picha

Tatizo la mapafu kuwa na usaha.

Post hii inahusu Zaidi tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,ni tatizo ambalo usababishwa na bakteria ambao uingia kwenye mapafu na kusababisha madhara na hatimaye mapafu kuwa na usaha .

Tatizo la mapafu kuwa na usaha.

1. Hili ni tatizo ambalo utoke pale bakteria wanapotoka sehemu mbalimbali za ndani ya mwili au nje ya mwili na kuingia kwenye mfumo wa hewa hali ambayo usababisha mapafu kushambuliwa na hao bakteria na kuanza kutoa usaha, na Kwa hiyo tunafahamu kabisa kazi ya mapafu Huwa ni kumsaidia katika kupumua ila yakisha shambuliwa na Hawa bakteria usababisha upumuaji Kuwa wa shida.

 2. Kuna sababu ambazo huangaliwa kama ni chanzo Cha kusababisha kuwepo Kwa hali ya kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,ni pamoja na kucheua hasa Kwa watu wenye matatizo ya meno yaliyooza, hali hii utokea Kwa sababu kwenye meno yaliyooza Kuna bakteria ambao usababisha uozo kwenye meno,Kwa hiyo mtu anapotafuna chakula na bakteria hao uwepo na kuingia tumboni pale mtu anapocheua chakula Kuna wakati wale bakteria uweza kuingia kwenye mfumo wa hewa na kuanza mashambulizi kwenye mapafu.

 

 

 

3. Pamoja na kuwepo bakteria waliotokana na mtu mwenye tatizo la kuoza Kwa meno,na wakati mwingine Ile asidi kutoka kwenye tumbo Kwa watu wanaocheua uweza kuingia kwenye mfumo wa hewa na kuanza kushambulia mapafu hali ambayo usababisha mapafu kuwa na usaha iwapo matibabu kama hayatafanyika mapema Kwa mgonjwa. Pia Kuna wakati mwingine mtu akipaliwa  na bakteria wakaingia kwenye mfumo wa hewa usababisha mapafu kuwa na usaha.

  

 

 

4. Tunapaswa kufahamu kwamba kwenye Kila sehemu ya mwili kunapaswa kuwepo Kwa bakteria wake wazuri tu ambao hawana madhara Kwa mtu, ila wakihama kutoka kwenye sehemu moja ya mwili na kwenda nyingine huweza kuleta matatizo na kusababisha hali isiyotarajiwa,Kwa hiyo bakteria wakitoka kwenye tumbo na kuingia kwenye mfumo wa hewa uleta maafa au kutoka mdomoni kuingia kwenye mfumo wa hewa uleta shida,Kwa hiyo kitendo Cha bakteria kutoka ndani au nje na kuingia kwenye mfumo wa hewa usababisha kuoza Kwa mapafu na kuleta usaha.

 

 

 

 

5. Pamoja na kuwepo Kwa bakteria kwenye mfumo wa hewa Kuna na Sababu nyingine ambazo ni pamoja na kuwepo Kwa Kansas ya mapafu,ambapo kwenye mapafu uzalishwa seli zisizo za kawaida Kwa kitaalamu huitwa abnormal sell,seli hizi zikixalushwa usababisha kuishiwa au kupungua Kwa seli za kawaida ambazo ufanya kazi kwenye mapafu na kusababisha mapafu kuoza na kuanza kutoa usaha na kushindwa kufanya kufanya kazi yake ya kawaida,hali hii ya Kansa ya mapafu inabidi kutambuliwa mapema lli kuanza matibabu Kwa sababu madhara yake Huwa ni makubwa isipotibiwa mapema.

 

 

 

6. Vile vile kuwepo Kwa uchafu au material mengine kwenye mfumo wa hewa ambayo usababishwa na vitu mbalimbali kama vile kuzalishwa Kwa tissue kwenye mfumo wa hewa au kemikali za sumu ambazo utokana mtido wa maisha wa mtu kama wale wanaovuta sigara Kwa mda mrefu ule Moshi uzalisha sumu ambao usababisha kuwepo Kwa sumu kwenye mfumo wa hewa na hivyo usababisha mapafu kuoza na utoa usaha.

 

 

 

 

7. Vile vile na wagonjwa wa kifua kikuu ambao hawatumii dawa usababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mfumo wa hewa,tukumbuke kwamba, kifua kikuu hasa hasa usababishwa na bakteria ambao ushambulia mapafu na kusababisha matatizo kwenye mfumo wa hewa, Kwa hiyo kama mgonjwa ana tatizo hilo na pia akakosa kutumia dawa za kutibu kifua kikuu anaweza kusababisha bakteria kuendelea kushambulia mapafu na hatimaye mapafu kuoza na kutoa usaha.

 

 

 

 

8. Pia na mashambulizi ya virusi na fungasi kwenye mfumo wa hewa,Kuna wakati mwingine mfumo wa hewa haushambuliwa na bakteria peke yake pengine inawezekana wakawa virus na fungasi,Kwa hiyo Hawa uweza kushambulia mfumo wa hewa na kusababisha mgonjwa kupata kikohozi Cha mda mrefu na kusababisha madhara makubwa kwenye mfumo wa hewa hatimaye kusababisha  mapafu kuoza na kuanza kutoa usaha.

 

 

 

9. Vile vile matumizi ya dawa za kupitia kwenye mishipa Kwa kitaalamu huitwa intravenous injection au iv injection,hizi dawa zikitumiwa mara Kwa mara na isivyosahihi yakifika kwenye mapafu ushambulia mapafu na kusababisha kuoza na kutoa usaha,Kwa hiyo wataalamu wa afya peke yao ndio wenye majukumu ya kuagiza dawa na jinsi ya kuzitumia ili kuepuka madhara kama haya.

