FANGASI SEHEMU ZA SIRI: DALILI ZAKE, CHANZO CHAKE NA NJIA ZA KUPAMBANA NAO
FANGASI
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.
Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Fangasi wanaweza kuathiri makwapa, vidole, sehemu za siri kwenye tumbo na maeneo mengine.
Fangasi wa sehemu za siri husababishwa na fangasi waitwao candida. Hawa wanaweza kuathiri sehemu za siri kuzungukia uume ama uke. Kunatafiti zinaonesha kuwa fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi. Japo tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha hili.
FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI DALILI ZAO KWA WANAUME
- Kuvimba kwa kichwa cha uume
- Kuwasha kwa sehemu za siri, hususan kichwa cha uume
- Uume kuwa mwekundu kwa kuchubuka ama kuvumba ama kwa mashambulizi ya fangasi hawa.
- Kuota kwa mapele na maruturutu kwenye uume
- Kuwasha uume ama kuungua moto kwa uume.
- Kutokwa na majimaji meupe kwenye uume, majimaji haya huwa na harufu mbaya.
- Maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo la ndoa.
DALILI ZA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE
- Maumivu na miwasho kwenye mashavu ya uke na sehemu ya juu ya uke
- Maumivu wakati wa kukojoa ama kufanya tendo la ndoa
- Uuke kuwaka moto kwa ndani
- Kuvimba kwa mashavu ya uke na kuwa mekundu
- Kuot mapele na maruturutu kwenye uke
- Kutokwa na majimaji kwenye uke
- Kutokwa na majimaji mazito meupe na yenye harufu mbaya kwenye uke.
WATU WALIO HATARINI KUPATA FANGASI HAWA
- Wachafu
- Kuwa na mikunjomikunjo kwenye ngozi kama kitambi
- Wenye kisukari
- Wenye HIV
- Wenye saratani
- Wenye kutumia baadhi ya madawa ya kuzuia mimba
- Wajawazito
NJIA ZA KUPAMBANA NA FANGASI HAWA
- Kuwacha kutumia madawa ya kusafishia ama kuunga uke
- Kutokuvaa nguo mbichi
- Kutokuvaa nguo za kubana hususani za mpira
- Kuwa msafi muda wowote
- Kuosha kichwa cha uume na ngozi ya govi mara kwa mara
- Kuosha uke mara kwa mara
- Kutumia pedi zilizo kavua na safi na kubadilisha mara kwa mara
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Namna ya kujikinga na VVU/UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza namna mbalimbali za kujikinga na VVU/UKIMWI
Soma Zaidi...Mie ni mwanamke ninamaumivu chini ya kitovu upande wa kushoto, na nikishika tumbo nahisi kitu kigumu upande huo huo wa kushoto... hii itakua ni nini?
Je unasumbuliwa na maumivuvya tumbo chini ya kitovu upande wa kushito. Post hii itakuletea sababu za maukivubhayo na nini ufanye.
Soma Zaidi...Madhara ya fangasi.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya fangasi za ukeni kwa kawaida tunajua kubwa fangasi zikiingia kwenye uke usababisha madhara mbalimbali ambayo mengine yanaweza ya kudumu na mengine ya mda kama yametibiwa mapema.
Soma Zaidi...Vidonda vya tumbo husababishwa na nini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu visababishi vya vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Ufahamu Ugonjwa wa hepatitis B
Hepatitis B Ni maambukizi ya ini ambayo yamekuwa sugu kuanzia mwezi na kuendelea.
Soma Zaidi...Ujue ugonjwa wa kuishiwa na damu
post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuishiwa damu kwa kitaalamu huitwa(Anemia) ni ugonjwa wa kuishiwa na damu mwilini na kusababisha maisha ya mtu kuwa hatarini
Soma Zaidi...