Bipolar disorder ni hali ya afya ya akili inayohusisha mabadiliko makubwa katika hisia, nishati, na shughuli za kila siku za mtu. Dalili za bipolar disorder zinaweza kuwa kwenye kipindi cha mania na kipindi cha unyogovu, zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa bipolar.
Ugonjwa huu wa bipolar una sehemu tofauti ambapo mgonjwa wa akili anaweza kuwa na furaha kubwa,kukasilika ghafla ,yaani Kwa ujumla anakuwa na pande mbili yaani furaha na huzuni na jinsi tutakavyozifafanua kama ifuatavyo.
Kipindi Cha furaha (mania)
1.Furaha kupita kiasi au msisimko usio wa kawaida, Hasira au kutokuelewana kwa urahisi,Kwa mda huu mgonjwa anaweza kuwa na furaha sana ,akachangamka akacheka ila Kwa mda mfupi tu akawa na Hasira na kutoelewana na mtu yeyote yule.
2.pia na hisia za kuwa na nguvu zisizo za kawaida.
Kwa mfano uongezeka kwa shughuli na uwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja pia mgonjwa anaweza kufanya shughuli zote Kwa ukamilifu na Kwa wakati mmoja zote zikaisha na katika kipindi hiki mgonjwa hapendi kuingiliwa kwenye shughuli zake.
3.kufanya mambo haraka haraka
Akili ya mgonjwa inakuwa inaamua mambo Kwa haraka ambapo mtu anaweza kuhamasika na mawazo mengi kwa wakati mmoja na kuwa na mipango mingi Kwa wakati mmoja,pia hali hii ikimpata mtu akiwa kiongozi wa kundi kabla hajagundulika watu wanapata shida sana Kwa sababu atakuwa na mipango mingi ya haraka Kwa wakati mmoja.
4.Kupuuza kutokea Kwa hatari.
Kutenda bila kufikiri matokeo, kama vile kuwekeza pesa nyingi au kushiriki katika tabia zisizo za kawaida ambazo zinaweza kuleta hatari Kwa mgonjwa,yaani Kila kitu anaweza kufanya bila kufikilia matokeo ya kitu anachokifanya,haogopi mtu,haogopi wakati wa hatari yeye kauli yake ni kwamba Kila kitu ni kawaida tu.
5.Kujiona Mtu anayefaa na mkubwa kuliko yeyote yule.
:Kujiona kuwa na uwezo au nguvu zaidi kuliko kawaida, au kuwa na dhana ya umbo kubwa zaidi wa kibinafsi,yeye anaona anafahamu Kwa Kila kitu bila yeye hakuna kitu ambacho kinaweza kufanya Kwa hiyo anao uwezo wa kuamrisha Kila mtu.
6.Kukosa Usingizi.
Kulala masaa machache tu au kutokulala kabisa kwa sababu yeye anajiona ni mweye nguvu Kwa hiyo atafanys kazi mda wote na pia kuzunguka huku na huku pia hatulii Kwa sababu anaona bila yeye hakuna kitu kinachoweza kufanyika hali ambayo anaona kulala ni kupoteza mda.
Kipindi cha Unyogovu(depression)
1.kuwa na huzuni.
kukatishwa tamaa, au hisia za kukosa thamani,hali hii umefanya kujisikia kwamba haifai na pia anachokifanya hakina maana hali inayomsukuma kukata tamaa.
2.Kupoteza hamu ya kufanya shughuli nyingine za kijamii
Kukosa hamu ya kufanya mambo ambayo kawaida yanawafurahisha na pia anashindwa kunifanyia chochote hata mambo ya kawaida anashindwa kabisa.
.3.Kupunguza au kuongezeka Kwa Uzito.
Mabadiliko makubwa katika uzito kutokana na mabadiliko ya hamu ya chakula Kwa sababu anaweza kuamua kula sana na uzito unaongezeka au anaweza kukosa kabisa hamu ya chakula na uzito ukapungua.
4.Kujisikia uchovu
, kuchoka au kuchoka bila sababu .Kipindi cha Unyogovu Kwa hiyo katika kipindi hiki utamkuta jamaa kalala mda wote ukimuuliza kulikoni anakwambia amechoka na huku hajafanya kitu.
.kwa hiyo huyu mgonjwa tunafahamu wazi kwamba ana vipindi viwili ,Kipindi cha unyogovu na kipindi cha maania Mchakato wa muda mrefu wa mabadiliko ya hisia kabla ya kuingia kwenye kipindi cha mania au unyogovu.Msaada na Matibabu:Ni muhimu kutafuta msaada wa kitaalam kama unadhani una dalili za bipolar disorder. Matibabu yanaweza kujumuisha dawa na Terapia ya kuzungumza ili kuweze kumsaidia mgonjwa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inaenda kuzungumzia zaidi kuhusiana na mimba zinazoharibika . mimba huweza kuaribika au kutoka anzia miezi 3 na kuendelea .
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa upele na matatibabu yake, ni ugonjwa unaosabavishwa na mdudu kwa kitaalamu huitwa mites sarcoptes scrabie mdudu huyu usababisha miwasho kwenye ngozi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa vericose veini, hili ni tatizo ambalo utokea katika mzunguko wa damu hasa kwenye miguu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kushindwa kushuka kwa makende kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye skolatumu(scrotum).
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za vidonda vya tumbo sugu
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalilili za kukosa oksijeni ambalo kitaalamu hujulikana Kama apnea.kukosa oksijeni ni tatizo ambapo kupumua kwako hukoma na kuanza unapolala.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa ,kwa kawaida Ugonjwa huu utokea kuanzia kwenye wiki ya pili mpaka mwaka mmoja na hapo Ugonjwa unakuwa bado haujaonesha Dalili na Dalili zikishaonekana ni vigumu kutibika.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo;
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...