemu mishipa mkuu inapoungana na moyo.

 

Ingawa moyo wa wanyama aina ya mamalia una vyumba vinne,moyo wa wanyama wengine upo tofauti ,mfano ,moyo wa wanyama aina ya amfibia kama vyura una vyumba vitatu..

 

Atriamu zote hupatikana sehemu ya juu ya moyo wakati ventrikali hupatikana sehemu ya chini ya moyo.kuta za ventrikali ni nene kuliko kuta za atriamu.hii ni kwa sababu vyumba hivi husukuma damu kwenda kwenye mapafu na mwili.ventrikali ya kushoto ni nene kuliko ventrikali ya kulia kwa sababu ventrikali ya kushoto husukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili .ventrikali ya kulia husukuma damu kwenda kwenye mapafu.

 

 Atriamu ya kushoto imeunganushwa na mishipa wa vena ya palmonari ambao hupokea damu yenye oksijeni kutoka kwenye mapafu na kuongoza kwenye ventrikali ya kushoto ,Atriamu ya kulia imeunganushwa na mshipa wa vena kuu ambao hupokea damu yenye kabondayoksaidi kutoka kwenye ventrikali ya kulia na kuipeleka kwenye mapafu.mshipa wa ateri kuu yaani aota hupokea damu yenye oksijeni kutoka kwenye ventrikali ya kushoto na kuipeleka sehemu mbalimbali za mwili.

 

.   Jinsi moyo unavyofanya kazi ya kusukuma damu:vyumba vya moyo vina huwezo wa kutanuka na kusinyaa kwa kupishana.ventrikali zinapopanuka,atriamu usinyaa ,hivyo hivyo,ventrikali zikisinyaa atriamu hutanuka .kitendo cha kutanuka na kusinyaa cha ventrikali na atriamu  huitwa mapigo ya moyo mapigo haya husababisha msukumo wa damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mishipa ya damu.kwa kawaida moyo hudunda aunkupiga mara 70 kwa dakika moja .mapigo aya ya moyo huwezesha damu huzunguka kwenye mwili bila kukomaa.atriamu zinaposinyaa ,vali vali iliyopo katikati ya atriamu na ventrikali hufunguka, hivyo damu husukumwa na atriamu kwenda kwenye vyumba vya chini viitwavyo ventrikali.Venzrikali zinaposinyaa ,vali iliyopo Kati ya atriamu na ventrikali hujifunga ili damu isirudi kwenye atriamu.kusinyaa kwa ventrikali ya kushoto husukuma damu kwenda sehemu zote za mwili kupitia mishipa ya aota .Hali kadhalika ,kusinyaa kwa ventrikaliu ya kulia husukuma damu kwenda kwenye mapafu kupitia ateri ya palmonari.vali zinazotenganisha hujifunga ili damu isirudi kwenye ventrikali .

 

. Mishipa ya damu:mishipa ya damu ni njia mahalumu ambazo damu hupita ili kuzunguka katika sehemu mbalimbali ya mwili.mishipa hii ni ateri,vena na kapilari.

ateri.hii ni mishipa inayosafirisha damu yenye oksijeni kutoka kwenye moyo kwenda sehemu mbali mbali za mwili isipokuwa ateri ya palmonari.ateri ya palmonari hisafirisha damu yenye kabondayoksaidi kutoka kwenye ventrikali ya kulia kwenda kwenye mapafu.kwa kawaida,mishipa ya ateri haina vali .Ateri ya palmonari ni mshipa pekee ateri wenye vali .kazin ya vali kwenye ateri ya palmonari ni kuzuia damu isirudi kwenye moyo na hivyo  kuwa na mwelekeo mmoja .Ateri kuu ambayo ni aota husaidia kusafirisha damu kutoka kwenye moyo na kwenda sehemu mbali mbali za mwili.

vena:hii ni mishipa inayosafirisha damu kw kiasi kikubwa cha gesi ya kabondayoksaidi isipokuwa vena ya palmonari.vena ya palmonari hisafirisha damu yenye oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenye moyo.vena zote hurudisha damu kwenye moyo.damu hiyo huwa kwenye msukumo mdogo.kwa hiyo ,vena zote tina vali ili kuzuia damu kurudi ilipotoka 

kapilari:hii ni mishipa midogo ambayo hisafirisha damu na kuifikisha kwenye kila seli ya mwili.kapilari hungana na ateri upande mmoja na upande wa pili imeungana na vena .kapilari ni mishipa yenye kuta myembamba sana na hivyo huruhusu miyeyusho mweneo kutokea miyeyusho mweneo huwezesha kupenya kwa mahitaji mbalimbali ya seli.na takamwili zilizozalishwa na seli.mahitaji haya ni kama majib,chakula,na gesi ya oksijeni ,takamwili za seli ni kama kabondayoksaidi,yurea chumvi chumvi na mabaki ya dawa

. Namna nyingine mfumo wa damu unavyofanya kazi.

damu kutoka kwenye moyo husukumwa kwenda sehemu mbalimbali za mwili.kupitia ateri kuu inayoitwa aota .Aota umegawanyika katika matawi matatu.tawi la kwanza hupeleka damu kwenye kuta za moyo.tawi la pili hupeleka damu sehemu za juu za mwili yaani mikono,shingo na kichwa .Tawi la tatu hupeleka damu sehemu za chini za mwili kiwiliwili na miguu.

