Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito, kaswende inaweza kukaa kwa mtu zaidi ya miaka mingi bila kuleta madhara ya moja kwa moja lakini kadiri ya siku zinavyokwenda madhara utokea hasa wakati wa ujauzito, madhara hayo umwadhiri mtot
1. Kaswende ni ugonjwa ambao uenezwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu huitwa Treponema pallidum ambaye kwa kawaida upitia kwenye njia ya kujamiiana kwa mtu ambaye ana ugonjwa huo akijamiiana na mtu ambaye hana ugonjwa huo,kwa kawaida wadudu hao wakiwa kwenye damu ya mama uweza kuingia kwa mtoto kupitia kwenye kondo la nyuma na kuweza kushambuliwa mtoto, ikiwa mama hatajulikanaa mapema kama ana ugonjwa huo mtoto anaweza kupata matatizo mbalimbali kama vile kuzaliwa akiwa kipofu au mtoto kufia tumboni.kwa hiyo ni vizuri kabisa akina Mama wakiwa wajawazito waweze kupima kaswende na iwapo mama akiwa na ugonjwa huo
aanze matibabu mara moja.
2. Kwa kawaida ni vizuri kabisa akina mama wajawazito wanaoanza mahudhurio ya kliniki waweze kwenda na waume zao ili nao waweze kupima kaswende kwa sababu ukimtibu Mama pekee yake na huko na baba ana ugonjwa huo unakuwa umefanya kazi bure kwa hiyo ni vizuri kabisa kupima wote na wakigundulika wana ugonjwa huo ni vizuri kabisa kupewa dawa na wote waanze matibabu ili kuweza kunusuru maisha ya mtoto, pia kuna tatizo moja ambalo utokea ikiwa wote baba na Mama wamekuja kupima na wakagundulika wote wana maambukizi ni vizuri kabisa kuwashauri kabla ya kuwapima ili watoe hali ya kuanza kuulizana kwamba ni nani aliyeleta ugonjwa huu bali wote watibiwe na kuokoa maisha ya mtoto.
3. Pia jinsi na njia ambazo uweza kusababisha kusambaa kwa kaswende kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, ya kwanza ni kufanya ngono zembe hali hii utokea pale mtu mwenye kaswende anapofanya ngono na mtu ambaye hana kaswende bila kupima afya zao na bila kutumia kondomu yaani ngono ya nyama kwa nyama, kwa hiyo watu wanashauliwa kama wanataka kufanya ngono zembe ni vizuri kabisa kupima afya zao ili kuweza kufahamu kama wana maambukizi au kama hawakuweza kupima ni vizuri kutumia kondomu, kwa hiyo jamii inapaswa kuelimika kuhusu ugonjwa huu hatari na kujihadhari kwa sababu madhara yake ni makubwa ingawa kwa bahati nzuri unatibika ila kinga ni nzuri hasa hasa vijana wanapaswa kufahamu jambo hili kwa sababu wenyewe ndio tegemeo la taifa la kesho pia ndio wapo kwenye mategemeo ya kupata watoto wenye afya nzuri sio wenye kaswende na matatizo yote yanayohusiana na mambo kama hayo.
4. Njia ya pili ambapo ugonjwa huu unasambaa ni kujamiiana na mwanaume ambaye anajamiiana na wanaume wengine,
Tunavyojua kwa sasa hali ya ulimwengu ilivyo Kuna wanaume wanaojamiiana na wanaume wengine na pia huko ana mke mwenye mimba na anategemea kupata mtoto mwenye afya nzuri, kwa njia hii pia kaswende inaweza kueneza kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanaume na kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke na pia mwanamke kama ana mimba ana asilimia zote za kumwambikiza mtoto. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuachana na njia hizi za kujamiana hasa wanafamilia kama wanategemea kupata watoto kwa sababu hali kama hiyo ni hatari kwa familia na jamii nzima kwa sababu watoto wenye ulemavu wanapatikana na pia watoto wanapoteza maisha wakiwa mimba. Kwa hiyo jamii inapaswa kuelimika na kuhakikisha wanapunguza maambukizi ya kaswende hasa kwa wajawazito.
