picha

Ufahamu ugonjwa wa UTI na dalili zake hasa kwa wajawazito

Wajawazito wanaposumbuliwa na ugonjwa wa UTI, dalili za UTI na namna ya Kujikinga na UTI

Ufahamu ugonjwa wa UTI na dalili zake hasa kwa wajawazito



UTI NA UJAUZITO.




Moja katika changamoto za ujauzito ni kupata maambukizi na mashambulizi ya UTI ya mara kwa mara. Bakteria ni rahisi kuingia kwenye mirija ya mkojo na kukifikia kibofu, haya kwa wajawazito ni rahisi sana kuliko ambao sio wajawazito. Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 18 ya wanawake wajawazito wanasumbuliwa na UTI.



Dalili za UTI
1.Maumivu wakati wa kukojoa na kuhisi kama unaungua
2.Kukojoa mara kwa mara
3.Mkojo kuwa na mawingi mawingu ama kuwa kama na damu
4.Maumivu ya kwenye nyonga
5.Maumivu ya mgongo sehemu ya chini
6.Homa
7.Kichefuchefu



Njia za kujikinga na UTI
A.Kojoa kila unapohisi mkojo
B.Kunywa maji mengi
C.Wacha kutumia viungo vya uke (kusafisha uke kwa kemikali, eti kufanya uke ukaze, msafi na wenye kuvutia)
D.Wacha kutumia sabuni kali sehemu za siri.



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu