Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake
NINI HUSABABISHA MAUMIVU YA TUMBO CHINI YA KITOMVU KWA WANWAKE NA WANAUME?
Watu wengi wamekuwa wakilalamikajuu ya maumivu makali ya tumbo chini ya kitomvu. Tatizo hili linaweza kuwapata wanawake na wanaume pia. Kwa upande wa wanawake tatizo hili limekuwa ni kawaida hasa wakati wa kukaribia kuingia siku zao. Kawaida maumivu haya hayana shida sana kiafya lakini ikzidi uangalizi wa dakatari unahitajika. Je na wewe ni muhusika wa maumivu haya? Makala hii itakuwa ni jibu lako.
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu. Ni katika maumivu amaboyo kwa wanaume mara nyingi huhusishwa an ngiri na kwa upande wa wanawake huhusishwa na chango hasa pale wanapokaribia kuingia katika siku zao. Makala hii itakuletea sababu za maumivu ya tumbo chini ya kitomvu kwa wanwake na wanaume.
Maumivu ya tumbo kitomvuni
Eneo hili la kitomvuni kitaalamu hufahamika kama umblical region. Eneo hili la tumbo linahusisha viungo kama tumbo la chakula, utumbo mdogo, utumbo mkubwa na kongosho. Hivi ni katika viungo muhimu sana katika mmengenyo wa chakula, na afya ya mtu kwa ujumla.
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
2. Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili.
3.Vidonda vya tumbo
Yes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum.
3. Matatizo kwenye kongosho
Huu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali.
5.Kuwa na ngriri ya henia
Ugonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-
1.Mashambulizi ya bakteria
2.Henia
3.Uvimbe
4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-
1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
2.Kuona damu kwenye choo
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Malaria ni katika maradhi yanayosumbua sana na kusababisha maradhi ya watu wengi sana duniani.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kufanya usafi wa sikio, sikio ni mojawapo ya ogani ambayo usaidia kusikia,kwa hiyo sikio linapaswa kusafishwa kwa uangalifu kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Kuvimbiwa kwa watoto ni shida ya kawaida. Kuvimbiwa kwa watoto mara nyingi huonyeshwa na kinyesi kisicho kawaida au kinyesi ngumu na kavu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.
Soma Zaidi...Saratani ya kwenye Njia ya haja kubwa ni aina isiyo ya kawaida ambayo kitaalamu hujulikana Kama saratani ya mkundu.Mfereji wa mkundu ni mirija fupi iliyo mwisho wa puru yako ambayo kinyesi hutoka mwilini mwako. Saratani ya kwenye Njia ya ha
Soma Zaidi...Wajawazito wanaposumbuliwa na ugonjwa wa UTI, dalili za UTI na namna ya Kujikinga na UTI
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa pre- eclampsia ni Ugonjwa ambao uwapata wanawake wajawazito uwapata pale mimba inapofikisha umri wa wiki ishilini, utokea pale ambapo Mama mjamzito huwa na kiwango kikubwa cha shinikizo la damu na pia kuwepo kwa protini
Soma Zaidi...Hawa ni fangasi ambao wanashambulia sana kwenye kucha za vidole vya mikonobna miguu.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo.
Soma Zaidi...