5. Pia wanawake wenye kiwango kikubwa cha virusi vya ukimwi,
Kwa kawaida mama akiwa na maambukizi na hatumii dawa inawezekana pengine anakuwa hajui kama ana maambukizi kwa sababu hajapima. Kwa kawaida mtu akiwa na maambukizi na kinga ya mwili inashuka kwa hiyo ni rahisi kabisa kupata maambukizi ya kaswende, kwa hiyo akina mama pindi wanapopata mimba ni vizuri kabisa kwenda kupima magonjwa hatarishi kwa mtoto na pia wasiende wenyewe ila waende na waume zao,na wakigundulika kwamba wana maambukizi ni vizuri kabisa kuanza matibabu mara moja ili kulinda afya ya mtoto.
6.Wanawake wenye wapenzi zaidi ya mmoja.
Pia na hili ni tatizo unaweza kukuta mwanamkea ana familia yake ana mme wake na pia ana wapenzi wengi nje na pia anajamiiana nao bila kinga ,na kuna wakati mwingine mama anakuwa ameshatoka kliniki kupima pamoja na mme wake na kukutwa hawana maambukizi ila mama anaendelea kutembea na wanaume wengi na bila mpangilio, kwa hiyo tunawasihi akina Mama wote wakishabeba mimba watulie na mme mmoja na hata kama labda mimba hiyo imepatikana bila matarajio au mama hana matunzo anapata matunzo kutoka kwa wanaume mbalimbali ila kwa usalama wa mtoto na kuepuka kupata mtoto wa ajabu atakayekutesa maisha yako yote ni vizuri kabisa kumlinda mtoto akiwa tumboni kwa kuachana nakutembea na wanaume wengi wakati wa ujauzito na kusababisha maambukizi ya kaswende kwa mtoto.
7. Napenda kuwashauri akina Mama na baba pia kwamba kaswende inatibika pindi ukipata ugonjwa huu ni vizuri kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu na pia wazazi wanapaswa kuja madhara ya kaswende kwa mtoto ambapo mtoto anaweza kuzaliwa akiwa kipofu au na ulemavu wowote au pengine anaweza kuzaliwa akiwa mfu, na pia ugonjwa huu unaweza kukaa kwenye mwili wa mtu kwa mda mrefu kwa hiyo ni vizuri kabisa kupima afya mara kwa mara, na kwa upande wa vijana wanapaswa kulinda maisha yao kwa kuepuka maambukizi haya ambayo yanasababisha kuwepo kwa watoto wasiohitajika kwenye jamii pia kuacha ngono zembe na pia kuwa waaminifu kwenye mahusiano maana vijana ndilo taifa la kesho.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yanayosababishwa na hali za maisha
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu visababishi vya vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni huduma maalumu ambayo utolewa kwa mtu ambaye ana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo. Zifuatazo ni huduma maalumu kwa mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Ugojwa wa pumu ni hatari na unaweza kutokea ghafla. Lakini je unaweza kusababisha kifo, makalahii itakwend akujibu swali hili
Soma Zaidi...Kubana kwa kifuwa ni katika hali ambazo si naweza kuhatarisha maisha. Huwenda kuwa ni miongoni mwa dalili za magonjwa mengi. Je unadhani na HIv na UKIMWI ni moja ya magonjwa hayo?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe wa tishu za matiti kwa wavulana au wanaume, unaosababishwa na kutofautiana kwa homoni za estrojeni na testosterone. Pia unaweza kuathiri matiti moja au zote mbili, wakati mwingine bila usawa. Watoto wachanga,
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanawake
Soma Zaidi...UGONJWA WA GONORIA NA DALILI ZAKE (GONORRHEA)Gonoria (gonorrhea) ni katika maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.
Soma Zaidi...