DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)
DALILI ZA MALARIA
Dalili za malaria huenda pia zikafungamana na maradhi mengine, lakini endapo zikikusanyika pamoja kwa asilimia kubwa vitakuwa vinaonyesha uwepo wa malaria. Kumbuka hizi ni dalili tu, lakini ni vyema kupima ili kuwa na uhakika zaidi kabla ya kumeza dawwa.
Homa, homa ni kupanda kwa joto mwilini. Kikawaida homa ni dalili za maradhi mengi sanaila leo nitakueleza homa ya malaria ilivyo. Kikawaida hima ya malaria inaweza kuambatana na mambo kadhaa wa kadhaa. Mambo hayo ni kama
Kuhisi baridi, kutetemeka na kutaka kuotea jua ama moto. Haijalishi ni saa ngapi iwe mchana ama usiku lakini mgonjwa atahisi baridi kali sana. Na inaweza kumsababishia hali ya kutetemeka viungo ama taya za mdomo wake kugongana kwa baridi. Hivyo endapo homa itaungana na hali hii huenda ni malaria. Lakini haitishi, inaweza pia kuambatana na japo hili hap chini:-
Maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya misuli pamoja na viungio. Endapo homa ya mgojwa itaambatana na baridi, kisha ikafuatiwa na maumivu ya kichwa, maumivu haya yanaambatana na misuli kuuma pamoja na viungio. Mgonjwa anahisi katikati ya akutano ya viungio kama kuna vuta. Halli hizi zikikusanyika kwa pamoja huashiria malaria.
Mvurugiko wa tumbo unaopelekea kichefuchefu, ama kuharisha, ama kutapika ama vyote kwa pamoja. Mgonjwa anaweza kupata hali moja kati ya hizi ama akawa nazo zote. Mgonjwa anaweza kutapika maji ama chakula alichokula ama anaweza kutapika ile tunayoita nyongo. Hali hizi zinaweza kumpelekea mgonjwa akachoka sana. Tofauti na kuchoka huku lakini hatakuwa na hamu ya kula, na hata ladha ya chakula inabadilika na kuwa kichungu.
Uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya viungo, kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, kutapika ama kuharishah. Hizi ni katika dalili za malaria.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 web hosting 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 ai web app 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Hofu ya kufanya makosa (Perfectionism) na jinsi ya kuikabili.
​Katika ulimwengu wa ushindani na mitandao ya kijamii, wengi wetu tunajikuta tukinyongwa na mzigo wa kutaka kila kitu kiwe "kamilifu." Makala hii inachunguza kwa kina dhana ya perfectionism—hofu inayozuia ubunifu na maendeleo. Tutachambua kwa nini tunahofu kufanya makosa, athari zake katika afya ya akili na tija, na kutoa mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuachana na tabia hii ili kufikia mafanikio ya kweli kupitia kukubali mapungufu.
Soma Zaidi...Fahamu sababu za ugonjwa unanipeleka Kuvimba kwa mishipa ya Damu
posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Kuvimba kwa Mishipa ya Damu hujulikana Kama Behcet amboyo husababisha dalili nyingi ambazo hapo awali zinaweza kuonekana kuwa hazihusiani. Dalili na ish
Soma Zaidi...YAMINYOO NA ATHARI ZAO KIAF
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Uwepo wa asidi nyingi mwilini
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kuwepo kwa asidi nyingi mwilini hali uwasumbua watu wengi na kufikia kiasi cha kusababisha madhara mengine mawilini ikiwamo pamoja na kansa ya koo, ili kujua kama una wingi wa asildi mwilini unapaswa kujua dalili kama ifu
Soma Zaidi...Maumivu, kizunguzungu, kichefuchefu na kutoka na damu ni dalili zamimba?
Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.
Soma Zaidi...