Zijuwe dalili kuu 7 za vidonda vya tumbo, kama kiungulia, tumbo kujaa, maumivu ya umbo..

Vidonda vya tumbo huweza kutokea ndani ya tumbo kutokana na mashambulizi ya bakteria aina ya H.pylori, ama kutokana na athari za madawa flani ama mashambulizi ya wadudu wengineo ama kwa sababu ya ugonjwa wa saratani. Makala hii inakwenda kukuletea dalili duu za vidonda vya tumbo.
1.Maumivu ya tumbo; hii pengine ndio katika dalili kuu zaidi ambazo wengi wenye vidonda vya tumo wanaipata. Maumivu haya yanawza kuwa makali sana wakati mgonjwa akiwa na njaa.Tumbo hili ni tofauti na tumbo la ngiri ama chango. Maumivu haya yanaweza kuanzia chini ya kitomvu na kupanda juu hadi kifuani. Maumivu haya yanaweza kufuatana na dalili zifuatazo hapo chini.
2.Tumbo kujaa; tumbo linaweza kujaa gesi hata akashindwa kula vyema. Huenda mgonjwa akajihisi ameshiba badala ya kuka kidogo. Uhalisia si kwamba ameshiba ila tumbo ndio limejawa na gesi.
3.Kukosa hamu ya kula; hii ni katika dalili ya hatari sana, maana umuhimu wa chakula unafahamika vyema. Mgonjwa anaumwa na tumbo na anakosa kabisa hamu ya kula pia anahisi tumbo kujaa.
4.Kupata kiungulia cha mara kwa mara. Kiungulia unaweza kukitibu kwa kutumia dawa, kwani hazina tabu kwa vidonda vya tumbo. Pia unaweza kulamba majivu, hii ni tiba mbadala ambayo inatumka kutibu kiungulia. Lakini epuka kula vyakula vyenye gesi.
5.Kupungua uzito; vidonda vya tumbo vinaweza kusababisha mtu kupungua uzito, bila ya kujuwa sababu maalumu. Inaweza kuwa ni kutokana na kutokula kwake kwa sababu ya kukosa hamu ya kula.
6.Kichefuchefu na kutapika. mgonjwa wa vidonda vya tumbo wakati mwingine anapata kichefuchefu kisicho na sababu maalumu. Hali hii inaweza kumpelekea akatapika ama asitapike. Na wakati mwingine anaweza kuona dmau kwenye matapishi yake.
7.Mapadiliko kwenye kinyesi. Mgonjwa anaweza kuona mabadiliko kwenye rangi ya kinyesi chake. Kinaweza kuwa cheusi sana na chenye harufu mbaya sana. Na wakati mwingine kinaweza kuwa na damu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye milija (follapian tube) kwa kitaalamu huitwa salpingitis, ni maambukizi kwenye milija ambayo husababishwa na bakteria.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata UTI, ni watu ambao wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa UTI kwa sababu ya mazingira mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu watu walio hatarini kupata gonorrhea gonoria
Soma Zaidi...Malaria inaweza kumpata mtu yeyote bila ya kujali mri.
Soma Zaidi...Poliomyelitis ni kuvimba kwa suala la kijivu la uti wa mgongo na wakati mwingine sehemu ya chini ya ubongo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu sababu za mwanamke kuumwa tumbo chini ya kitovu, ni tatizo ambalo limewapata wanawake wengi na pengine sababu ni vigumu kupata au pengine zinapatikana lakini kwa kuchelewa hali ambayo usababisha madhara mbalimbali kwenye mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha dalili,Sababu,na namna ya kujikinga na ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani ambao kitaalamu hujulikana Kama orchitis.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu athari za maambukizi ya magonjwa ya ngonoย ambapo magonjwa ya ngono isipokuwa UKIMWIย yanatibika .mgonjwa anashauriwa kuwahi hospitali au kituo chochote cha afya kupata matibabu mara anapoona dalili za magonjwa haya.
Soma Zaidi...Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni.
Soma Zaidi...