Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV
Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani
VVU na UKIMWI ni mzigo mzito wa siri ambao watu wengi hawataki kutoa siri zao. Hii hupelekea kukaa muda mrefu akiwa na VVU ana UKIMWi bila hata kutumia dawa. Ni athari zipi anazipata. Hili hana haja nalo. Mwisho wa siku anafikia katika hatuwa ambao ni ngumu kurudi katika hali ya kawaida na hatimaye ni kifo.
Je unasubiliwa na mawazo kama umeathiria? Ni muda gani naweza kuishi na VVu na UKIMWI bila ya kupoteza maisha. Je ni zipi hasa dalili za kwanza kama una VVU na UKIMWI. Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakwenda kujibu maswali hayo na swali letu kuu lisemalo “ni muda gani naweza kuishi na VVU na UKIMWI bila hata ya kutumia dawa za ARVs?
Dalili za VVU na UKIMWI huweza kujitokeza katika hatuwa kuu tatu. Katika hatuwa hizo tutaendelea kuona je ni muuda gani mtu anaendelea kuishi katika hali hizo bila ya kutumia dawa za ARV?
1.Katika hatuwa ya kwanza wiki ya 2 mpaka ya 4 baada ya kuathirika.
Hii ni hatuwa ya kwanza, punde baada ya kuathirika yaani kupata VVU. Hapa mwanzoni mtu atahidi dalili ambazo zinatokea wiki ya pili mpaka wiki ya nne. Kwa baadhi ya watu inaweza kufika mpaka wiki ya 6. katika kipindi hiki mgonjwa atona dalili kadha zitakazoonyeshwa hapo chini:-
Dalili za VVU ndani ya mwezi mmoja toka kuathirika
1.Homa
2.Maumivu ya viungo na misuli
3.Uchou
4.Kutokwa na jasho jingi usiku
5.Kutokwa na upele au ukurutu kwenye ngozi
6.Kutokwa na vidonda vya mdomo
7.Kuwashwa na koo ama vidonda vya koo
8.Kuvimba kwa tezi za limfu kwenye mapaja (mitoki) kwenye makwapa na kwenye shingo (tonsils)
9.Kichefuchefu na kutapika
Katika kipindi hiki virusi huendelea kuzaliana kwa kasi sana, na kujirundika kwa wingi sana kwenye damu kuliko maeneo mengine. Kipindi hiki huchukuwa wiki 2 mpaka nne ama 6 kwa wastani ni mwezi mmoja. Amam mmoja na nusu. Baada ya hapa mtu hatahisi dalili zingine za VVU wala UKIMWI. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuambukiza wengine kwa urahisi.
2.Katika hatuwa ya pili kutoka kwezi mmoja na kuendelea.
Katika kipindi hiki virusi vinaanza kujichimbia ndani zaidi kwenye mwili. Uwingi wa virusi unasambaa maeneo mengine ya mwili na kuendelea kuambukiza wengine. Hatuwa hii mgonjwa kama hatatumia dawa za ARV anaweza kuishi mpaka miaka 10 ama zaidi ya hapo. Endapo mtu atatumia dawa virudi vitaweza kuzuiwakujizalia na hatimaye kupunguwa mwilini na vinawez akufikia katika hatuwa mabayo havionekani kabisa, ila mtu ataendelea kuwa muathirika, na ataendelea kutumia dawa.
Katika hatuwa hii hakuna dalili maalumu za VVU zitakazojitokeza. Yaani hakuna dalili yeyote katika hatuwa hii. Hatuwa hii ni mbaya sana kwani mtu anajihisi yupo sawa kiafya na hana shida yeyote, lakini virusi vinaendelea kuharibu kinga ya mwili kidogo kidogo. Mwishoni mwa hatuwa hii mtu atakuwa kinga yake imeshuka sana. Katika hatuwa hii mi bado haambiwi ana UKIMWI ila bado ni muathirika wa VVU
3.Hatuwa ya tatu, UKIMWI.
UKIMWI hutokea pale virusi vya VVU vinapoharibu kinga ya mtu hadi kufikia CD4 200. ipo hivi; mtu mwenye afya ya kawaida katika kila kipimo kimoja seli zake za CD$ zinakuwa kati ya 500 mpaka 1500. sasa endapo zitashuka na kufika 200 mtu huyu ataambiwa ana upungufu wa kinga mwilii yaani UKIMWI, tu endapo upungufu huu umesababishwa na VVU. Katika hatuwa hii kama mtu hatatumia dawa za ARV anaweza kuishi kwa miaka 3 baada ya hapo huwenda akafariki dunia.
