HATUA ZA KUJIKINGA NA VIDONDA VYA TUMBO Unaweza kupunguza hatari yako ya vidonda vya tumbo ikiwa unafuata mikakati sawa inayopendekezwa kama tiba ya nyumbani kutibu vidonda.
HATUA ZA KUJIKINGA NA VIDONDA VYA TUMBO
Unaweza kupunguza hatari yako ya vidonda vya tumbo ikiwa unafuata mikakati sawa inayopendekezwa kama tiba ya nyumbani kutibu vidonda. Inaweza pia kusaidia:
Jilinde dhidi ya maambukizo. Haijulikani wazi jinsi bakteria aina ya H. pylori inavyoenea, lakini kuna ushahidi fulani kwamba inaweza kupitishwa kutoka kwa mtu hadi mtu au kupitia chakula na maji.
Unaweza kuchukua hatua za kujikinga na maambukizo, kama vile H. pylori, kwa kuosha mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji na kwa kula vyakula ambavyo vimepikwa kabisa.
Chukua tahadhari dhidi ya dawa za kupunguza maumivu. Ikiwa unatumia kila wakati dawa za kupunguza maumivu ambazo zinaongeza hatari ya vidonda vya tumbo, chukua hatua za kupunguza hatari hiyo. Kwa mfano, kunywa dawa yako pamoja na chakula.
Zungumza na daktari kupata dawa ambayo itakupa utulivu wa maumivu bila ya kusababisha hatari zaidi.
Epuka au punguza kunywa pombe wakati unatumia dawa. Kama tulivyoona unywaji wa pombe unaweza kuhatarisha zaidi vidonda vya tumbo kwa kuchochea uzalishwaji wa asidi tumboni.
Ikiwa unahitaji dawa za kutuli za maumivu na zile za NSAID, unaweza kuhitaji pia kuchukua dawa za ziada kama vile antacid, PPI, blocker acid au cytoprotective agents. Kikundi cha NSAIDs kinachoitwa COX-2 inhibitors kinaweza kuwa na nafasi ndogo ya kusababisha vidonda vya tumbo, lakini vinaweza kuongeza hatari ya mshtuko wa moyo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa vipele kwenye midomo na sehemu za siri .Ni ugonjwa ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa upele na matatibabu yake, ni ugonjwa unaosabavishwa na mdudu kwa kitaalamu huitwa mites sarcoptes scrabie mdudu huyu usababisha miwasho kwenye ngozi.
Soma Zaidi...Hepatitis C ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoshambulia ini na kusababisha kuvimba. Watu wengi walioambukizwa na virusi vya Hepatitis C (HCV) hawana dalili. Kwa kweli, watu wengi hawajui kuwa wana maambukizi ya Hepatitis C hadi uharibifu wa ini
Soma Zaidi...Je unahitaji kujuwa kama umepata ujauzito baada ya kufanya tendo la ndoa? hakika sio rahisi ila kama utakuwa makini utaweza.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mfumo wa mwili ambao huhusika na kusafirisha damu ,virutubisho na takamwili.mfumo huu unajumuisha damu,mishipa ya damu na moyo.moyo husukuma damu kupitia mishipa ya damu na kufika maeneo yote ya mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna au njia za kuepuka na Ugonjwa huu wa ngiri ambao uleta madhara kwa watoto, vijana na watu wazima, kwa hiyo ili tuweze janga hili ni lazima tufanye yafuatayo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ingawa sio watu wote wenye dalili kama hizi Wana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo Ila zikitokea mtu anapaswa
Soma Zaidi...