Yafahamu magonjwa ya kurithi na dalili zake pia na jinsi ya kujikinga nayo
Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya kurithi ambayo hubebwa na vinasaba vya urithi kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.magonjwa haya hata hivyo ,si kila kasoro huwa ni ugonjwa kwa mtu mfano ,ualbino na kitoweza kutofautisha rangi kama vile nyekundu na kija
yafuatayo ni magonjwa ya kurithi
Anemiaselimundu,hii ni hali ambayo seli nyekundu za damu kubadilika umbile lake la kawaida na kuwa kama mundu au hilali.kwa kawaida, seli nyekundu za damu Tina hemoglobini ambayo hisafirisha oksijeni nankabondayoksaidi ndani ya mwili.umbile la seli nyekundu za damu linapobadilika kuwa kama mundu hupunguza huwezo wa kuzalisha seli nyekundu za damu,pia selimundu zinazozalishwa huishi kwa muda mfupi.hali hizi husababisha upungufu wa gesi ya oksijeni katika seli,kushindwa kuunguza glukosi ya kutosha ili kuzalisha nishati ya mwili.
dalili za ugonjwa wa anemia selimundu:
miongoni mwa dalili za anemia selimundu ni
1.mwili kukosa nguvu.Hali hii humfanya mgonjwa kuwa dhaifu na kufanya kushindwa kuongea hivyo,kushindwa kutekeleza majukumu mbalimbali.
2.kupata maumivu katika sehemu mbalimbali za mwili.sehemu hizo ni mikono,miguu,tumbo,mgongo,kifua na sehemu mbalimbali zenye maungio.
3.homa.za mara kwa mara.
4.kuvimba miguu na mikono.
5.kupungukiwa na damu mara kwa mara.
6.kukakamaa sehemu za maungio na kupata maumivu makali sana.
7.kukohoa au kupata shida ya kupumua.
8.kupoteza hamu ya kukaa ,kudumaa nabkushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.
9.kupoteza fahamu kunakosababishwa na kupungua kwa mzunguko wa oksijeni inayoenda kwenye ubongo.
9.mapigo ya moyo kuongezeka.
Dalili hizi zikiendelea kwa mda mrefu husababisha bandama kuathirika na wakati mwingine mgonjwa anaweza kupoteza maisha .mishipa ya damu kwenye ubongo ikipasuka ,mgonjwa kupoteza maisha kwa haraka muno.
tahadhari za kuchukua kwa mgonjwa wa anemia selimundu.ni vema kuhakikisha kwamba mgonjwa wa anemia selimundu anakuwa katika uangalizi mkubwa , bahadhi ya mambo ya msingi kuzingatia ni:
1.kumpatia mgonjwa maji ya kutosha au vyakula vya maji maji.
2.kumkinga dhidhi ya magonjwa yanayoweza kumshambulia kwa urahisi.
3.kumpatia matibabu kwa haraka pindi wanapougua.
4.kumpatia lishe bora ili kuijenga afya yake na kuwezesha mwili kujikinga dhidhi ya magonjwa.
5.kumshirikisha kufanya mazoezi mepesi na kumpa muda wa kupumzika hasa siku za joto.
6.kufuatilia kwa karibu jotoridi la mwili na kumpeleka hospitali haraka endapo jotoridi litazidi nyuzi za sentigredi 37.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 ai web app 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Madhara ya kutotibu uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo
Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu ugonjwa wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni madhara yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kupitisha mkojo na via vya uzazi kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Njia za kufanya ukiwa na tatizo la uti wa mgongo.
Posti hii inahusu zaidi Njia za kufanya Ili kupunguza maumivu ya tatizo la uti wa mgongo, ni njia unazopaswa kufanya pale unapokuwa na tatizo la uti wa Mgongo.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa Malengelenge sehemu za siri
Malengelenge sehemu za siri ni maambukizi ya kawaida ya zinaa ambayo huathiri wanaume na wanawake. Makala ya malengelenge sehemu za siri ni pamoja na maumivu, kuwasha na vidonda katika sehemu yako ya uzazi. Lakini huenda usiwe na dalili au ishara za mal
Soma Zaidi...Ugonjwa wa macho mekundu (Conjunctivitis): Jinsi ya kujikinga.
Ugonjwa wa macho mekundu, kitaalamu Conjunctivitis (au Pink eye), ni uvimbe wa utando mwororo unaofunika sehemu nyeupe ya jicho na ndani ya kope. Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na virusi, bakteria, au mzio (allergy). Kwa kuwa ni rahisi sana kuambukiza, elimu kuhusu usafi wa kibinafsi na mbinu za kuzuia usambazaji ndizo nguzo kuu ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huu ndani ya jamii.
Soma Zaidi...Maumivu ya magoti.
Maumivu ya magoti ni malalamiko ya kawaida ambayo huathiri watu wa umri wote. Maumivu ya goti yanaweza kuwa matokeo ya jeraha, kama vile ligament iliyopasuka au cartilage iliyochanika.
Soma Zaidi...SABABU ZINAZOPELEKEA KUJAA KWA MATE MDOMONI NA MATIBABU YAKE
Kutokwa na mate mengi mdomoni si ugojwa ni hali inayoweza kutokea kwa mtu yeyote. Mara nyingi hali hii haihitaji matibabu wa dawa, na huondoka yenyewe. Lakini hutokea baadhi ya nyakati ikawa mate yanatoka zaidi mdomoni. Je na wewe ni miongoni mwao? Makala
Soma Zaidi...