Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate na namna ya kutibu tatizo la kujaa kwa mate mdomoni
NI NINI HUSABABISHA MATE KUJAA MDOMONIKutokwa na mate mengi mdomoni si ugojwa ni hali inayoweza kutokea kwa mtu yeyote. Mara nyingi hali hii haihitaji matibabu wa dawa, na huondoka yenyewe. Lakini hutokea baadhi ya nyakati ikawa mate yanatoka zaidi mdomoni. Je na wewe ni miongoni mwao? Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate. Sababu hizi zipo nyingine ni kwa wanawake tu, pia zipo ambazo ni kwa watu wa jinsia zote. Tunatarajia baada ya kusoma makala hii utaweza kuzijuwa sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate, pia utaweza kupata kujuwa nini unatakiwa ufanye kulingana na tatizo lako.
KUJAA KWA MATE MDOMONI NI NINI HASA?
Kitaalamu kitendo hiki cha kujaa kwa mate mdomoni hufahamika kama hypersalivation. Hiki ni kitendo cha mdomo kujaa mate na wakati mwengine hutokea mate yakatoka yenyewe kwenye midomo baada ya kujaa. Kitaalamu kitendo hiki sio ugonjwa ila ni dalili ya kuwepo kwa tatizo lakiafya ama kuwepo kwa jambo lililopelekea mabadiliko ya mwili na kiafya.
JE MATE NI NINI?
Mate ni kimiminika cheupe kinachopatikana mdomoni ambacho hutengenezwa kwenye tezi za mate zinazojulikana kama salivary glands. Mate yana vichochezi (enzymes) ambavyo hutumika katika mmeng'enyo wa chakula hasa chakula cha wanga mdomoni. Mate pia husaidia katika kulainisha chakula na kuweka mgomo katika hali ya usafi, usalama na ubichibichi.
Tafiti zinaeleza kuwa mtu wa kawaida anaweza kuzalisha mate yanayofikia lita moja na nusu kwa siku. mate huzalishwa kwa wingi mtu anapokula na uzalishaji huu hupunguwa pale anapolala.
MADHARA YA KUWA NA MATE KIDOGO
Kwa kuwa mate yana faida kubwa mwilini hivyo endapo uzalishaji wa mate hautakuwa wa kutosheleza madhara huweza kumpata mtu ni kama:-
1. mdomo kuwa mkavu
2. Mmeng'enyo wa chakula kutofanyika vyema mdomoni kwa vyakula vya wanga
3. Mtu anaweza kupata taabu wakati wa kumeza
4. Anaweza kupata vidonda vya mdomo
5. Mdomo utaweza kuathiriwa kwa urahisi na fangasi, bakteria na sumu na kemikali za kwenye vyakula
6. Hata kuzungumza kunaweza kuathiriwa endapo mtu atakosa mate ya kutosha
MADHARA GANI ATAYAPATA MTU KAMA ATAKUWA NA MATE MENGI ZAIDI?
Kama ilivyokuwa kuna hasara kwa mate kukosekana mwilini, halikadhalika endapo mate yatakuwa mengi zaidi pia hali hii itakuwa na madhara yake. Madhara hayo ni kama:-
1. Matatizo wakati wa kusema, yaani hatoweza kuema vyema kama mate yatakuwa yamejaa mdomoni
2. Itakuwa vigumu kuufunga mdomo
3. Pia mdomo utaweza kupata mashambulizi ya bakteria kwa urahisi.
4. Mtu atashindwa kujiamini na kukaa na watu kwa sababu ya mate yake.
NINI HUSABABISHA MDOMO KUJAA MATE?
Hizi ni katika sababu ambazo hupelekea mate kujaa mdomoni:-
1. Kuongezeka kwa uzalishwaji wa mate mdomoni
2. Kama mtu atakuwa na shida na kushindwa kumeza mate ama mdomo kuondoa mate yote wakati wa kutema
3. Kama mtu atakuwa na matatizo ya kutoweza kuufunga mdomo
NINI HUSABABISHA ONGEZEKO LA UZALISHAJI WA MATE MDOMONI
Kama ulivyoona hapo juu sababu za kuwa na mate mengi mdomoni ni ongezeko la uzalishwaji wa mate mdomoni. Sasa swali la msingi kuwa "ni nini husababisha hili ongezeko la uzalishwaji wa mate mdomoni" . Sababu gizo ni kama:-
1. Kichefuchefu
2. Homa ya asubuhi na ujauzito
3. Kama kuna maabukizi na mashambulizi ya bakteria na virusi kwenye koo, tonsil na meneo mengine ya mdomoni
4. Kama umeng'atwa na buibui mwenye sumu, ama umekula uyoga ama umeng'atwa na wadudu
5. Kama unatumia meno ya bandia
6. Kama hufanyi usafi wa kinywa kwa umakini
7. Kama una maambukizi ya T.B ama ugonjwa wa rabies
8. Kama una kiungulia cha mara kwa mara
9. Mipasuko kwenye taya ma amifupa ya taya kutojipanga vyema
10. Vidonda vywnyw mfumo wa mmeng'enye wa chakula kama mdomoni, kooni na tumboni
NINI HUSABABISHA KUSHINDWA KUMEZA MATE AMA KUTEMA MATE YOTE?
