DALILI ZA MINYOO Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote.
DALILI ZA MINYOO
Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-
1.Kichefuchefu
2.Kukosa hamu ya kula
3.Maumivu ya tumbo
4.Kupungua uzito
5.Uchovu wa viungo
6.Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
7.Kuona minyoo kwenye kinyesi.
8.Kuona damu kwenye kinyesi
9.Tumbo kujaa
Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-
1.minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
A.Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
B.Kuwa na alegi
C.Kuwa na homa
D.Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa
2.minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
A.Kuwashwa
B.Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
C.Kuwa na uchovu wa hali ya juu.
3.minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
A.Kupata homa
B.Kuvimba kwa uso
C.Maumivu ya misuli na kuchoka
D.Maumivu ya kichwa
E.Kutokupenda kupigwa na mwanga
F.Matatizo katika macho (conjuctivist)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Kuziba kwa utumbo ni kuziba kwa chakula au kimiminika kisipite kwenye utumbo mwembamba au utumbo mpana (colon). Kuziba kwa matumbo kunaweza kusababishwa na mikanda ya nyuzi kwenye fumbatio ambayo huunda baada ya upasuaji, mifuko iliyovimba au iliyoambuk
Soma Zaidi...Post hii inahusu dalili za uvimbe kwenye kinywa ambapo kitaalamu hujulikana Kama oral candidiasis Uvimbe kwenye kinywa husababisha vidonda vyeupe, kwa kawaida kwenye ulimi au mashavu ya ndani. Wakati mwingine uvimbe kwenye kinywa huweza ku
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa mbalimbali ambayo watoto chini ya miaka wanaweza kuyapata kiurahi.
Soma Zaidi...Pisti hii inahusu zaidi dalili za mtoto mwenye Maambukizi ya ugonjwa wa Dondakoo, tunajua wazi kuwa ugonjwa huu uwashambulia hasa watoto wadogo ambao wako chini ya miaka mitano, kwa hiyo zifuatazo ni baadhi ya Dalili zinazoweza kujitokeza kwa watoto hawa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye nephroni, ni njia zinazotumika kuzuia maambukizi kwenye nephroni
Soma Zaidi...Post hii itakwena kukufundisha kuhusu historia fupi ya Ukimwi na matibabu yake. Ni wapi wapo hatarini kupata maambukizi na ni kitu gani wafanye?
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha ishara na dalili za Saratani ya utumbo mdogo
Soma Zaidi...Ugonjwa huu hupelekea kuvimba kwenye ini yako ambayo hutokea wakati mfumo wa kinga ya mwili wako unaposhambulia ini lako.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea pale ambapo Ugonjwa wa ngiri unaposhindwa kutibiwa mapema.
Soma Zaidi...