SABABU ZA MIGUU KUFA GANZI.


image


Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali,za miguu kufa ganzi,ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi na walio wengi hawafahamu kabisa ni sababu zipi ambazo uleta tatizo hili.


Sababu za miguu kufa ganzi.

1. Kupungua kwa virutubisho mbalimbali kwenye mwili,

Kwa kawaida mwili huwa na virutubisho mbalimbali ambavyo ufanya kazi tofautitofauti na vikiongezeka na pia uweza kuleta matatizo na vikipungua na penyewe uleta matatizo na kusababisha miguu kufa ganzi kwa hiyo kama kuna upungufu wa vitamini,B complex usababisha kuwepo kwa ganzi kwenye miguu kwa hiyo ndio maana watu wenye tatizo hili upewa dawa za vitamini B complex ili kuweza kupunguza kiwango cha ganzi mwilini.

 

2. Pengine kuna tatizo la matumizi ya dawa.

Matumizi ya dawa mbalimbali nazo usababisha kuwepo kwa matatizo ya kwa ganzi kwenye miguu, kwa sababu ya matumizi ya mda mrefu uweza kuleta matatizo kwa mfano kwa matumizi ya dawa za kurefusha maisha kwa wanaozitumia kwa mda mrefu usababisha kuwepo kwa ganzi kwenye miguu na pia kwa wale wanaotumia dawa za kifua kikuu nao pia wana tatizo la kuwepo kwa ganzi kwenye miguu, kwa hiyo wakishagundua tatizo hilo wanapaswa kuwahi kwa daktari ili kuweza kupata matibabu na kuendelea na hali yao ya kawaida.

 

3. Kuwepo kwa uzito mkubwa wa mwili.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa wa mwili ambapo mwili uelemewa na jinsi ya kusafirisha damu huwa kwa shida hali ambayo Usababisha miguu kufa ganzi.

 

4. Kuwepo kwa Ugonjwa wa kisukari.

Kwa namna moja au nyingine kuna kipindigonjwa wa kisukari hasa wa siku nyingi upatwa na tatizo la kuwepo kwa ganzi mwilini hii ni hali ya kawaida kwa wagonjwa wa kisukari kwa hiyo wakipatwa na tatizo kama hili ni vizuri kabisa kupata matibabu ili kuweza kuendelea na maisha ya kawaida.

 

5. Pia na wagonjwa wenye shinikizo la damu huwa matatizo mbalimbali ambayo Usababisha pia miguu kufa ganzi kwa hiyo ni vizuri kabisa wagonjwa wa hivi wakishapata tatizo kama hili ni kujitahidi kabisa kumwona daktari ili waweze kupata msada zaidi.

 

6. Hili tatizo lipo na linatibika kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya ili kuweza kupata msaada zaidi na kuepukana na tatizo hili.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizuri na kuwa na afya nzuri. Soma Zaidi...

image Madhara ya kutotibu Ugonjwa wa homa ya utu wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu homa ya uti wa mgongo, kwa kuwa ugonjwa huu mara nyingi uathiri sehemu za kwenye ubongo kuna madhara ambayo yanaweza kutokea endapo Ugonjwa huu haujatibiwa mapema. Soma Zaidi...

image Zijue sababu za moyo kutanuka.
Posti hii inahusu zaidi sababu za moyo kutanuka, Kuna kipindi ambapo moyo utoka kwenye hali yake ya kawaida na kutanuka hali ambayo usababisha madhara kwa mwenye tatizo hilo, ila Kuna sababu ambazo usababisha moyo kutanuka kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

image Chini ya Tumbo langu Kuna uchungu lakini si sana shinda ni ni?
Nini kinasababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu? Soma Zaidi...

image Namna ya kuzuia Ugonjwa wa kaswende
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia Ugonjwa wa kaswende, tunajua wazi kuwa Ugonjwa huu unasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kufanya ngono zembe na njia nyingine kwa hiyo tunaweza kuzuia kusambaa na kuenea kwa ugonjwa huu kwa njia mbalimbali kama tutakavyoona hapo baadaye. Soma Zaidi...

image Mambo yanayoweza kudhoofisha kinga ya mwili
Kinga ya mwili inapodhoofu mwili unakuwa hatarini kupata maradhi. Je unayajuwa mambo yanayodhoofisha kinga ysbmeili? Soma Zaidi...

image Bawasili usababishwa na nini?
Posti hii inahusu zaidi visababishi vya ugonjwa wa Bawasili,kuna watu wengi wanapenda kujua kabisa chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii na kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu visababishi vya Bawasili. Soma Zaidi...

image Fahamu ugonjwa wa Varicose vein
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa vericose veini, hili ni tatizo ambalo utokea katika mzunguko wa damu hasa kwenye miguu. Soma Zaidi...

image Huduma kwa watu waliodhani wamepatwa na maambukizi.
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo utolewa kwa watu wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya virus vya ukimwi. Soma Zaidi...

image Hatua za kupambana na ugonjwa wa UTI
Posti hii inahusu zaidi hatua au mbinu za kupambana na ugonjwa wa UTI kwa sababu ugonjwa huu umekuwa tishio kubwa kwa sasa kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali ili kuweza kupambana na Ugonjwa huu. Soma Zaidi...