Kama tulivyoona kuwa katika sababu zinazopelekea mate kujaa mdomoni ni kushindwa kuyameza yote, ama kuyatema yote. Sasa ni kitu gani husababisha hali hii?
1. Kuwa na shida ya kiafya kwenye mfumo wa fahamu
2. Kuwa na shida ya kiafyakwenye figo
SABABU NYINGINE ZINAZOPELEKEA MDOMO KUJAA MATE
1. Mpangilio mbaya wa meno
2. Majeraha kwenye mdomo
3. Hewa mbaya
4. Upungufu wa maji mwilini
5. Matatizo kwenye mfumo wa fahamu hasa katika kuhisi ladha ya chakula
6. Kama una maradhi ya pneumonia
NINI UFANYE KAMA UNA HILI TATIZO:
1. Kwa kupitia dalili zilizotajwa hapo juu, angalia ambayo huwenda ndio sababu kwako.
2. Kawaida tatizo hili halihitaji dawa, ila kama imezidi fika hospitali kwa uchunguzi zaidi.
3. Fika kituo cha afya kwa vipimo zaidi kama hali yako itaendelea kwa muda bila kurudi nyuma.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 11891
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Koo langu limekauka yaweza kuwa ni muadhirika?
kuwashwa na koo ni katika dalili za kuwa na maambukizi mwilini. Kuwa na maambukizi haimaanishi ni HIV ama UKIMWI laa hili ni neno pana. Hapa nitakujuza kwa ufupi kuhusu swali hilo la muulizaji kuwa anawashwa na koo. Soma Zaidi...
Habari nasumbuliwa na tumbo upande wakilia adi nikikojoa mkojo wa mwisho uwa wa kahawia tiba take nini?
Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula. Soma Zaidi...
VIPIMO VYA MINYOO (UTAJUAJE KAMA UNA MINYOO)? fecal test, blood test, colonoscopy tape test X-ray, MRI na CT scan.
VIPIMO VYA MINYOO Haitoshelezi kuwa na dalili pekee ukathibitisha kuwa una minyoo. Soma Zaidi...
VIDONDA VYA TUMBO NA ATHARI ZAKE
Soma Zaidi...
Je dalili za kisonono au gonoria kwa mwanamke huonekana baada ya mda gani
Soma Zaidi...
Dalili zinazoonyesha joto la kupungua mwilini (hypothermia)
joto la mwili wako linapungua, moyo wako, mfumo wa neva na viungo vingine haviwezi kufanya kazi kwa kawaida. Isipopotibiwa, Hypothermia hatimaye inaweza kusababisha moyo wako na mfumo wa upumuaji kushindwa kabisa na hata kifo. Soma Zaidi...
Dalili na Ishara za mawe kwenye figo
Mawe kwenye figo yana sababu nyingi na yanaweza kuathiri sehemu yoyote ya njia yako ya mkojo kutoka kwa figo hadi kibofu chako. Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia Ugonjwa wa ini
Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini. Soma Zaidi...
Kivimba kwa mishipa ya Damu
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa yako ya damu. Inasababisha mabadiliko katika kuta za mishipa ya damu, ikiwa ni pamoja na kuimarisha, kudhoofisha, kupungua na kupungua. Mabadiliko haya huzuia mtiririko wa damu, na kusababi Soma Zaidi...
Dalili za UTI upande wa wanawake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za UTI upande wa wanawake Soma Zaidi...
Dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, ni dalili ambazo zinaweza kujitokeza Kwa mgonjwa,Kwa hiyo baada ya kuona dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospital mara moja Kwa ajili ya matibabu. Soma Zaidi...
Njia za kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi njia mbali mbali ambazo uweza kitumiwa na wataalamu ili kuweza kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu. Soma Zaidi...