Njia za kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu

Post hii inahusu Zaidi njia mbali mbali ambazo uweza kitumiwa na wataalamu ili kuweza kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

Njia za kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

1. Njia ya kwanza ni Kwa kutumia mionzi ambayo Kwa kitaalamu huitwa x- ray, mgonjwa huingizwa kwenye chumba maalumu na kuweza kuchukua picha kwenye sehemu ya kifua na pia baada ya kuchukuliwa picha uweza kusomwa na wataalamu ili kuweza kugundua kama Kuna tatizo hili la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

 

2. Njia nyingine ni Kwa kutumia kifaa Fulani ambacho Kwa kitaalamu huitwa bronchoscopy,ni kutoa sehemu ya usaha ili kuweza kupima kama Kuna usaha kwenye mapafu,Kwa kawaida kifaa hicho uingizwa kwenye mfumo wa hewa na kuangalia kama usaha upo na upo sehemu gani na hatimaye njia za kupitoa uendelea.

 

 

 

3. Pia kutumia maji maji na damu kutoka kwenye sehemu ya mapafu ili kuweza kuangalia ni mdudu gani ambaye yumo kwenye mapafu Kwa kufanya hivyo inakuwa rahisi kugundua ni mdudu gani aliyeshambulia kwenye mapafu na baada ya kufanya hivyo wanaweza kupata dawa ya kuweza kutibu hao wadudu Kwa kuangalia kama ni virus, bakteria au wadudu wengine wale.

 

 

 

4.vile vile tunaweza kugundua tatizo hili Kwa kutumia damu Kwa kitaalamu full blood picture, unaweza kukuta seli nyeupe za damu ziko juu sana na kuona kwamba hapa Kuna maambukizi.

 

 

5. Kwa kutumia kifaaa Kwa kitaalamu huitwa stereoscope ili kuweza kusikiliza sauti kwenye mapafu , mgonjwa kama anapumua vibaya ni wazi kwamba Kuna Maji maji au usahaa usio wa kawaida kwenye mapafu.

 

 

 

6. Tunaweza kutumia pia makohozi ili kuweza kutambua rangi yake,kama rangi ni nyeusi moja Kwa moja tunafahamu kwamba ni usaha kwenye mapafu.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/11/09/Thursday - 09:40:45 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 562


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-