Makala hii itaeleza dalili za ukimwi, dalili za VVU, magonjwa nyemelezi na matumizi ya ARV
ELIMU YA KUHUSU HIV NA UKIMWI
Ni nini maana ya Ukimwi?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno “upungufu wa kinga mwilini” ni hali sugu, inayoweza kutishia maisha inayosababishwa na virusi vya Ukimwi (VVU). Kwa kuharibu mfumo wako wa kinga, VVU huingilia uwezo wa mwili wako kupambana na viumbe vinavyosababisha magonjwa. Viumbe hivyo ni kama bakteria, virusi, protozoa, fangasi na vinginevyo.
Nini maana ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)?
VVU ni ufupisho wa maneno Virusi Vya Ukimwi, ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini. Hudhoofisha mwili uwezo wake kujilinda dhidi ya vijidudu vya maradhi. Neon hili kwa lugha ya kiingereza hufupishwa kama HIV.
VVU ni maambukizo ya zinaa. Yanayoweza pia kuenezwa kwa kuongezewa damu iliyoambukizwa au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kunyonyesha. Inaweza kuchukua miaka mimngi huwenda 5 mpaka 10 kabla ya VVU kudhoofisha kinga yako ya mwili hadi kufikia ukimwi.
Je ipo tiba ya VVU na UKIMWI?
Hakuna tiba ya VVU / UKIMWI, lakini kuna dawa ambazo zinaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa magonjwa na uharibifu wa kinga ya mwili. Dawa hizi zimepunguza vifo vya UKIMWI katika mataifa mengi yaliyoendelea. Lakini VVU inaendelea kupunguza idadi ya watu barani Afrika, Haiti na sehemu za Asia. Dawa hizi mimkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja hufahamika kama ARV yaani Ant-Retrovirus na matibabu yake hufahamika kama ART yaani Ant-Retroval Therapy. Dawa hizi piazimegawanyika katika makundi mengi kama NRTIs, NNRTs, Protease inhibitors na nyinginezo kibao.
DALILI ZA VVU NA UKIMWI NI ZIPI?
Dalili za VVU na UKIMWI hutofautiana, kulingana na awamu ya maambukizo, muda kutoka maambukizo yalipotokea pia afya ya mtu kabla ya maambukizo.
Hatua ya kwanza ya maambukizi (Primary infection)
Watu wengi walioambukizwa na VVU hupata ugonjwa unaofanana na Homa ndani ya mwezi mmoja au miwili baada ya virusi kuingia mwilini. Hivyo kutengeneza dalili za awali za VVU na UKIMWI. Dalili hizi si lazima zimpate kila mtu, wapp wengine hawazipati kabisa. Sana dalili hizi hutokea wiki mbili toka kupata maambukizi mpaka wiki nne kisha hupotea. Kwa baadhi ya watu zinaweza kuanzia wiki ya kwanza, na wengine kuishia wiki ya sita. Dalili hizo ni:-
1.Kupatwa na homa.
2.Maumivu ya kichwa yasiyo na sababu
3.Maumivu ya misuli
4.Kuota upele
5.Kupatwa na baridi ama kuhisi baridi.
6.Kukauka na koo ama kupatwa na vidonda kooni.
7.Kupatwa na Vidonda vya kinywa au sehemu za siri
8.Kuvimba kwa Tezi za limfu kwenye mapaja, makwapa na haswa kwenye shingo
9.Mwili kuwa na Maumivu bila ya sababu maalumu.
10.Kutokwa na Jasho la usiku
11.Kuharisha
Ingawa katika kipindi hiki kiwango cha virusi sio rahisi kuviona kwa vipimo vya kawaida vinavyotumika kupima, lakini ni kuwa katika kipindi hiki kiwango cha virusi ni kingi sana kwenye damu, na muathirika anaweza kumuambukiza mwengine kwa urahisi sana. Baada ya wiki sita dalili hizi hupotea na hazitajirudia tena. Hapa virusi vitatulia ndani ya mwili kwa miaka mingi bila ya kuonyesha dalili yeyote ile, huku vukiendelea kuharibu kinga ya mwili kidogokidogo.
Hatuwa ya pili Toka kuambukizwa.