Dalili za UKIMWI
1.Kutokwa na jasho jingi usiku
2.Homa za mara kwa mara
3.Kifua kikavu kisichopona
4.Maradhi ya ngozi na mdomo
5.Maambukizi na mashambukizi ya mara kwa mara
6.Kuharisha kusikokoma
7.Kupunguwa uzito
Kwa nini ni muhimu kutumia ARV?
Kwa kuwa sasa umeshajuwa kuwa usipotumia dawa unaweza kuishi zaidi ya miaka 10.sasa nikujuze faida za kutumia dawa hizi:-
1.Kuzuia uzalishaji wa virusi vya UKIMWi
2.Kuongeza umathubuti wa kinga ya mwili na kurefusha muda wa kuishi
3.Kupunguza uwezekano wa kuambukiza watu wengine.
Je naweza kufanya ngono na aliyeathirika na nisiathirike?
Ndio inawezekana kabisa kwa sababu zifuatazo:-
1.Kama umetumia kinga (kondomu)
2.Kama hakukutokea muchubuko wakati wa tendo la ndoa
3.Kama mgonjwa ametumia ARV kwa muda mrefu angalau kwa miezi 6 na kutumi na hali hiyo kwa muda zaidi hata akafikia kiasi idadi ya virusi haionekani kwenye kipimo.
Dawa ya kuzuia kuathirika kwa walio hatarini zaidi.
Kuna watu wapo hatarini sana kuathirika. Kwa mfano madaktari na wakunga, muda wowote wanaweza kuathirika. Shuikrani ziwaendee wataalamu wa dawa, wametuletea dawa inayotambulikwa kwa PrEP au kwa kirefu pre-exposure prophylaxis. Hii ji dawa inayotumika kwa dharura endapo umepatwa na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukupelekea kuathirika. Dawa hii inafanya kazi ndani ya masaa 72 baada ya kupata virusi. Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii ni bora kwa asilimia 80 inaweza kuzuia kmaambukizi ya muda mfupi.
Utaratibu wa maisha kwa aliyeathirika
1.Jilinde na maambukizi
2.Punguza misongo ya mawazo
3.Tumia kondomu wakati wa kushiriki ngono
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Kula mlo kamili
6.Wacha kuvuta sigara
7.Wacha ama punguza kutumia vilevi
Umeionaje Makala hii.. ?
tambuwa chanzo na dalili za UTI na tiba yake, pamoja na njia za kupambana na UTI
Soma Zaidi...ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO Kukaa na minyoo na kutoitibu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara mengi hususani kwenye ini na maeneo mengine ya mfumo wa kumeng’enya chakula.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na matatizo ya mapigo ya moyo.Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, unaodunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza k
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia sehemu yenye maumivu, hili kugundua mahali mtu anaumia ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya mgonjwa na mhudumu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kansa, ni dalili ambazo utokea kwa mtu Mwenye tatizo la ugonjwa wa Kansa ingawa sio lazima dalili hizi kutokea tukadhani kuwa ni Kansa Ila zilizonyingi huwa ni kweli dalili za kansa.
Soma Zaidi...Baada ya kujifungua mwili wa mwanamke huwa na mabadiliko tofauti na siku za nyuma. Kwa mfano hatapatavtena hedhi, hatoweza kupata ujauzito kwa muda wa mwezi ama zaidi. Endelea na post hii ujifunze zaidi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa vipele kwenye midomo na sehemu za siri .Ni ugonjwa ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster
Soma Zaidi...Posti hii inahusu athari za maambukizi ya magonjwa ya ngono ambapo magonjwa ya ngono isipokuwa UKIMWI yanatibika .mgonjwa anashauriwa kuwahi hospitali au kituo chochote cha afya kupata matibabu mara anapoona dalili za magonjwa haya.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia za kumgundua mgonjwa wa kaswende, njia hizi utumika baada ya kuongea na mgonjwa kuhusu maisha yake hasa kujamiiana na watu mbalimbali.
Soma Zaidi...