image

Maumivu makali ya tumbo la chango wakati wa hedhi na sababu zake

Kwa nini unapata maumivu makali wakati wa kuingia hedhi, je unajuwa sababu za maumivu makali ya tumbo la chago.

Maumivu makali ya tumbo la chango wakati wa hedhi na sababu zake


MAUMIVU YA HEDHI MAKALI SANA



Maumivu ya tumbo la hedhi kikawaida yanatambulika kama tumbo la chango kwa wakinamama. Katika hali ya kawaida maumivu haya sio makali kiasi cha kuharibu ratiba za mwanamke. Lakini hutokea wakati mwingine yakawa makali sana kiasi cha kupelekwa hospitali, ama mwanamke kushindwa kufanya shughuli zake. Sasa nini sababu ya maumivu haya kupitiliza? Makala hii itakwenda kuangalia sababu za maumivu makali ya tumbo la chango au maumivu makali ya tumbo la hedhi.


Sababu za maumivu makali ya tumbo la hedhi
Kama mwanamke anaingia hedhi kwa na maumivu makali anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu kama ibuprofen. Lakini kama kuna sababu nyingine zinazopelekea maumivu kuwa makali hata akimeza dawa hii maumivu yatakuwa ni yenye kuendelea.


Dalili za maumivu makali ya hedhi ni
1.maumivu yasiyokata hata baada ya kumeza dawa za kupunguza maumivu
2.Kama maumivu makali kiasi cha kuharibu ratiba za shunguli za kawaida
3.Kama maumivu yanafuatana na damu nyingi ama kuganda kwa damu


Nini sababu ya maumivu makali ya hedhi?
1.kuota kwa tishu (nyamnyama)
maeneo mengine tofauti na tumbo la mimba. Kitaalam hali hii inatambulika kama endometriosis. Hali pia inaweza kuwa na dalili zifuatazo:-
A.Kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi
B.Hedhi kuchukuwa siku zaidi ya 7
C.Kutokwa na damu kabla ya siku za hedhi kufika
D.Maumivu ya tumbo
E.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
F.Kupata maumivu wakati wa haja kubwa.
G.Kuchelewa kupata ujauzito


2.Shida kwenye mfumo wa homoni, hali hii kitaalamu inatambulika kama Polycystic Ovary Syndrome (PCOS). hali hii ni ya kawaida sana takribani kwa kila wanawake 10 mmoja wao huwa na hali hii. Miongoni mwa sababu kuu ni kuwa na homoni za kiume nyingi (androgens) na kutokuwa na siku maalumu za kupata hedhi. Hali hii inaweza kuwa na dalili kama:
A.Kutokwa na damu nyingi sana
B.Kupata hedhi kwa muda mrefu
C.Kuota ndevu ama mwele kuwa nyingi maeneo mbali mbali ya mwili kama ilivyo kwa wanaume
D.Kuwa na uzito mwingi na usio rahisi kuupunguza
E.Kuota chunusi
F.Kunyonyoka kwa nywele na kukosa afya
G.Kuwa na madoa madoa meusi kwenye ngozi


3.kuwa na uvimbe kwenye kizazi kitaalamu hali hii hutambulika kama fibroids. Huu I uvimbe usio wa saratani unaoota kwenye tumb la mimba. Unaweza kuwa uvimbe mmoja ama zaidi. Unaweza pia kuwa na uvimbe bila ya kuonyesha dalili zozote hali hii ikichanganyika na maumivu ya chango inaweza kuonyesha dalili kaka:
A.Maumivu ya mgongo kwa chini
B.Maumivu ya miguu
C.Kupata damu nyingi ya hedhi
D.Kupata hedhi zaidi ya wiki
E.Kukosa choo kikubwa
F.Kukojoakojoa mara kwa mara
G.Kushindwa kumaliza mkojo wote.


