Aina mbalimbali za michubuko

Post hii inahusu zaidi aina mbalimbali za michubuko,kwa Sababu michubuko utokea sehemu tofauti tofauti na pia Kuna aina mbalimbali kama tutakavyoona hapo mbeleni.

Aina mbalimbali za michubuko.

1. Michubuko kwenye ngozi.

Hii ni aina mojawapo ya michubuko ambayo mara nyingi utokea kwenye ngozi ya juu ya mtoto hasa hasa ni kwa sababu ya kuzalisha watoto kwa kutumia vyuma, ambapo michubuko hii utokea kwenye ngozi ya juu ya kichwani , kwa kawaida uweza kugunduliwa na wahudumu wa afya mara tu mtoto akimaliza kuzaliwa, kwa hiyo ikitokea mtoto amevutwa na vyuma ni vizuri kabisa watoa huduma kuwa makini kukagua mtoto kama Kuna sehemu ambayo imeathirika na kuweza kutoa msaada . Pamoja na kazi za wahudumu na wazazi pia wanapaswa kuwa waangalifu katika kuona mabadiliko yoyote kwa mtoto na kutoa taarifa Ili mtoto aweze kuhudumiwa.

 

2. Kwa kawaida michubuko kwenye sehemu za ngozi ya juu ya mtoto mara nyingi haiitaji matibabu zaidi ila kusafishwa na kuiweka sehemu safi na kukausha usaidia sana kupona kwa ngozi hiyo ,vile vile na dawa za kupunguza maambukizi utolewa ambazo dawa hizo kwa kitaamu huiitwa antibiotics. Kwa kawaida mikwaruzo kwenye sehemu ya juu ya ngozi ya kichwa upona mapema na pia wazazi au ndugu hawapaswi kuweka dawa yoyote ambayo ni kinyume na dawa za hospital kwa sababu dawa nyingine uongeza matatizo zaidi kuliko kupona.

 

3. Vile vile aina nyingine ya michubuko kwenye ngozi ni kuvimba kwenye ngozi ya kichwani ambayo Kwa kitaamu huiitwa caput succedaneum,u uvimbe huu utokea kwa watoto hasa pale wanapopambana kutoka kwenye tumbo la mama na kuzaliwa ukutana na obstacles au ukutana na vitu ambavyo umsababishia hali ya kushindwa kutoka vizuri au kutoka kwa shida na kusababisha uvimbe kwenye sehemu ya kichwa , kwa kawaida uvimbe huu uonekana tu baada ya mtoto kuzaliwa na ndani ya siku tatu uvimbe huo uisha taratibu na hatimaye kutoweka kwa hiyo wahudumu wa afya wanapaswa kuwaelimisha wazazi na ndugu kutoweka vitu vyovyote kwenye uvimbe.

 

4. Michubuko kwenye sehemu za misuli.

Kuna wakati mwingine michubuko utokea kwenye sehemu za misuli au kwa kitaamu kwenye muscle ni kutokana na mishipa kupasuka au kukwaruzwa kwa ngozi hasa za kwenye misuli .kwa kawaida misuli inayoshambuliwa Zaid ni misuli ya kwenye shingo ambayo Kwa kitaamu huiitwa Torticollis muscle, hali hii utokea hasa pale mtoto anapozaliwa hasa kama ametanguliza bega au bega katika kuvutwa misuli ya shingoni inawezekana kulegea na kusababisha michubuko kwenye ngozi, kwa hiyo kama mtoto amezaliwa kwa shida ni vizuri kabisa kuangalia sehemu mbalimbali za misuli Ili kuweza kugundua tatizo lolote ambalo linaweza kujitokeza.

 

5. Mikwaruzo kwenye nevu.

Pia Kuna Kipindi ambapo mikwaruzo utokea kwenye nevu na kwa kiwango kikubwa nevu ambazo zinakuwa affected au zinazoathiriwa ni nevu za kwenye uso na pia na nevu za kwenye mabega, mikono,na kwenye vidole, ndio maana unaweza kumkuta mtoto amelemaa mkono,au bega na pia sehemu yote kuanzia kwenye bega na mikono kwa hiyo kama Kuna Neva yoyote ambayo imeathirika ni kuangalia kwa kutumia utrasound au x- ray kwa Sababu huwezi kuona kuaribika kwa Neva kwa macho ila unaweza kutumia dalili ila kufahamu ni Neva gani imeathirika ni kutumia utrasound au x-ray. Kwa hiyo tutaweza kuona nevu Moja badala ya nyingine kama ifuatavyo.

 

6. Nevu za kwenye uso.

Kuna wakati panakuwepo na kuharibika kwa nevu za kwenye uso kwa kitaamu huiitwa facial nevu.

 Kwa kawaida mtoto kama amezaliwa kwa kuvutwa na vyuma au wakati mwingine kuzaliwa kwa shida kwa sababu mbalimbali ambazo uchangia matatizo ya uzazi, Kuna mda mwingine mtoto uzaliwa akiwa na matatizo kwenye nevu za uso kwa sababu pengine zinakuwa zimevutwa hali ambayo usababisha mtoto kuzaliwa akiwa mdomo wazi, macho yanakuwa yamefunguka na mtoto hawezi kuyafumba, hali ambayo usababisha mtoto kushindwa kunyonya au pengine kabisa anashindwa kumeza, kwa hiyo ukimwona mtoto wa hivyo Kuna dawa ambayo Kwa kitaamu huiitwa methyl cellulose usaidia kurahisisha nevu za usoni na kumfanya mtoto kufumba macho na mdomo na kuanza kunyonya kawaida.

