Dalili za ugonjwa wa schizophrenia
Schizophrenia ni ugonjwa wa akili ambao huathiri jinsi mtu anavyofikiri, kuhisi, na kuamua. Dalili za schizophrenia zinaweza kuwa kama ifuatavyo hapo chini
1.Mawasiliano Kwa ujumla hasa kuhusu hisia zao na kutoziwasilisha Kwa mpangilio.
Watu wenye schizophrenia wanaweza kushindwa kueleweka au kuwasiliana vyema, Hii inaweza kujumuisha mambo kama kuzungumza bila mpangilio au kuacha mazungumzo,au wakati wa kuongea hawezi kuongea jambo akalimaliza vizuri hatua Kwa hatua na likaeleweka na pia hawezi kuielezea hisia yoyote aliyo nayo na ikaeleweka Kwa watu,Kwa hiyo ni vigumu kumwelewa.
2.Mawazo ya Kutosheleza.
Hii inaweza kujumuisha wazo la kutokuwepo na hali halisi, au kutokuwa na muono sahihi wa hali halisi, yaani hawezi kuongea kitu Kwa uhalisia wake mpaka azunguke na pia anaweza akafumba au akaweka story ambayo haiko nauhalisia Kwa wakati huo Kwa ujumla sio rahisi kuwa na mawazo ya kutosheleza katika jambo fulani.
3.Hallucinations.
Hizi ni uzoefu wa kuona, kusikia, kugusa, au kuhisi mambo ambayo hayapo. Mara nyingi, watu wanashuhudia sauti zisizokuwepo.kwa mfano mnaweza kuwa na mgonjwa wa hali hiyo mmekaa akasema naoa nyoka mkubwa akaanza kukimbia,au akasema mnaningenya au mnanitukana na mambo kama hayo ambayo watu wa kawaida wenye afya ya akili huwezi kuyaona.
4 kuwepo na Delusions.
Hizi ni imani zisizo za kawaida na zisizoweza kubadilishwa. Mfano ni kudhani kuwa mtu anafuatwa au kuhitaji watu fulani kuwasaidia kwa njia zisizo za kweli.Kujitenga: Watu wenye szichophrenia wanaweza kuwa na hisia ya kujitenga kutokana na familia na marafiki, na mara nyingi wanaweza kutojihusisha na shughuli za kijamii.
5.Kutokuwepo na hisia
: Hii inaweza kujumuisha kukosa hisia ya furaha, huzuni, au hisia nyingine za kibinadamu,yaani Kwa ujumla mtu haeleweki kama amefurahi,amekasilika au kuwepo Kwa hisia yoyote,Kwa mfano akifurahi ni mda mfupi na ameacha na hisia zozote Kwa kweli hazitabiliki kwake.
: 6.kubadilikabadilika Kwa Tabia
Watu wenye ugonjwa huu wanaweza kuonyesha tabia zisizotarajiwa au za ajabu, kama vile kuzungumza na mtu ambaye hayupo, Kwa hiyo unaweza kukuta mtu yupo busy na kuongea na mtu ambaye alifariki thamani au mtu wa maana Kwa mfano unaweza kukuta mgonjwa anasema nipo naongea na kiongozi wa Nchi Sasa hivi na ukiona alivyojipanga kama anaongea nakiongozi kweli kumbe ni ugonjwa tu.
kuukosa hamu ya kushiriki shughuli za kawaida kwenye jamii.
Wanaweza kuwa na ugumu wa kujihamasisha kufanya kazi au shughuli za kawaida za kila siku Kwa sababu mara nyingi jinsi wanavyowaza wanaona ni watu wa pekee kabisa na wanastahiki kupewe Kila kitu,Kwa hiyo wanajiona hawana haha ya kufanya chochote,Kwa mfano anayejiita kiongozi wa Nchi kadri ya akili yake huyo hatutegemei kabisa kama anaweza kufanya chochote au mwingine anajiita BOT,,na mambo kama hayo yanayoweza kusababisha uvivu katika jamii.
8. Kuhisi sio watu wa muhimu Miongoni mwa Watu
: Wanaweza kuwa na wazo la kujiona kama miongoni mwa watu wasioeleweka au wasio na thamani,Kwa sababu mara nyingi watu hawawaelewi hali hii inatokea pale wagonjwa wa schizophrenia wanapokuwa kero katika jamii Kwa hiyo Kuna kipindi jamiii inaweza kuwatenga Kwa sababu ya halo yao halisi.
ujua dalili hizi ni muhimu kwa sababu ugonjwa wa schizophrenia unahitaji matibabu sahihi. Ikiwa unafikiri kuwa wewe au mtu unayemjua anaweza kuwa na dalili hizi, ni muhimu kutafuta msaada wa kitaalamu. Matibabu yanaweza kujumuisha dawa na terapi ya mwili na kisaikolojia..
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
vidonda vya tumbo, dalili zake, chanzo chake na tiba yake
Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya vidonda vya tumbo, nini hasa chanzo chake, vipi vinatokea ni zipi dalili zake, ni zipi njia za kujilinda dhidi ya vidonda vya tumbo. Pia tutaangalia matibabu ya kutibi vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Dalili za madhara ya ini
Ini Ni kiungo kikubwa Sana mwili na hutumika kuondoa sumu mwili ambayo hujulikana Kama detoxification
Soma Zaidi...Kazi ya kongosho na athari za ugonjwa wa kisukari.
Kongosho ni kiungo muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na udhibiti wa homoni mwilini. Ugonjwa wa kisukari hutokea pale kongosho inaposhindwa kufanya kazi zake ipasavyo, hasa katika uzalishaji wa insulini. Makala hii inachunguza kwa kina kazi za kongosho, uhusiano wake na ugonjwa wa kisukari, athari za muda mrefu za ugonjwa huu, na mbinu za kitaalamu za kuzuia na kudhibiti hali hii ili kulinda afya ya kongosho na mwili kwa ujumla.
Soma Zaidi...Athari za unywaji wa pombe kupita kiasi kwenye Ini.
Ini ni kiungo cha ajabu chenye kazi nyingi, ikiwemo kusafisha sumu mwilini, kutengeneza protini, na kusaidia mmeng'enyo wa chakula. Hata hivyo, ini lina uwezo mdogo wa kuhimili kiasi kikubwa cha pombe. Unywaji wa pombe kupita kiasi hauumizi tu "roho" ya mtu, bali husababisha uharibifu wa kimwili kwa ini ambao unaweza kuwa wa kudumu. Makala haya yanaelezea mzunguko wa uharibifu huo na kwa nini ni muhimu kuelewa hatari hizi.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kushoto
Soma Zaidi...