Kama tulivyoona dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza. Sasa hutokea kwa baadhi ya watu kuwa tezi za limfu zisivimbe wakati wa hatuwa ya kwanza, ila zikavimba katika hatuwa hii ya pili. Tofauti na hili hakuna dalili nyingine maalumu ya VVU katika hatuwa hii ya pili. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka miaka 10. Kwa watu wengi ni kati ya miaka 4 mpaka 10 ila wengine mara chache hutokea ikawa chini ya hapo.
Baada ya maambukizi ya Awali
Hiki ni kipindi cha miaka kadhaa baada ya kuambukizwa. Katika wakati huu hakuna dalili ya VVU inayoonekana. Hata hivyo kadri iaka inavyosonga mbele ndivyo seli zinavyozidi kudhoofu. Wakati virusi vinaendelea kuongezeka na kuharibu seli za kinga, unaweza kupata maambukizo kidogo au ishara sugu na dalili kama vile:
1.Homa
2.Uchovu
3.Node za mtoki, kwapa, na shingo kuvimba – na hii ndio mara nyingi moja ya ishara za kwanza za maambukizo ya VVU
4.Kuhara
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Kupumua kwa pumzi
Kuendelea kwa UKIMWI
Ikiwa hautapata matibabu maalumu ya ART na kutumia ARV mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuthibiti maambukizo yako ya VVU, ugonjwa huendelea hadi kufikia kuwa UKIMWI kwa takriban miaka 10. Wakati huu ukiwa na UKIMWI unakua, mfumo wako wa kinga umeharibiwa sana, na hivyo kukufanya uweze kuambukizwa na magonjwa nyemelezi – Mgonjwa nyemelezi ni magonjwa ambayo hayangemsumbua mtu aliye na kinga nzuri.
DALILI ZA UKIMWI.
Mpaka kufikia hapa ndipo mgonjwa huambiwa ana UKIMWI. Kumbuka mpaka kufikia hapa tayari miaka Zaidi ya mine hadi 10 itakuwa imepita. Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa endapo mgonjwa hatatumia matibabu maalubu ya ARV hatoweza kuzidi miaka 3. Sasa hebu tuzione dalili na Ishara za UKIMWI katika hatua hii:-
1.Kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kutetemeka kwa homa au Homa juu inayofikia nyuzi 100 F (38 C) na kudumu kwa wiki kadhaa
3.Kikohozi
4.Kupumua kwa pumzi za taabu
5.Kuhara kusiko kata
6.Utando mweupe wa kudumu au vidonda visivyo vya kawaida kwenye ulimi wako au kinywani mwako
7.Maumivu ya kichwa mara kwa mara
8.Uchovu wa kudumu, usioelezewa
9.kuona maluweluwe
10.Kupungua uzito bila ya sababu maalumu
11.Vipele kwenye ngozi au majipu
NJIA AMBAZO VVU HUAMBUKIZWA;
Kuna nadharia nyingi zinaelezea ni namna gani ambazo VVU huambukizwa. Katika hizo kuna mbazo ni Imani potofu kabisa na hazifai kukubaliwa. Hapa nitakuletea njia ambazo zinaambukiza VVU. Njia hizo ni:-
1.Kwa kufanya mapenzi (ngono). Unaweza kuambukizwa ikiwa unafanya ngono ya uke, ya mkundu au ya mdomo na mwenzi aliyeambukizwa VVU ambaye damu yake au shahawa zake au majimaji ya ukeni huingia mwilini mwako kwa kupitia michubuko midogo, ama vidonda ama mikato ama sehemu iliyowazi inayoruhusi kufikiwa damu kwa urahisi. Na hii ndiyo njiainayoongoza katika kuambukiza VVU
2. Kwa kuongezewa damu kutoka kwa aliye athirka. Katika namn nyingine, virusi vinaweza kuambukizwa kupitia kuongezewa damu. Kwa sasa si sana njia hii maana damu anayopatiwa mgonjwa itapitia uchunguzi wa kina kabla ya kuongezewa ijapokuwa madhaifu ya kibinadamu yanaweza kufanyika.
3. Kwa kushirikiana matumizi ya sindano na vitu vyenye ncha kali kama visu na viwembe. VVU vinaweza kuambukizwa kupitia sindano, inaweza kutokea wakatiwa matibabu yatakayofayika chini ya utaratibu. Inaweza pia kuwa watumiaji a madawa ya kulevya hushirikiana sana matumizi ya sindano. Endapo mtumiaji wa kwana ana VVU na akajidunga ama kujikata, kisha akachukuwa mtumiaji mwinine na kujidunga ama kujikata muda mfupi toka mtumiaji wenye VVU kutumia.