 

 

 

10. Tatizo jingine ni kuwepo Kwa aleji au Kwa kiswahili kizuri ni mzio,utokea Kwa wale wagonjwa ambo Huwa na aleji kubwa na vitu mbalimbali kaama vile chakula, maua , manukato na mambo kama hayo, iwapo mgonjwa huyapata mara Kwa mara na kusababisha kutumia madawa Makali kwenye mfumo wa hewa mara Kwa mara usababisha mapafu kuharibika taratibu na hatimaye kusababisha madhara kwenye mfumo wa hewa na kuanza kutoa usaha.pia Kwa wale wenye aleji hizona hawako tayari kuanza matibabu na kusababisha maambukizi ya mara Kwa mara kwenye mfumo wa hewa usababisha tatizo hilo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

 

11. Kwa hiyo tunapaswa kuwa makini kuhakikisha kwamba tunaepuka na tatizo hili ambalo utokea kwenye mapafu Kwa kutibu kwanza tatizo la magonjwa ya kinywa Kwa sababu bakteria wengi huweza kujificha kwenye meno na ikitokea wakaenda kwenye mfumo wa upumuaji usababisha madhara makubwa mno ambayo ni pamoja na kushambulia mfumo wa hewa na kusababisha mapafu kuoza na kutoa usaha.

 

 

 

 

12. Pia tunapaswa kutumia dawa mapema pindi tunapoona dalili za kifua kikuu na kuanza dawa mara moja, Kuna wengine wanaweza  kupenda kufahamu dalili za kifua kikuu ingawa unaweza kuona dalili hizi ila usiwe na kifua kikuu ,dalili za mwanzoni ni pamoja na kukohoa wiki mbili Kwa mfululizo, kutokwa na jasho hasa wakati wa usiku,mwili kuhisi hauna nguvu pamoja na homa za mara Kwa mara,uzito kupungua Kila wakati,baada ya kuona dalili kama hizo ni vizuri kabisa kwenda hospital Kwa ajili ya matibabu ili kuweza kuepuka madhara  katika mfumo wa hewa ambayo usababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

 

13. Pia ni vizuri kabisa kutibu Kansa kwenye wakati wa hatua za kwanza Kwa sababu Kansa ya mapafu mtu  kama haijagundulika mapema na yenyewe usababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, Kwa hiyo matibabu ni mapema.

 

 

 

14. Vile vile ni vizuri kuepuka matumizi ya dawa zenye kemikali ambazo pia uweza kuleta madhara kwenye mfumo wa hewa,hasa Kwa wavutaji wa sigara zile kemikali zikiingia kwenye mfumo wa hewa utengeneza sumu ambayo uingia kwenye mapafu na kuyashambulia na kusababisha madhara kwenye mfumo wa ambao ni kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

 

15. Pia Kwa wale wanaopenda kutumia dawa za kupitia kwenye mishipa ya damu Kwa kitaalamu intravenous injection wanapaswa pasipokuwa na maagizo kutoka Kwa wataalamu wa afya nao wapo kwenye hatari ya kuambukizwa kwenye mfumo wa hewa na kusababisha mapafu kuoza na kutoa usaha,Kwa hiyo wapendwa tunapaswa kutunza mfumo wa hewa Kwa sababu mapafu yakisha shambuliwa ni hatari,Kwa sababu ya kazi yake kubwa ya kusafirisha hewa,ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya ikitokea hali isiyo ya kawaida kwenye mapafu au kwenye mfumo wa upumuaji.

 

 

 

 

 

a

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2023/11/07/Tuesday - 06:56:40 am Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 1334

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Dalili za ugonjwa sugu wa Figo.

Ugonjwa sugu wa figo, pia huitwa kushindwa kwa figo sugu, huelezea upotevu wa taratibu wa utendakazi wa figo. Figo zako huchuja taka na Majimaji kupita kiasi kutoka kwa damu yako, ambayo hutolewa kwenye mkojo wako. Ugonjwa sugu wa figo unapofikia hatua

Soma Zaidi...
Ni nini husababisha kuziba kwa Njia ya machozi

Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa kuziba kwa Njia ya machozi yaani kukosa machozi ambayo husababishwa na maambukizi.

Soma Zaidi...
Sababu kuu za maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, Tumbo la ngiri na chango

Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake

Soma Zaidi...
Dalili za madhara ya figo

Posti hii inahusu dalili za figo.figo husawazisha maji mwilini pamoja na kuchuja mkojo.

Soma Zaidi...
Dondoo muhimu ya ki afya.

Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu ya ki afya, ni maelekezo ambayo utolewa ili kuweza kuzifanya afya zetu ziwe bora zaidi na kuepuka madhara yoyote ya ki afya

Soma Zaidi...
Yaani minasumbuliwa na mgongo kuuma pia kuchoka mgongo na homa zisizo isha

Maumivu ya mgongo yanaweza kuwa ni dalili inayoonyesha tatizo fulani la kiafya ikiwemo magonjwa au majeraha.

Soma Zaidi...
Typhoid husabisha mwili kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na joint za miguu kuchoka

Dalili za typhid zinapasa kuangaliwa kwa umakini. Bila vipimo mtu asitumie dawa za tyohod, kwanu dalili za tyohid hufanana na daliki za maradhi mengi.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kujilinda na maradhi ya ini

Hapa nitakueleza namna ambavyounaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi ya ini. Kwa njia hizi unaweza kujikina wewe na wengineo na maradhi haya hatari ya ini.

Soma Zaidi...
Kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI

Soma Zaidi...
Dalili za gonorrhea - gonoria

Jifunze dalili za gonorrhea na namna inavyoambukiza, zipi athari za gonori kwa wanawae na wanaume

Soma Zaidi...