Navigation Menu



image

VIRUSI VYA KORONA AU CORONA (CORONAVIRUS)

Virusi vya korona ni katika aina za virusi ambavyo asili yake ni kutoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu.

VIRUSI VYA KORONA AU CORONA (CORONAVIRUS)

VIRUSI VYA KORONA au CORONA (CORONAVIRUS)

virusi vya corona
Virusi vya korona ni katika aina za virusi ambavyo asili yake ni kutoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu. Virusi hivi vipo katika aina nyingi. Na vimeshatambulika toka zamani. Na sasa aina nyingine ya virusi hivi vya corona vimejulikana na mpaka sasa vimesababisha maafa na mamia ya watu wameathirika.


<

NI NINI VIRUS VYA CORONA?
Corona ni neno la kilatini lenye maana ya taji (crown). Na hii ni kutokana na kuwa virusi hivi vina umbo hili na taji (crown) ambayo kwa kilatini ndio corona. Virusi hivi husababisha matatizo katika mfumo wa upumuaji. Virusi hivi vinaweza kusababisha maradhi kama SARS yaliyogundulika kwa mara ya kwanza China mwaka 2003 na kuuwa zaidi ya watu 800, maradhi ya MERS yaliyogunduliwa saud arabia mwaka 2012 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 850 na 2400 kuathirika.


<

NINI ASILI NA CHANZO CHA VIRUS HIVI?
Asili ya virusi hivi ni kutoka kwa wanyama kuja kwa watu. Yaani virusi hivi vinapatikana kwenye wanyama kama ngamia, popo, samaki, ngombe na wengineo. Kisha virusi hivi husambaa kutoka kwa wanyama kwenda kwa watu. Baada ya hapo kutoka kwa mtu kwend kwa mtu kwa njia ya hewa ama kugusana. Tafiti zilizofanyika nchini china ambapo ndipo chimbuko la ugonjwa wa virusi vya corona unaotambulika kama 2019-nCoV inathibitishwa kuwa asili ya virusi vya kurona vilivyosababisha ugonjwa wa 2019-nCoV kuwa virusi vimeanzia kwenye vyakula vya baharini, yaani samaki.


<

NI YAPI MARADHI YANAYOSABABISHWA NA VIRUSI VYA CORONA
Mpaka sasa kuna maradhi matatu yananayojulikana kuwa yamesababishwa na virusi vya corona. Na maradhi haya yote huathiri mfumo wa upumuaji na kusababisha mgonjwa kuumwa na homa, kukohoa pamoja na kushindwa kupumua vizuri. Maradhi hayo ni kama:-
A. SARS uligundulika China mwaka 2003 na kuuwa watu 800
B. MERS uligundukika Saud Arabia na kuuwa watu 850
C. 2019-nCoV mpaka kufikia 3/2/2020 umeua watu 361


<

AINA YA VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA MERS
MERS ni neno linalimaanisha Middle East Respiratory Syndrome Coronavirus (MERS-CoV) kwa mara ya kwanza virusi hivi vimegunduliwa mwaka 2012 katika nchi ya Saud Arabia na vilisababisha madhara kwenye nchi zaidi ya 25 ikiwemo Marekani. Miongoni mwa dalili za virusi hivi ni homa kali, kukohoa pamoja na kushindwa kupumua.


<

AINA YA VIRUSI CORONA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA SARS
SARS ni ufupisho wa maneno Severe acute respiratory syndrome (SARS-CoV) huu ni ugonjwa katika mfumo wa upumuaji unaosababishwa na virusi vya corona. Kwa mara ya kwanza virusi vya corona wanaosababisha ugonjwa huu waligundulikwa mwaka 2003. baada ya hapo ugonjwa ulisambaa katika nchi za marekani, ulaya na bara la asia.


<

VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA 2019-nCoV
2019-nCoV ni ufupisho wa maneno 2019 Novel Coronavirus huu pia ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona unaoathiri mfumo wa upumuaji. Ugonjwa huu umeibuka china na kusababisha maafa na kuathiri watu wengi. Ugonjwa huu una dalili kama homa, kukohoa na kushindwa kupumua. Unaambukizwa kwa njia ya hewa na kugusana. Ugonjwa huu hutokea siku mbili mpaka 14 toka kuvipata virusi hivi.


<

UGONJWA WA VIRUSI VYA CORONA UJULIKANAO KAMA 2019-nCoV
Kina mengi bado hayajulikani kuhusu ugonjwa huu na bado wataalamu wa afya wanazidi kuuchunguza ugonjwa huu. Ugonjwa huu husambazwa zaidi kwa njia ya hewa pindi mgonjwa anapopiga chafya ama kukohoa. Unaweza kupata virusi hivi kwa umbali wa futi sita toka kwa mgonjwa. Pia unaweza kuupata kwa njia ya kugusana.