4. Wakati wa ujauzito au kujifungua au kupitia kunyonyesha. Mama walioambukizwa VVU wanaweza kuambukiza watoto wao endapo hwatakuwa makini. Mama mjamzito mwenye VVU anatakiwa atumie dozi haraka iwezekanavyo ili kuepushamaambukizi kwa mtoto. Hata hivypo inampasa azalie hospitali ili uangalifu zaidi ufanyike wakati a kujifunguwa.
HAYA HAYAWEZI KUAMBUKIZA VVU
1.Mate
2.Mkojo
3.Kugusana mikono ama kukumbatia
4.Kula pamoja
5.Kucheza pamoja.
6.Kung’atwa na mbu
SASA UKIMWI UNATOKEAJE?
Seli ndio matofali yaliyojengea miili yetu. Ndani ya miili yetu kuna aina nyingi za seli, na seli za damu. Ndani ya damu pekee kuna aina zisizopunguwa tatu za seli. Kuna seli hai nyekundu, nyeupe na seli sahani. Kila seli kati ya hizi ina kazi zake. Sasa hii seli hai nyeupe yenyewe ndio inakazi ya kupigana na vijidudu vya maradhi vinapoingia katika miili yetu. Vijidudu hivyo vinaweza kuwa bakteria, virusi ama fangasi. Seli hizi ndizo ambazo ambazo huitwa CD4.
Sasa virusi vya VVU vinapoingia mwilini vinaanza kuharibi hizi seli ambazo zinalinda mwili. Kawaida mtu anaweza kuwa na seli hizi 500 mapa 1500 katika kipimo kimoja. Sasa VVU vinaanza kuziharibu hizi na kupunguza idadi yake. Na kila seli hizi zikipunguwa ndipo mfumo wa kinga unavyoendelea kuharibika na ndivyo maradhi yanapozidi kupata nafasi ya kuingia mwilini.
Sasa endapo zimeharibiwa na kufika idadi ya 200 katika kipimo kimoja hapa mtu huyu ataambiwa ana Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI. Katika hatuwa hii mtu atakuwa akinyemelewa na maradhi nyemelezi kama fangasi, kifuwa kikuu, na mengineyo.
Endapo mgonjwa atatumia ARV mapema anaweza kukaa miaka mimngi sana bila ya kufikia hatuwa hii. Kuna umuhimu wa kutumia ARV mapema, sababu hizo ni kama:-
1.Kupungua maambukizi ya VVU
2.Kulinda afya ya mtu
3.Kupunguza uharibifu wa seli
4.Kulinda mwili dhidi ya maradhi nyemelezi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1023
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Nini chanzo cha malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria Soma Zaidi...
NAMNA YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO
NAMNA YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO Unaweza kupata nafuu kutoka kwa maumivu ya kidonda cha tumbo ikiwa utafata taratibu za kiafya kama:- 1. Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster. Kwa hiyo ili kugundua kubwa mtu ana Ugonjwa huu Dalili kama hizi zifuatazo zinaweza kutokea kwa mgonjwa. Soma Zaidi...
Maradhi yatokanayo na fangasi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yatokanayo na fangasi Soma Zaidi...
Kumsaidia sliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo
Posti hii inahusu namna ya kumsaidia mgonjwa aliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo. Soma Zaidi...
Athari za kutotibu fangasi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi Soma Zaidi...
Elimu kuhusu HIV na UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu elimu ya kuhusu HIV na UKIMWI Soma Zaidi...
VIDONDA VYA TUMBO NA ATHARI ZAKE
Soma Zaidi...
MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Soma Zaidi...
Njia za kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi njia mbali mbali ambazo uweza kitumiwa na wataalamu ili kuweza kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu. Soma Zaidi...
Hatua za kupambana na ugonjwa wa UTI
Posti hii inahusu zaidi hatua au mbinu za kupambana na ugonjwa wa UTI kwa sababu ugonjwa huu umekuwa tishio kubwa kwa sasa kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali ili kuweza kupambana na Ugonjwa huu. Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia Ugonjwa wa ini
Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini. Soma Zaidi...