MARADHI YA MOYO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

MARADHI YA MOYO

1.MAGONJWA YA MOYO:
Moyo unanasibiana na magonjwa mengi sana ambayo wengi hawayajui. Watu wamezoea presha kuwa ndio gonjwa la moyo wanalolijua, ila sio hivyo kuna mengi zaidi. Hali za maisha zinaweza kuwa sababu nzuru ya kupata magonjwa ya moyo, miongoni mwa hali hizo ni kutofanya mazoezi ama vyakula mtu anavyokula

Cardiovascular diseases (CVD) ni maradhi au upungufu flani unaotokea kwenye moyo au mishipa ya damu. Moyo na mishipa ya damu hutengeneza mfumo unaoitwa cardiacvascular system. Hivyo magonjwa yote na matatizo yeyote yanayotokea kwa kuathiri moyo na mishipa ya damu huitwa magonjwa ya cardiacvascular diseases. Tafiti zilizofanywa marekani zinaonesha kuwa maradhi haya ndio yanayochangia vifo vya watu wengi marekani. Miongoni mwa magonjwa haya ni kama shambulio la moyo (heart attact), kupalalaiz (stroke), shinikizo la juu la damu yaani presha ya kupanda na atherosclerosis. Magonjwa haya hushambulia zaidi watu walio na umri zaidi di ya miaka 40. Na maradhi haya yanaweza kutokea tangia utototni.

Unawezakupata maradhi haya kwa kurithi kutoka kwa wazazi, ila inategemea namna unavyoishi ndio tatizo linaweza kuwa kubwa ama dogo. Kwa mfano kuvuta sigara, kuwa na uzito mkubwa, kuwa na kisukari na kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu husababisha tatizo hili kuwa kubwa zaidi. Tafiti zinaonesha karibia milioni 60 marekana wana moja kati ya magonjwa hya na karibia watu milioni moja hufa kwa sababu ya magonjwa haya kila mwaka.

AINA ZA MAGOJWA HAYA (CARDIACVASCULAR DISEASES)
1.Kupalalaizi (stroke); karibia watu 160,000 hufa kwa stroke. Stroke ni shambulio la harka amablo linatokea pindi damu inayotembea kwenye ubongo ikapata hitilafu yoyote. Hutokea pindi damu ikaganda katika vimishipa hivyo na kuzuia mzunguruko wa damu kwenye ubongo. Au hutokea mishipa ikapasuka na kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo. Hali hizi zote zikitokea hueza kusababisha kupalalaizi. Mishipa hii huweza kupasuka kama shinikizo la damu likawa kubwa sana. Wataalamu wa afya wanatueleza dalili ya tatizo hili kabla halijatokea. Dalili hizi ni kama:-
A).Kuchoka kwa ghafla kwa mikono, miguuna kuona maluelue.
B).Kushindwa kuona jicho moja au yote
C).Kizunguzungu cha ghafla au kupoteza fahamu.
D).maumivu ya kichwa ya ghafla bila ya sababu maalum

2.Shinikizo la juu la damu (high blood pressure);Kitaalamu tatizo hili huitwa high blood pressure au hypertension. Watu wengi hawajijui kama wana tatizo hili ila wanakuja kujikuta wamepatwa na shambulizi la moyo (heart attack) au stroke. Shinikizo la damu ni hali inayotokea katika mfumo wa damu ambapo kasi ya mzunguruko wa damu inakuwa kubwa zaidi kiasi kwamba njia haitoshi hivo kujalibu kutanua kuta za mishipa ya damu na misuli ya moyo

. Huweza kusababisha stroke au kuufanya moyo kufanya kazi kwa taabu ama moyo kushindwa kabisa kufanya kazi. Pia huweza kuathiri baadhi ya viungo vya mwili kama figo, na macho. Kuganda kwa mafuta kwenye kuta za damu huenda ikawa ni sabubu kubwa ya kutokea kwa tatizo hili kama tutakavoona hapo mbele.
v 3.Shambulio la moyo (heart attack); mishipa ya coronary arterries inakazi ya kusafirisha dabu yenye oxyjen na virutubisho (nutrients) kwa ajili ya kulisha seli za moyo zinazoufanya moyo ufanye kazi yake. Mishipa hii ni myembamba na imeuzungurika moyo.sasa ikitokea damu imeganda kwenye mmoja ya mishipa hii na kuzuia damu isipite kwenye mshipa ule na kuifanya damu isifike kwenye moyo, hii huweza kusababisha seli za moyo zikafa kwa kukosa hewa ya oksijeni na virututisho vilivyotakiwa kuletwa kupitia mshipa ule.

