Sababu za mdomo kuwa mchungu
Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu.
KWA NINI MDOMO UNAKUWA MCHUNGU?
Umeshawahi kuamka asubuhi ukiwa na ladha chungu sana ya mdomo, na je hali hii ulishawahi kudumu nayo kwa muda wa masaa kadhaa?. bila shaka ungependa kujuwa sababu inayopelekea kutkea hali hii. Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakujuza sababu kuu za kuwa na ladha chungu ya mdomo, na nini kifanyike. Endelea kusoma makala hii hadi mwisho. Ila ningependa utambuwe kuwa mdomo kuwa mchungu mara nyingi sio shida sana ya kiafya kiasi cha kuhitaji dawa ama kumuona daktari. Endapo shida itaendelea hapo fanya maamuzi ya kuonana na daktari
Mdomo kuwa mchungu mara nyingi sio maradhi. Hali hii hutokea na kuondoka yenyewe ndani ya masaa machache. Mara nyingi hutokea wakati wa asubuhi ama unapotoka kulala. Hali hii pia huwapata wagonjwa. Hali hii wakati mwingine inakuwa ni dalili ya maradhi. Kama utaona mdomo wako unaendelea kuwa mchungu kwa muda mrefu onana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
Ni nini husababisha mdomo kuwa mchungu?
1.Mdomo kutokuwa msafi. Hii ni kawaida wakati umelala mdomo bakteria waliokuwa wapo mdomoni wanaendelea kufanya kazi yao, kula mabaki ya chakula na kuendelea kuzaliana. Kumbuka mate yana kazi ya kusafisha mdomo,lakini wakati umelala mate hayawezi kufanya kazi hii kwani huwezi kuyatoa. Hivyo uchafu huendelea kujizalisha bila ya kutolewa. Hali hii inaweza kusababisha mdomo kuwa mchungu unapoamka.
Vyema usile kitu muda huu, kabla ya kupiga msaki. Safisha kinywa vyema ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya muda mchache. Pia kama ulitoka kulala baada ya kutema mate kwa muda mchache yaani baada ya mdomo kujisafisha hali hii inaweza kuondoka bila ya wasi wala hakuna ulazima wa kupiga mswaki, kwani mdomo una sifa ya kujisafish awenyewe kwa kutumia mate.
2.Matumizi ya madawa ya antibiotics au antidepressants. Dawa hizi pindi mdu anapozitumia hufyonzwa ndani ya mwili na kutolewa kwa kupitia mate na kusababisha mate kuwa machungu. Mfano wa dawa hizi ni:-
A. Tetracycline
B.Gout medication kama allopurinol na lithium
C.Madawa yanayotumika kutibu maradhi ya moyo.
Baada ya kuacha kutumia dawa hizi ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya siku chache. Pia unaweza kunywa juisi ya vitu vichachu kama hali itaendelea kukusumbuwa.
3.Ujauzito, hali ya mdomo kuwa mchungu ama kuwa na ladha ya chuma kwa wajawazito ni kawaida na hali hii kutaalamu hufahamika kama dysgeusia ama metallic taste. Hutokea kwa uda wa siku kadhaa kisha huondoka. Baadhi ya wajawazito wanapata ladha ya pesa, yaani kama ulishawahi kuweka mdomon hela ya sarafu, ile ladha unayoipata ndio ambayo huwapata baadhi ya wajawazito.
4.Kama unatumia dawa za kuongeza vitamini, unaweza kupata ladha hii. Kuna baadhi ya dawa za vitamini zina madini mengi ya metali. Madini hayokama zinc, shaba, chuma na chromium. Kama dawa hiyo ina madini haya inaweza kubadili ladha ya mdomo na kuwa chungu
5.Ni dalili ya maradhi ya ini. Kama ini lako halifanyi kazi vyema ama lina matatzo, mwili utakuwa na kiasikikubwa cha ammonia ambayo ni sumu. Hatimaye kubadili ladha ya mdomo.
6.Mashambulizi ya kwenye mfumo wa upumuaji. Wakati mfumo wa upumuaji unapokuwa katika mashambulizi ya bakteria ama virusi au fangasi, inaweza kuathiri ladha ya mdomo.
7.Kama umecheuwa, hali hii inaweza kupelekea kubadilika kwa ladha ya mdomo
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 ai web app 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Je vidonda vya tumbo husababisha maumivu mpka upande mmoja wa mgongoni !?
Ni ngumu kujuwa vidonda vya tumbo uhakika wake bila ya kupata vipimo. Unajuwa ni kwa nini, ni kwa sababu maumivu ya tumbo ni dalili ya shida nyingi za kiafya kama ujauzito, mimba, typhod, na shida kwenye unfumo wa chakula.
Soma Zaidi...Zijue dalili za maambukizi ndani ya sikio na madhara yake
Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu inayotumiwa kwa ajili ya kusikia, Kuna wakati mwingine hushambulia na bakteria na virusi
Soma Zaidi...Maambukizi ya tezi za mate
Psti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi ya tezi za mate ambao hujulikana Kama MABUSHA (mumps) ni maambukizi ya virusi ambayo kimsingi huathiri tezi mojawapo ya jozi tatu za tezi za mate zinazotoa mate, zilizo chini na mbele ya masikio
Soma Zaidi...Dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanawake
Somo hili linakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanawake
Soma Zaidi...Athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa wajawazito
Post inahusu zaidi athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa wajawazito au ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri.ugonjwa huu uleta madhara kwa wajawazito kama tutakavyoona
Soma Zaidi...