<

Kwa sasa hakuna chanjo ya kuzuia ugonjwa huu. Njia salama kwa sasa ya kujikinga na ugonjwa huu ni kuwa mbali na muathirika wa ugonjwa huu. Pia zipo njia ambazo zimeelekezwa, njia hizi husaidia kujikinga na maradhi yanayoambukizwa kwa kugusana kama haya ya corona. Njia hizo ni kama:-
A. Osha mikono yako kwa sabuni baada ya kutoka chooni, baada ya kupinga kua yako, kabla ya kula, baada ya kupiga chafya au baada ya kukohoa. Uoshe kwa maji ya kuchirizika angalau kwa muda wa sekunde 20.
B.Kama maji yatakosekana kuna dawa za kuoshea zenye alcohol, ni njema kutumia endapo utakosa maji na sabuni
C.Jiepushe kugusa macho, pua na mdomo kwa mkono mchafu
D.Ukiwa mgonjwa bakia nyumbani
E.Unapokwenda kwenye maeneo hatarishi ziba mdomo na pua yako kwa mask ama na unapopiga chafya ama kukohoa jizibe kwa kitambaa ama nguo na si kwa mkono.


<

Pia kwa sasa hakuna matibabu maalumu ya virusi hivi. Waathirika wanapewa tiba mbadala za kupunguza athari hizo za ugonjwa. Pia kwa wagonjwa waathirika zaidi tiba maalumu ya kulinda viungo vya ndani hutolewa.


<

ATHARI ZA UGONJWA WA 2019-nCoV
Mpaka kufikia jumatatu ya tarehe 3 mwezi wa pili mwaka 2020 yapata watu 361 wamefariki kwa ugonjwa huu na kuacha waathirika maeflu. Hii inaonesha asilimia 2 tu ya waathirika ndio wamefariki. Hii ni tofauti na ugonjwa wa MERS ambao karibia robo ya waathirika walifariki. Na mpaka kufikia tarehe hiyo tajwa hapo juu 3/2/2020 watu wapatao 2,110 wapo katika hali mbaya.



                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 609


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Ugonjwa wa Uharibifu wa seli nyekundu za damu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na was Uharibifu wa seli nyekundu za damu ambapo hujulikana Kama Ugonjwa wa Hemolytic uremic (HUS) ni hali inayotokana na uharibifu usio wa kawaida wa seli nyekundu za damu mapema. Mara tu mchakato huu unapoanza, seli nye Soma Zaidi...

Samahan naomb kujua staili za tendo la ndoa
Post hii inakwenda kujibu swali la muulizaji. Kuhusu syyle za tendo la ndoa Soma Zaidi...

Njia za kusambaa kwa ugonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo (Peptic ulcers)
Vidonda vya tumbo ni vidonda vilivyo wazi vinavyotokea kwenye utando wa ndani wa umio, tumbo na sehemu ya juu ya utumbo wako. Dalili ya kawaida ya Peptic ulcer ni maumivu ya tumbo. Vidonda vya tumbo ni pamoja na: Vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani Soma Zaidi...

Yajue magonjwa ya jicho
Posti hii inahusu zaidi Magonjwa ya jicho,ni Magonjwa ambayo ushambulia sehemu mbalimbali za jicho kwa mfano kwenye retina,kuaribu mishipa ya retina ,macho kuwa makavu na pia mtoto wa jicho, hali hii ya magonjwa ya macho Usababisha madhara mbalimbali kama Soma Zaidi...

Dalili za kifua kikuu kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kifua kikuu kwa watoto,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto pindi wanapopata Maambukizi ya kifua kikuu. Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya viungo na viungo kuwaka moto nini sababu zake
Soma Zaidi...

Sababu zinazoweza kumfanya figo kuharibika.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kufanya figo kuharibika.hili ni janga ambalo linawakumba Watu wengi siku hizi na kusababisha kupoteza maisha kwa wagonjwa wa figo hasa hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kulipia hela ya kusafishia figo. Soma Zaidi...

Tatizo la Kikohozi Cha muda mrefu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kikohozi cha muda mrefu ni zaidi ya kero. Kikohozi cha muda mrefu kinaweza kuharibu usingizi wako na kukuacha unahisi uchovu. Matukio makali ya kikohozi cha muda mrefu yanaweza kusababisha kutapika, kizunguz Soma Zaidi...

Bawasili usababishwa na nini?
Posti hii inahusu zaidi visababishi vya ugonjwa wa Bawasili,kuna watu wengi wanapenda kujua kabisa chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii na kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu visababishi vya Bawasili. Soma Zaidi...

Aina za kifua kikuu.
Posti hii inahusu zaidi aina mbili za kifua kikuu, aina ya kwanza ni ile ya kawaida ambayo ushambulia mapafu na aina ya pili ni ile ambayo ushambulia sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye limfu node, kwenye sehemu za moyo, kwenye uti wa mgongo, kwen Soma Zaidi...

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k
Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende. Soma Zaidi...