Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo.
Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo. Lakini kabla ya kutokea kifo malaria huanza kwa kuathiri maeneo nyeti sana ya kiafya na hivyo hupelekea athari kubwa ambazo huleta kifo. Hebu tuone maeneo ambayo malaria hushambulia:-
Ubongo, vimjidudud vya malaria vinapoingia kwenye mfumo wa damu huanza kushambulia seli hai nyekundu za damu. Kupitia damu vijidudu hivi vinaweza kuingia kwenye ubongo na kusababisha kuziba kwa vimishipa vijidogo ndani ya upongo. Vimishipa hivi ndivyo hupeleka virutubisho na hewa kwenye ubongo. Hali hii inaweza kumfanya mgonjwa achanganyikie na kupoteza fahamu kabisa.
Ini na figo, vijidudu hivi vinaweza kusababisha ini na figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, ama tena kufa kabisa. Endapo hali hii ikitikea basi itakuwa ni athari kubwa sana katika afya ya mtu husika.
Mapafu, endapo malaria haitatibiwa na ikiendelea kuwepo mwilini inaweza kusababisha kujaa kwa majimaji kwenye mapafu. Hali hii inaweza kusbabisha mgonjwa kushindwa kupumua kwa ufanisi. Endapo hili litatokea itakuwa ni katika athari mbaya sana za malaria.
Damu, kwakuwa vijidudu hivi hushabulia seli hai nyekundu za damu, na seli hizi ndizo hubeba hewa ya oksijeni na kuisambaza mwilini. Hivyo malaria inaweza kusababisha upungufu wa hewa ya oksijeni mwlini na kusababisha ugonjwa unaotambulika kama anaemia.
Wakati mwingine malaria inaweza kuwa kali zaidi na kusababisha sukari kushuka, hali hii kitaalamu inajulukana kama hypoglycaemia. Na ni katika hali mbaya sana kwani mgonjwa anaweza kupoteza fahamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.
Soma Zaidi...'UTI (urinary tract infection) no ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya husababishwa na bacteria, fangasi,na virus. Pia unaweza athiri rethra, kibofu Cha mkojo na figo.lakini Mara nyingi UTI huathiri Hadi mfumo wa uzazi na w
Soma Zaidi...Fangasi na Aina zao Fangasi wa kwenye kucha Fangasi wa Mapunye Fangasi aina ya candida Fangasi wa Mdomoni na kooni Fangasi wa kwenye uke Fangasi wanaoshambulia mfumo wa damu na ogran kama moyo, figo n.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kwa mtu ambaye ana tatizo kwenye mishipa ya retina,ni tatizo ambalo uwakumba wafu wengi wenye matatizo ya kisukari.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kichaa cha mbwa ni virusi hatari vinavyoenezwa kwa watu kutoka kwa mate ya wanyama walioambukizwa. Virusi vya kichaa cha mbwa kawaida hupitishwa kwa kuuma.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya?
Soma Zaidi...Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa.
Soma Zaidi...