DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo.
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO
Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Basi HIV nayo ina hatua zake mpaka kuwa UKIMWI.
DALILI ZA MWANZO ZA HIV AMA UKIMW
Dalili hizi huanza kuonekana kuanzia wiki mbili mpaka nne na wakati mwingine mpaka sita toka kuingia mwilini. Mara chache sana huweza kuonekana mwanzoni mwa wiki ya kwanza. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuona dalili zifuatazo:
1.kufimba kwa tezi za kwenye makwapa, mapaja na shingo
2.Homa
3.Uchovu
4.Kuharisha
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Pumzi kutoka kidogodogo
8.Mafua
Dalili hizi pia zinaweza kuhusiana na maradhi mengine, hivyo inaweza kuwa vigumu kujuwa nini chanzo zaidi. Wengi katika wanaopata HIV wametaja kuwa kuvimba kwa tezi ndio dalili pekee walioweza kuopata mwanzoni mwa kuathirika kwao. Wengine wanataja mafua kuwa ndio dalili yao ya kwanza.
Baada ya kipindi hiki kupita mgonjwa hatapata dalili yeyote ile. Hiki ni kipindi hatari sana kwani mtu hataweza kujijua kama ameathirika. Kipindi hiki kinaweza kudumi mpaka miaka 10. katika kipindi hiki virusi vinaendelea kuathiri seli za mwili. Baada ya mwili kuwa umeathirika sana na kudhoofu mtu ataanza kupata dalili za UKIMWI.
DALILI ZA UKIMWI
1.kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kupata homa za mara kwa mara na kuhisi baridi
3.Kikohozi
4.Kushinwa kupumua vyema
5.Madoa madoa kwenye ulimi na mdomoni
6.Maumivu ya kichwa
7.Uchovu usiokuwa na sababu na usioisha
8.Kutokuona vyema
9.Kupungua uzito
10.Mapele na ukurutu kwenye ngozi
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata UTI, ni watu ambao wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa UTI kwa sababu ya mazingira mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo dalili zake na namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo hilo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kufanya usafi wa sikio, sikio ni mojawapo ya ogani ambayo usaidia kusikia,kwa hiyo sikio linapaswa kusafishwa kwa uangalifu kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye viungo, ni ugonjwa unaowapata na wanaume ila kwa wanaweza unaowapata sana ukilinganisha na wanaume.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazopelekea kukosa choo ,yaani kinyesi kuwa kigumu au kukosa kabisa choo.
Soma Zaidi...Maumivu ya kifua huja kwa aina nyingi, kuanzia kuchomwa na kisu hadi kuuma kidogo. Baadhi ya Maumivu ya kifua yanafafanuliwa kama kuponda kuungua. Katika baadhi ya matukio, maumivu husafiri juu ya shingo, hadi kwenye taya.
Soma Zaidi...Poliomyelitis ni kuvimba kwa suala la kijivu la uti wa mgongo na wakati mwingine sehemu ya chini ya ubongo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo UKIMWI hutokea
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu ni madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mgonjwa pale ambapo matibabu yanapokuwa hayatolewi kwa mgonjwa wa maumivu chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za Maambukizi kwenye mifupa, ni dalili ambazo ukionyesha kwa mtu mwenye Maambukizi kwenye mifupa.
Soma Zaidi...