Unyogovu (Depression ) ni mojawapo ya ugonjwa wa akili ambao unahusishwa na hisia za huzuni, kukosa matumaini, na kupoteza furaha au shauku katika shughuli za kila siku. Huu si tu hisia ya huzuni iliyokatisha tamaa, bali ni hali sugu inayoweza kuathiri mabadiliko ya mwili, mawazo, na tabia ya mtu. Unyogovu unaweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kemikali katika ubongo, maumbile, mazingira, na matukio mbali mbali katika maisha ambayo kupelekea mgonjwa kuwa hivyo.
Unyogovu au Kwa kitaalamu depression ni hali ya kiakili inayoweza kuathiri njia ambavyo mtu anafikiri, anavyojihisi, na anavyofanya kazi katika maisha yake ya kila siku mara nyingi hali hii mtu ukumbana nayo kwenye mazingira ya Kila siku sio kwamba anazaliwa nayo.
Hapa kuna maelezo ya kina juu ya dalili za unyogovu au depression ambazo zinaweza kuonekana Kwa mtu na pia zinaweza zikaonekana Kwa mtu mara moja au zikatumia mda kuonekana kutokana na hali ya mtu.
Dalili za Kihisia
mtu anaweza kubadilikw taratibu kutoka kwenye tabia yake ya kawaida akaanza kuwa na huzuni inayoendelea ambayo haiwezi kabisa kutoweka,Kutokuwa na matumaini,Hisia ya kukosa matumaini kuhusu maisha au hali ya baadaye,Kukata Tamaa: Mtu anaweza kuhisi kama hakuna chochote cha maana au kizuri kinachoweza kutokea,Wasiwasi au Kukasirika Mara nyingi watu wanahisi wasiwasi, hasira, au ukosefu wa utulivu kujiweka Kando.
.Dalili za Kimwili
Mabadiliko ya Kula kupita kiasi au kupoteza hamu ya kula. Hii inaweza kusababisha kupoteza uzito au kuongeza uzito Kwa Wakati Mrefu Ndan Kuwepo kwa uchovu wa mara kwa mara bila sababu ya kimwili,maumivu Yasiyo na Sababu, Kuumwa kwa mwili kama vile maumivu ya kichwa, mgongo, au misuli ambayo hayawezi kueleweka,Usingizi Mzito au Watu wanaweza kukumbana na matatizo ya usingizi, kama vile kushindwa kulala au kulala kupita kiasi.
4. Dalili za Kijamii na Kitendo
Kukosa Hamu ya Shughuli Kupoteza hamu ya shughuli ambazo mara nyingi zilikuwa na furaha,Kujiondoa katika Mahusiano,Kutoroka kutoka kwa urafiki na familia, au kukwepa shughuli za kijamii,Mabadiliko katika Utendaji, Kushindwa kufanya kazi vizuri katika kazi, shule, au katika majukumu mengine ya kila siku.
5. Dalili za Wazo na Hisia
Mawazo ya Kufa,Watu wengine wanaweza kuwa na mawazo ya juu kuhusu kifo au kujiua, ambao ni dalili nzito ambazo zinahitaji msaada Zaidi,Kwa hiyo mtu mwenye depression anapaswa kutafutiwa tiba ipasayo baada ya kuona dalili ambazo zinampelekea kutaka kujiu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kikohozi cha muda mrefu ni zaidi ya kero. Kikohozi cha muda mrefu kinaweza kuharibu usingizi wako na kukuacha unahisi uchovu. Matukio makali ya kikohozi cha muda mrefu yanaweza kusababisha kutapika, kizunguz
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za ugonjwa wa Dondakoo,hali hii utokea iwapo ugonjwa haukutibiwa mapema au umetibiwa lakini bado Kuna matokea hasi ambayo yanaweza kujitokeza kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili la jeraha la kawaida kwenye ubongo, jeraha la kawaida utokea kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ajali na kugongwa na kitu chochote kichwani,
Soma Zaidi...Je umeshawaho kujiuliza maswali mengi kihusu fangasi?. Huyu hapa ni mmoja katika waulizaji waliopata kuuliza rundo la maswali haya. Soma post hii kuona nini ameuliza
Soma Zaidi...Zijuwe sababu za kutokea kwa vidonda vya tumbo. Sababu kuu za vidonda vya tumbo hizi hapa
Soma Zaidi...post hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa kifaduro ambao hujulikana Kama Pertussis pia inajulikana kama kifaduro ni maambukizi ya bakteria ambayo huingia kwenye pua yako na koo.
Soma Zaidi...Ingawa mbu hunyonya damu kwa binadamu, hawana uwezo wa kueneza virusi vya UKIMWI (VVU). Sababu ni kwamba virusi vya VVU haviwezi kuishi wala kuzaliana ndani ya mwili wa mbu, na pia mbu hawaingizi damu ya mtu mmoja kwa mwingine wanapong’ata.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe au puto katika mshipa wa damu kwenye ubongo. Uvimbe kwenye Ubongo unaweza kuvuja au kupasuka, na kusababisha kuvuja damu kwenye ubongo. Mara nyingi, kupasuka kwa Uvimbe wa Ubongo hutokea katika nafasi kati
Soma Zaidi...