4.kuwa na maambukizi ama mashambulizi ya bakteria, fangasi ama virusi kwenye kizazi. Kitaalamu hii huitwa Pelvic Inflammatory disease au maarufu kama PID. Miongoni mwa dalili zake ni:-
A.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
B.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
C.Kutokwa na majimaji yanayotoa harufu kwenye uke
D.Maumivu wakati wa kukojoa
E.Homa
F.Kutokwa na damu kidogo kabla ya kuingia hedhi na baada ya kuingia hedhi


5. Maumbile ya kwenye shingo ya uzazi kitaalamu huitwa cervical stenosis, hii ji hali ambayo mlango wa shingo ya kizazi unakuwa ni mdogo sana. Huenda mwanamke amezaliwa ivyo ama mlango umeziba baadaye.


6.kukaza kwa tishu (nyamnyama) za kwenye tumbo la mimba kitaalamu hai hii inatambulika kama (andenomyosis). hali hii hutokea pale nyamnayma laiki za kwenye tumbo la mimba zinapokuwa ngumu na kubadilika kuwa misuli.


7.matumizi ya baadhi ya njia za kuthibiti uzazi kama Intrauterine Device (IUD). hiki ni kifaa kidogo kinachowekwa kwenye tumbo la mimba. Kijikifaa hiki mwa wanawake wengine kinaweza kuwaletea shida za kiafya kama:
A. Maumivu makali wakati wa hedhi
B. Kutokuwa na siku maalumu za hedhi yaani hedhi inaruka ruka
C. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi


NINI NIFANYE KUKABILIANA NA MAUMIVU HAYA
1.fanya mazoezi mara kwa mara
2.Tumia pad zilizo kavu
3.Hakikisha huna stress yaani misongo ya mawazo kupitiliza
4.Oga maji ya moto
5.Tumia dawa za kupunguza maumivu ya chango kama ibuprofen na acetaminophen
6.Tumia vitamini kama vitamini B1, na B6, madini ya magnesium na omega-3 fatty acid.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2538


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Fangasi wanaosababisha mapunye dalili zao na jinsi ya kupambana nao
Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni. Soma Zaidi...

Njia za kuangalia sehemu yenye maumivu
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia sehemu yenye maumivu, hili kugundua mahali mtu anaumia ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya mgonjwa na mhudumu. Soma Zaidi...

NINI SABABU YA VIDONDA VYA TUMBO
NENO LA AWALI Hapa utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu vidonda vyatumbo. Soma Zaidi...

AFYA NA MAGONJWA: (kisukari, saratani, UTI, presha, mafua, vidonda vya tumbo) na mengine
Soma Zaidi...

Zijue sababu za kushindwa kushuka kwa makende (testicle))
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kushindwa kushuka kwa makende kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye skolatumu(scrotum). Soma Zaidi...

Msaada kwa wenye Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwahudumia wenye Maambukizi kwenye mifupa, ni njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuwasaidia wenye Maambukizi kwenye mifupa. Soma Zaidi...

Dalili kwa mtu anayeharisha
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitia kinyesi chenye maji inawezekana kina damu au kisichokuwa na damu. Soma Zaidi...

Madhara ya kutotibu uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo
Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu ugonjwa wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni madhara yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kupitisha mkojo na via vya uzazi kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa moyo.
Posti hii inaelezea kuhusiana na mambo hatari yanayosababisha ugonjwa wa moyo. Soma Zaidi...

MARADHI YA MOYO: KUPALALAIZI, PRESHA, SHAMBULIZI LA MOYO, Atherosclerosis;
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dalili za ngozi kuwasha.
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa kuhusiana na dalili za ngozi kuwashwa. Soma Zaidi...

Sababu za Uvimbe wa tishu za Matiti kwa wavulana au wanaume
posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe wa tishu za matiti kwa wavulana au wanaume, unaosababishwa na kutofautiana kwa homoni za estrojeni na testosterone. Pia unaweza kuathiri matiti moja au zote mbili, wakati mwingine bila usawa. Watoto wachanga, Soma Zaidi...