Posti hii inahusu zaidi hatua au mbinu za kupambana na ugonjwa wa UTI kwa sababu ugonjwa huu umekuwa tishio kubwa kwa sasa kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali ili kuweza kupambana na Ugonjwa huu.
1. Hatua ya kwanza ni matumizi ya maji ya kunywa na baada ya kunywa maji nenda haja kubwa mara kwa mara ili kuweza kupunguza uchafu mwilini.
2. Katika matumizi ya vinywaji epuka sana vinywaji ambavyo vinaweza kuhatarisha kibofu cha mkojo kwa sababu kama kuna maambukizo kwenye kibofu cha mkojo kupona ugonjwa wa UTI ni ndoto vinywaji vyenyewe ni kama vile kahawa na matumizi mengi ya vinywaji vyenye wingi wa caffeine.
3. Nenda haja ndogo baada ya kufanya ngono zembe.
Kwa hiyo baada ya kufanya tendo la ndoa nenda haja ndogo ili kama kuna maambukizi yoyote ya ugonjwa wa UTI uweza kuondoka.
4. Kawaida jipanguse kutoka mbele kwenda nyuma.
Kwa sababu kujipangusa kutoka nyuma kwenda mbele unasababisha bakteria walio kwenye kinyesi kuja mpaka kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha Maambukizi kwa hiyo siku zote wafundishe watoto kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma sio nyuma kwenda mbele.
5. Hakikisha kila siku sehemu za siri ni safi mda wote ili pia kupunguza Maambukizi unapaswa kuosha sehemu za siri bila kutumia sabuni za manukato tumia sabuni ya kawaida ya kipande.
6. Kila mara jaribu kuoga maji masafi na yanayotiririka kwa sababu maji masafi yanasababisha kuwepo kwa hali ya usafi na kuzuia kuwepo kwa Maambukizi kwenye via vya uzazi.
7. Kwa kawaida ugonjwa huu mwanzoni ilionekana ni ugonjwa unaowapata sana akina dada au wanawake kwa ujumla ila kwa sasa ugonjwa huu uwapata wote yaani wanawake na wanaume kwa hiyo wote tuna haki ya kupigana na ugonjwa huu ili tuweze kuondokana nao na inawezekana.
8. Kwa hiyo usipotibu ugonjwa huu unaweza kupata madhara mengi pamoja na ugumba kwa wanawake, kupata kansa ya kibofu kwa mwanaume na madhara mengine mengi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download Nowmm nahis miguu pamoja na mikono kuishiwa nguvu ni mgongo kuuma ni dalili za ugonjwa gan ?
Soma Zaidi...Mapacha walioungana ni watoto wawili wanaozaliwa wakiwa wameunganishwa kimwili. Mapacha walioungana hukua wakati kiinitete cha mapema kinapojitenga na kuunda watu wawili. Ingawa vijusi viwili vitakua kutoka kwa kiinitete hiki, wataendelea kushikamana mar
Soma Zaidi...Mngurumo wa moyo ni sauti wakati wa mzunguko wa mapigo ya moyo wako kama vile kutetemeka inayotolewa na damu yenye msukosuko ndani au karibu na moyo wako. Sauti hizi zinaweza kusikika na kifaa kinachojulikana kama stethoscope. Mapigo ya moyo ya kawaida
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu faida za bamia mwilini
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye milija (follapian tube) kwa kitaalamu huitwa salpingitis, ni maambukizi kwenye milija ambayo husababishwa na bakteria.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa ukoma ni Ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayejulika kama mycobacterium leprae.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya magonjwa yanayotokea kwenye sehemu za siri,kwa sababu siku kwa siku kuna magonjwa mengi yanayotokea kwenye sehemu za siri ila kuna vyanzo mbalimbali ambavyo usababisha kuwepo kwa magonjwa kwenye sehemu mbalimbali za siri
Soma Zaidi...UGONJWA WA GONORIA NA DALILI ZAKE (GONORRHEA)Gonoria (gonorrhea) ni katika maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.
Soma Zaidi...Poliomyelitis ni kuvimba kwa suala la kijivu la uti wa mgongo na wakati mwingine sehemu ya chini ya ubongo
Soma Zaidi...