Matawi haya ya ateri kuu hugawanyika kufanya mishipa midogo midogo zaidi inayoitwa kapilari ambayo hufika kwenye seli .vyakula na mahitaji mengine huchukuliwa na seli za mwili kwa njia ya miyeyusho mweneo.hali kadhalika takamwili na hewa ya kabondayoksaidi kutoka kwenye seli huingizwa kwenye kapilari hizo hungana kutengeneza vena ambazo hurudisha damu kwenye moyo kupitia vena kuu.

 

Ateri ya palmonari husafirisha damu yenye kabondayoksaidi kwenda kwenye mapafu .Gesi ya kabondayoksaidi hupenya kwenye kapilari na kutolewa nje kupitia mfumo wa hewa .vilevile ,oksijeni iliyopo kwenye mapafu huingia kwenye kapilari ambazo hungana kufanya vena ya palmonari inayorudisha damu kwenye moyo.mfumo wa damu hufanya kazi kwa kishirikiana na ogani nyingine amabazo ni bandama ,ini,figo,na mapafu .

.      Uhusiano Kati ya mifumo ya damu na mifumo mingine.

Mfumo wa damu una uhusiano na mifumo mingine kama mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ,mfumo wa utoaji takamwili na mfumo wa upumuaji.

 

    uhusiano Kati ya mfumo wa damu wa chakulachakula.Damu yenye oksijeni inayoingiza kwenye utumbo mwembamba hubeba chakula kilichomeng'enywa  na kuipeleka kwenye ini kupitia vena ya potoini . kutoka kwenye ini damu hiyo huchukuliwa na vena ya hepatiki ambayo hujiunga na vena kuu.

 

 

 

 

 

 

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4404


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Magonjwa ya kuambukiza
Magonjwa ya kuambukiza: Ni yale yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine au kutoka kwa wanyama kwenda kwa mtu Mlipuko tukio lililoenea la ugonjwa katika jamii kwa wakati fulani ambao huonekana kama kesi mpya kwa kiwango ambacho kinazi Soma Zaidi...

Namna ya kuzuia virusi vya ukimwi
Posti hii inaelezea kuhusiana na kujikinga au kuzuia virusi vya ukimwi. Soma Zaidi...

Tatizo la ngozi kuwasha (ugonjwa wa kuwashwa kwa ngozi
Dermatitis ni hali inayofanya ngozi yako kuwa nyekundu na kuwasha. Ni kawaida kwa watoto, lakini inaweza kutokea katika umri wowote. Hakuna tiba iliyopatikana ya ugonjwa wa Dermatitis Soma Zaidi...

Dalili za miguu kufa ganzi
Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo Uweza kujitokeza na kuona kwamba ni Dalili za miguu kufa ganzi, pengine utokea kwa watu wote na pengine huwa ni kwa ghafla Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye mfumo wa usagaji chakula unaotokea kwenye utumbo mkubwa (diverticulitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na mifuko midogo midogo, iliyobubujika ambayo inaweza kuunda kwenye utando wa mfumo wako wa usagaji chakula. Wao hupatikana mara nyingi katika sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (koloni). Hali hiyo inajulikana kama Divert Soma Zaidi...

Saratani ya matiti (breasts cancer)
Post yetu inaenda kuzungumzia kuhusiana na Saratani ya Matiti ni Saratani ambayo hutokea katika seli za matiti. Baada ya Saratani ya Ngozi, Saratani ya matiti ndiyo Saratani inayojulikana zaidi hugunduliwa kwa wanawake Mara nyingi. Saratani ya Soma Zaidi...

Vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Zijue hatua za kufata ili kuepuka maradhi ya tumbo
Posti hii inaelezea kuhusiana na hatua za kufata ili kujikinga au kuepuka maradhi ya tumbo.kuna vitu vikikosekana husababisha maumivu ya tumbo. Soma Zaidi...

Dalili na ishara za kuvimba kope.
Posti hii inaonyesha Dalili na ishara za kuvimba kope ambayo kitaalamu hujulikana Kama blepharitis. Soma Zaidi...

Dalili na ishara za jipu la Jino
Jipu la jino ni mfuko wa usaha unaosababishwa na maambukizi ya bakteria. Soma Zaidi...

Maajabu ya damu na mzunguuko wake mwilini.
Ukistaajabu ya Musa utastaajabu ya Firauni. Haya ni maneno ya wahenga. Sasa hebu njoo u staajabu ya damu Soma Zaidi...

ninatatizo la miguu kuuma nimepima wanasema seli nyeupe za damu ipo chini Sana sasa nauliza dawa hizi za vitamin k na sindano vinaweza nisaidia?
Upungufu wa damu ni tatizo la kiafya, lakini kupunguwa seli nyeupe za damu ni tatizo zaidi, nikwa sabaabu seli hizi ndizo ambazo hupambana na wadudu shambulizi wanapoingia mwilini. Soma Zaidi...