Kwa kuwa mbu wanaosambaza malaria wanang’ata usiku sana ama alfajiri, hivyo tunaweza kujikinga na malaria kwa :-
Kulala kwenye chandarua, ni vyema kikatiwa dawa. pia ni vyema ukahakikisha kuwa chandarua hakina matundu yaani kiwe kizima. ha hakikisha unawatoa mbu kwenye chandarua kama wapo kisha ndipo ujiandae kulala.
Kupaka losheni ya mbu; hiki ni losheni ambazo zina harufu mbaya ambayo inawakera mbu. harufu hiki huweza kutofautiana. kuna nyingine ni kali na nyengine ni kawaida. kuna nyingine utapenda harufu zao na nyingine hutapenda. watu wengine wakipaka losheni hizi huwashwa hususani wanapopaka usoni. hakikisha haupaki mdomoni kiasi kwamba unaweza kuila losheni kwa bahati mbaya.
Kuvaa nguo ndefu zinazoziba viungo; nguo hizi zisiwe ndefu tu bali ziwe nzito kiasi kwamba zinaweza kuzuia mbu kuifikia ngozi yako. ni vyea zikafunika mikono na miguu, na maeneo mengine ambayo yanashambuliwa na mbu kama shingo.
Kutumia dawa za mbu; dawa hizi zipo za kupulizia kama pafyumu na zipo za kuchoma. unaweza kutumia za kupulizia wakati hupo ndani kwa muda wa dakika kama 30. dawa za kuchoma nazo pia ni vyema ukachoma ukiwa umetoka kisha baada ya dakika 30 kisha ingia ndani.
Fyeka vichaka, punguza nyasi na fukia madimbwi yaliyo karibu na nyumba. hakikisha hakuna makopo, vifuu ama chochote kinachoweka maji. hii itasaidia kupambana na mazalia ya mbu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa
Soma Zaidi...Saratani ya Figo ni Saratani ambayo huanzia kwenye figo. Figo zako ni viungo viwili vyenye umbo la maharagwe, kila kimoja kikiwa na ukubwa wa ngumi yako. Ziko nyuma ya viungo vyako vya tumbo, na figo moja kila upande wa mgongo wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Soma Zaidi...Je unahitaji kujuwa kama umepata ujauzito baada ya kufanya tendo la ndoa? hakika sio rahisi ila kama utakuwa makini utaweza.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.
Soma Zaidi...