Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
4.UGONJWA WA UTI
UTI ni kifupisho cha Urinary Track Infection. Ni ugonjwa unaoshambulia katika mfumo wa mkojo, hususan kibofu, figo na mirija ya urethra. Ugonjwa huu umekiwa ukiwapata sana wanawake kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 5 mmoja ana UTI.
Maambukizi ya ugonjwa huu yanapatikana hasa chooni. Pia huenda ugonjwa huu ukaenezwa kupitia kuingiliana kimwili na utaratibu mbovu wa kujisafisha baada ya kukidhi haya. Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata zaidi watu ambao wanatumia vyoo vya shirika yaani vyoo vinavyotumiwa na watu wengi.
Ugonjwa wa UTI umekuwa ukisababishwa na bakteria kwa kiasi kikubwa. Bakteria aina ya E.coil ambao wanapatikana kwenye utumbo mkubwa wamekuwa wakisababisha UTI kwa kiasi kikubwa kuliko bakteria wengine. Pia fangasi (fungi) na virusi huweza kusababisha UTI japo kwa kiwango kidogo.
Mtu anaweza kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa huu kwa,;-
1.Jisafishe kutokea mbele kuelekea nyuma baada ya kukidhi haja kubwa (kwa wanawake). Hii husaidia kuzuia bakteria wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wasipate nafasi ya kuingia kwenye njia ya haja ndogo.
2.mwaga maji kila uingiapo chooni kwaajili ya nkujisaidia. Kitendo hiki kitaondosha vijidudu vilivyopo pale chini.
3.Jisafishe sehemu za siri kabla ya kuingiliana na baada.
4.Hakikisha unakwenda kutoa haja ndogo (kukojoa) baada ya tendo la ndoa. Kitendo hiki kitasaidia kuondosha vijidudu vilivyoingia wakati wa tendo.
5.Nenda katoe haja ndogo haraka sana baada ya kuhisi.
6.Kunywa maji mengi zaidi. Husaidia kuondowa vijidudu kwa njia ya mkojo.
7.Vaa nguo za ndani za pamba, kavu na zisizobana.nguo za mpira na zinazobana husababisha jasho (majimaji) sehemu za siri. Majimaji haya husaidia bakteria kukuwa na kuishi hivyo wanaweza kuathiri njia ya mkojo.
Ugonjwa wa UTI una dalili nyingi na huenda nyingine zikafanana na dalili za malaria. Miongoni mwa dalili hizi ni;-
1.Maumivu wakati wa haja ndogo
2.Kutowa mkojo mchafu. Mkojo unawea kuwa na rangi sana, ua kama wa mawingu na kadhalika.
3.Harufu kali sana ya mkojo.
4.Mkojo kuwa na damu
5.Kukojoa marakwa mara hata kama mkojo utakuwa ni mchache sana.
6.Maumivu ya mgongo na tumbo kwa chini.(lower abdomen)
7.Maumivu ya kichwa.
8.Kuhisi uchovu sana
9.Miwasho sehemu za siri.
Itambulike kuwa ugonjwa wa UTI unatibika bila ya matatizo. Jambo la msingi ni kuwa wagonjwa wengi wamekuwa hawamalizi dozi. Kwakuwa ugonjwa huu umeenea sana na ni rahisi kuupata imetokea hali za kujirudia rudia. Hivyo mgonjwa ni muhimu kuchukuwa tahadhari tulizotzja hapo juu wakati akiwa anatumia dozi. Pia watu wawe makini na tiba za kiasili ambazo husemekana zinatibu UTI.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kushindwa kupitisha mkojo, ni madhara makubwa yanayotokea kwa mtu iwapo akishindwa kupitisha mkojo.
Soma Zaidi...Malaria ni moja ya magonjwa hatari yanayoongoza katika vifo vya watoto wengi duniani walio chni ya umri wa miaka 5. Katika post hii utakwend akujifunza kuhusuugonjwa huu jinsi unavyotokea, hatuwa zake na dalili zake.
Soma Zaidi...post Ina onyesha madhara na matatizo ya Unene Utoto ni hali mbaya ya kiafya inayoathiri watoto na vijana. Inatokea wakati mtoto yuko juu ya uzito wa kawaida kwa umri na urefu wake
Soma Zaidi...Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hukua kutoka kwenye tishu laini za misuli ya uterasi. Fibroids nyingi ambazo zimekuwepo wakati wa ujauzito hupungua au kutoweka baada ya ujauzito, kwani uterasi inarudi kwenye ukubwa wa kawaida.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa usafi katika maisha ya mwanadamu au mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Kabla ya kubanwa zaidi na pumu, kuna dalili za awali zinzznza kujitokeza, na hapo ndipo utakapoanza kuchukuwa tahadhari. Makala hii itakwenda kukujulisha zaidi kuhusu dalili hizo.
Soma Zaidi...posti hii inaelezea kuhusiana na dalilili na Mambo ya hatari ya Macho makavu hutokea wakati machozi yako hayawezi kutoa unyevu wa kutosha kwa macho yako. Machozi yanaweza kuwa duni kwa sababu nyingi. Kwa mfano, Macho makavu yanaweza ku
Soma Zaidi...Kaika post hii utakwenda kujifunz akuhusu dalili za homa ya ini. Dalili hizi sio lazima zitokee zote. Zinaweza zikatokea baadhi tu na ikatosha kuonjesha kuw auna homa ya ini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la tezi koo, ni tatizo ambalo uwapata watu mbalimbali ambapo Usababisha koo kuvimba na mgonjwa huwa na maumivu mbalimbali na pengine mgonjwa upata kikohozi kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo.
Soma Zaidi...