 

7. Mikwaruzo kwenye nevu za kuanzia kwenye bega mpaka kwenye mikono ambazo kwa kitaamu huiitwa branchial plexus.

Ni nevu ambazo pamoja na kuhathiri mabega na mikono vile vile uingiliana na uti wa mgongo katika nevu za mbavu ya nane na pia kuelekea kwenye shingo, ndio maana Kuna watoto wanaozaliwa wakiwa na shingo limelegea na pengine kushindwa kulisimamisha shingo kabisa, kwa hiyo watoto wa namna hiyo hawapaswi kufanyiwa mazoezi kiholela kwa lengo la kufanya shingo zao ziwe vizuri ila badala ya kumsaidia unaweza kuleta matatizo zaidi, kwa hiyo ni vizuri watu wa mifupa ndio wawafanyie mazoezi kwa kitaamu huiitwa watu wa physiotherapy,na wenyewe baada ya kutumia utrasound na x-ray na kuangalia mtiririko wa nevu ndipo waanze kazi mara moja.

 

8. Vile vile Kuna kupalalizi kwenye bega na sehemu ya juu ya mikono na sio kwenye vidole.

Kuna wakati mwingine kwa sababu ya michubuko kwenye mikono hali ambayo usababisha mtoto kupalalizi kwenye bega na pia kwenye mikono ya juu, kwa sababu nevu za sehemu ya juu ziliaribiwa wakati wa kuzaliwa inawezekana kabisa ni kwa sababu ya kutumia vyuma wakati wa kuzaliwa au mtoto kushindwa kutoa au kwa sababu ya mtoto kuvutwa sana na hatimaye kuharibika kwa nevu za mkono na bega, pia hali hii kwa kitaamu huiitwa erb;s palsy, kwa matibabu zaidi ni kuwaona wataalamu wa physiotherapy Ili waweze kumfanyia mtoto mazoezi kulingana na jinsi alivyoumia.

 

9.  Vile vile Kuna mikwaruzo ya kwenye nevu za vidole na sehemu ya chini kabisa ya vidole , ambapo unakuta mtoto Kwa upande wa bega na shingo yupo vizuri kabisa ila kwenye vidole na sehemu ya chini amepalalize na hawezi kufanya chochote au kushika chochote, hali hii utokea kwa sababu ya nevu za chini kwenye mikono zinakuwa zimehadhiriwa, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa waangalifu punde mtoto anapozaliwa Ili kuweza kutambua kama Kuna tatizo lolote linalohusiana na kuharibika kwa nevu kwa sababu mtoto asipoangaliwa mapema anaweza kupata madhara zaidi.

 

 10. Kwa hiyo kazi ya kumfanya mtoto aonekane jinsi alivyo ni kazi ya wataalamu wa afya na pia ikiwa taratibu za kuzalisha mtoto ni nzuri na kugundua mapema hali ya hatari kwa mtoto kabla ya kuzaliwa ni vizuri kabisa kwa sababu ufanya matatizo mbalimbali yasitokee matatizo kama vile kupalalizi na kuondoa ulemavu kwa watoto. Na pengine tatizo linaweza kuwepo ila kama mtoto ameandaliwa mapema na kufanyia uchunguzi mapema mtoto anaweza kupona na kuendelea na hali yake ya Kawaida.

 

 

11. Pia kwa sababu ya kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa jamii, Kuna tabia ya watu kutumia madawa ya mbalimbali au kuwafanyia mazoezi bila mpangilio hali inayowafanya kuleta madhara badala ya kusaidia , kwa hiyo tatizo hili likitokea ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya na kuweza kuwapa ushauri unaopaswa Ili kuepuka kuleta madhara zaidi.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 1779

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

YAMINYOO NA ATHARI ZAO KIAF

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Nini husababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake na wanaume

Somo hili linakwenda kukueleza vitu vinavyosababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu

Soma Zaidi...
Yajue mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi (cellulitis)

Mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi hujitokeza sehemu yenye jeraha pia huonyesha wekundu wenye upele,Uvimbe na malengelenge.

Soma Zaidi...
Dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo

Posti hii inahusu zaidi dalili la jeraha la kawaida kwenye ubongo, jeraha la kawaida utokea kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ajali na kugongwa na kitu chochote kichwani,

Soma Zaidi...
Hernia

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa hernia

Soma Zaidi...
Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu

Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo.

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa.

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa,ni madhara ambayo utokea endapo Maambukizi kwenye mifupa yasipotibiwa kwa mda wake.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma

Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa ukoma ni Ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayejulika kama mycobacterium leprae.

Soma Zaidi...
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO

MWISHO Vidonda vya tumbo vinatibika bila ya shaka.

Soma Zaidi...
NINI CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA? NI YUPI MBU ANAYESAMBAZA MALARIA

Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles.

Soma Zaidi...