Na hapa mtu atasikia maumivu kwenye kifua chake. Na hii ni kwa sababu ya moyokutoweza kupata damu ya kutosha. Shambulio la moyo ni kuathirika kwa misuli ya moyo au kushindwa kufanya kazi misuli ya moyo. Shambulio la moyo halinaga dalili za waziwazi ila wataalamu wa afya wanataja hizi;-
A)kuhisi kubanwa na maumivu katikati ya kifua na hali hii huendelea kwa muda wa dakika kadhaa.
B)Maumivu yanayoendelea mpaka kwenye mabega, shingo na mkono.
C)Kutokujisikia saswa kifuani kunakofuatana na kuzimia, kutoka jasho jingi sana, damu za pua, au kuvuta punzi chache sana.

4.Atherosclerosis; hii hutokea pale mishipa ya damu inapokuwa na mafuta (fatty) yaliyoganda kwenye mishipa hiyo na kuathiri mzunguruko wa damu wa kawaida. Hali hii ni hatazi kwani inaweza kuzuia damu kuzunguruka katika shemu kadhaa za damu. Pia kama donge la mafuta haya likibanduka na kuingiea kwenye damu na likaingia kwenye coronary arterries (vimishipa vinavyolisha misuli ya moyo) inaweza kusababisha shambulio la moyo na kama litaingia kwenye ubongo litasababisha stroke. mafuta Kawaida

NAMNA YA KUPAMBANA NA MARADHI HAYA
1.Punguza kula kula vyakula vya mafuta kwa wingi na upunguze pia kula chumvi nyingi.
2.Hakikisha uzito wako upo katika kiwango kinachotakiwa. Nnda kapime ujuwe unazito sahihi.
3.Wacha kuvuta sigara
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Punguza misongo ya mawazo.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Download App yetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 722

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Dalili za mimba changa kutoka

Post hii inaenda kuzungumzia zaidi kuhusiana na mimba zinazoharibika . mimba huweza kuaribika au kutoka anzia miezi 3 na kuendelea .

Soma Zaidi...
Dalili za saratani ya tishu (leukemia)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na saratani za tishu ambazo kitaalamu hujulikana Kama Leukemia kawaida huhusisha seli nyeupe za damu. Seli zako nyeupe za damu ni wapiganaji hodari wa maambukizo - kwa kawaida hukua na kugawanyika kwa utaratibu, kadri mwi

Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa unaohusiana na kuzidi kwa joto mwilini (anhidrosis) ama heatshock

posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa na Ugonjwa unaohusiana na joto ambao hujulikana Kama Anhidrosis ni kutoweza jasho kawaida. Usipotoa jasho mwili wako hauwezi kujipoza, jambo ambalo linaweza kusababisha joto kupita. wakati mwingine inaweza k

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia ugonjwa wa kisonono

Posti hii inahusu zaidi njia ambazo utumiwa Ili kuweza kuzuia kuwepo ugonjwa wa kisonono, kwa kufuata njia hizi ugonjwa huu wa kisonono unaweza kupungua kwa kiasi au kuisha kabisa.

Soma Zaidi...
Ishara na dalili za saratani ya mdomo.

Posti hii inaonyesha dalili na mabo ya hatari kwenye ugonjwa wa saratani ya mdomon.Saratani ya mdomo inarejelea Kansa inayotokea katika sehemu zozote zinazounda mdomo. Saratani ya mdomo inaweza kutokea kwa: Midomo, Fizi, Lugha, Nd

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa degedege na dalili zake

Ugonjwa wa degedege ni ugonjwa unaowapata sana watoto chini ya miaka mitano ingawa na watu wazima wanapatwa na ugonjwa huo

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu ugonjwa wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni madhara yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kupitisha mkojo na via vya uzazi kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
ninaisi kma kunakitu kwenye koo alafu kuna ali ya weupe kwenye ulimi na Mashavu kwa ndan

Weupe kwenye ulimi unaweza kuwa ni hali ya kawaida. Weupe huu ukichanganyika na utandu huwenda ikaashiria uwepo wa hali fulani za kiafya.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Uvimbe kwenye ubongo

Posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe au puto katika mshipa wa damu kwenye ubongo. Uvimbe kwenye Ubongo unaweza kuvuja au kupasuka, na kusababisha kuvuja damu kwenye ubongo. Mara nyingi, kupasuka kwa Uvimbe wa Ubongo hutokea katika nafasi kati

Soma Zaidi...
NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO: kuosha mikono, kuwa msafi, kuvaa viatu, maji safi, kuivisha nyama vyema

NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo.

Soma Zaidi...