Dalili za HIV na UKIMWI kwenye Ulimi na Mdomo

Dalili za HIV na UKIMWI kwenye Ulimi na Mdomo

Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi utaziomna hapa. hizi zinaweza kuwa ndio za kwanza kwa ambaye hajapima HIV

Dalili za HIV na UKIMWI kwenye Ulimi na Mdomo


DALILI ZA UKIMWI NA HIV KWENYE ULIMU NA MDOMO


HIV hivi ni virusi vilivyopata umaarufu sana kwa kufahamika kuwa ndio virusi pekee vinavyoweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI. Virusi hivi anaweza kuvipata binadamu yeyote yule. Zipo njia nyingi ambazo unaweza kupata virusi hivi kama kushiriki ngono zembe, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kijifungua, kushiriki vitu vyenye ncha kali, kupewa damu yenye virusi, na njia nyingine kibao. Dalili za HIV na UKIMWI zinatofautiana kulingana na hatua ya mgonjwa. Lanini kuna wakati Ulimi na Mdomo kuweza kuonyesha dalili hizi wazi wazi.


Dalili za HIV na UKIMWI kupitia mdomoni zinaweza kuwa ni dalili za mwanzoni sana za UKIMWI kwa baadhi ya watu. Ukweli ni kuwa dalili hizi zinaweza kumpata yeyote lakini kuna watu wapo hatarini zaidi kama watoto wachanga, wazee na watu wenye upungufu wa kinga yaani UKIMWI. Dalili hizi tutaziona moja hadi nyingine hapo chini.


Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi
1.Kukauka kwa mdomo na kuoza kwa meno.
Virusi vya HIV vinaweza kupelekea mdomo kukauka na kukosa mate ya kutosha. Hivyo miongoni mwa kazi za mate ni kulinda meno na mdomo. Hivyo kupelekea meno kuoza. Ni vyema mgonjwa kama anatatizo hili kuonana na daktari aweze kumpa ushauri. Unaweza kutumia dawa maalumu kwa ajili ya kuchochea mate ama kutafuna bigji ambazo hazina sukari.


2.Kupata fangasi wa kwenye mdomo wajulikanao kama candidiasis (thrush).
Fangasi hawa wanaweza kusababisha madoa mekundu kwenye ulimi, ama mdoa meupe kwenye mdomo. Pia wanaweza kusababisha kupasuka kwa kona za mdomo na kutengeneza weupe kwenye kona za mdomo. Pia mdomoni kunaweza kuta buda la nyama lisilokuwa na maumivu. Fangasi hawa wanaweza kuhamia kwenye koo na kusababisha maumivu. Fangasi hawa ni rahisi sana kuondoka baada ya matibabu ila kwa baadhi ya sababu wanaweza kuwa sugu.


3.Vidonda kwenye mdomo na ulimi
Hivi ni vijidonda vijidogo ambavyo vipo duara. Vinaweza kutokea kwenye ulimi na kwenye mashavu kwa ndani. Pia vinaweza kutokea nyuma ya koo. Vidonda hivi vinakuwa na rangi nyekunu pembeni na rangi ya kijivu katikati. Misongo ya mawzo na baadhi ya vyakula vinaweza kuwa ni sababu.


4.Vidonda vya homa.
Kama umeshawahi kushuhudia vidonda ambavyo vinatokana na homa. Vidonda hivi kwa watu wenye UKIMWI vina tabia ya kujirudia mara kwa mara. Dawa za ART huweza kusaidia hali hii kutotokea.


5.Maradhi ya ufinzi ama periodontitis or gingivitis
Haya ni maradhi ya ufizi ambapo ufinzi unakosa nguvu na kushindwa kuzuia meno vyema. Hal hii inaweza kupelekea kung’oka kwa meno. Hali hii inaweza tokea mapema sana miezi 18 baada ya kupata HIV. Ukavu kwenye mdomo, kuvuta sigara kunaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.


6.Kuota kwa kambakamba ama vinywele vinywele kwenye ulimi na pembeni ya ulimi.
Kitaalamu hivi hujulikana kama Hairy Leukoplakia. Vikambakamba ama vinyweleo nyweleo hivi havina maumivu lakini pia haviwezi kutoka hata kwa kupiga mswaki. Hii inaweza kuwa ni katika dalili za mwanzo zaidi za UKIMWI. Vyenyewe vipo na rangi nyeupe


7.Madoa ya rangi ya dhambarau iliyowiva ama nyekundu kwenye mafinzi, sehemu ya juu ya mdomo na nyuma ya ulimi. Kitaalamu hufahamika kama Kaposi’s Sarcoma (KS Hii inaweza kuwa ni dalili ya kwanza kwa mtu ambaye hajapima HIV. Na kwa ambaye ameshaanza kutumia dawa dalili hizi ni si rahisi kujionyesha.


8.Kuota chunjua kwenye mdomo,na ulimi. Hizi husababishwa na virusi vinavyojulikana kama Human Papillomavirus, HPV. Kikawaida chunjua inaweza kuota popote pale kwenye mwili hasa hasa hutokea mara nyingi kwenye mikono. Watu wenye HIV chunjia hizi huweza kuvamia ulimi na kuhama maeneo mengine kwenye mdomo. Pia baadhi ya virusi wanao;eta hali hii wanaweza kusababisha saratani.


Mwisho nikufahamishe tu kuwa mdomo ni katika sehemu za kwanza kuonyesha dalili za HIV na UKIMWI. Ni vyema kwenda kupima endapo utagundua una moja ya dalili hizo hapo juu.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 24193

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 web hosting     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Halow samahan dokta nmekuwa nikiumwa tumbo muda mwingi takriban wiki ya 3 halipon naharisha kuna muda nikila chakula hata kama kdogo tu maumivu makali,je nifanyaje msaada

Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii

Soma Zaidi...
Je kwa mfano mimi nmeupata ukimwi leo na sihitaji kwenda kupima yaaan uanza kujionyesha baada ya muda gani

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa ukimwi huonekana baada ya muda gani toka kuathirika?

Soma Zaidi...
Dalili za kwanza za ugonjwa wa kaswende na kisonono.

Kaswende (Syphilis) na Kisonono (Gonorrhea) ni magonjwa ya zinaa (STIs) yanayoambukizwa kupitia tendo la ndoa. Ingawa husababishwa na vimelea tofauti—Kaswende (bakteria Treponema pallidum) na Kisonono (bakteria Neisseria gonorrhoeae)—yote yanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini ikiwa hayatatibiwa mapema. Makala hii inaangazia dalili zao za awali ambazo mtu yeyote anayeshiriki ngono anapaswa kuzifahamu.

Soma Zaidi...
Dalili na madhara ya Kiungulia

post hii inaelezea kuhusiana na dalili au ishara na madhara ya Kiungulia ni maumivu ya moto kwenye kifua chako, nyuma ya mfupa wako wa kifua. Maumivu huwa mabaya zaidi wakati wa kulala au kuinama

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa macho mekundu (Conjunctivitis): Jinsi ya kujikinga.

Ugonjwa wa macho mekundu, kitaalamu Conjunctivitis (au Pink eye), ni uvimbe wa utando mwororo unaofunika sehemu nyeupe ya jicho na ndani ya kope. Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na virusi, bakteria, au mzio (allergy). Kwa kuwa ni rahisi sana kuambukiza, elimu kuhusu usafi wa kibinafsi na mbinu za kuzuia usambazaji ndizo nguzo kuu ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huu ndani ya jamii.

Soma Zaidi...