Figo ni nini, ni yapi maradhi yake na nitajiepusha vipi na maradhi ya figo
Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.
IJUWE FIGO NA MARADHI YAKE NA NAMNA YA KUJIKINGA NA MARADHI YA FIGO:
Figo ni katika viungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ijapokuwa kila kiungo ni muhimu kwenye mwili wa binadamu, lakini katika mfumo wa kutoa mkojo na kuchuja damu figo ni muhimu zaidi. maradhi ya figo yamekuwa yakiongezeka kuliko ilivyokuwa hapo zmani, ijapokuwa kasi yake sio sawa na maradhi mengine. Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.
Kila mtu ana figo mbili kwenye mwili wake, ukubwa wa figo unakadiriwa kufukia ukubwa wa ngumi yako. Katika mwili wako figo hupatikana karibia na katikati ya mgongo chini kidogo ya mbavu. Ndani ya kila figo kuna mamilioni ya vichujio vya kuchuja damu vinavyojulikana kama nephron. Kazi yake kubwa ni kuchuja damu, kuondoa uchafu kwenye damu na kuondoa maji ya ziada kwenye damu na kupata mkojo ambao ni mchanganyiko wa majina na uchafu uliotoka kwenye damu. Baadaye maji haya ya mchanganyko yanakwenda kwenye kibofu na kuhifadhiwa kama mkojo.
Kati ya maradhi mengi ya figo huanza kuathiri hizi nephone. Na endapo hizi nephrone zikiharibiwa zinapelekea figo kuathirika na kushindwa kufanya kazi vyema na kushindwa kuondoa uchau kwenye damu. Katika sababu za tatizo hili la kuathirika kwa nephone inaweza kuwa matatizo ya kurithi, majeraha, ama matumizi ya madawa ambayo athari yake yanaweza kuathiri figo.
Unaweza kuwa hatarini sana kama una maradhi ya kisukari, ama kama una shinikizo kubwa la damu ama una ukaribu wa kifamilia na watu ambao wana tatizo hili. Maradhi hatari ya figo ni yale ambayo huathiri nephone kipolepole na huwenda hii kuchukuwa miaka kadhaa hadi kuja kuumwa. Matatizo mengine yanayoweza kuathiri figo ni kama saratani ya figo na vijiwe vya kwenye figo.
Katika njia za kulinda figo yako dhidi ya maradhi ni pamoja na kunywa maji mengi angalau glasi 8 kwa siku. Fanya mazoezi na punguza kula vyakula vyenye chumvi sana. Nenda chooni kila unapohisi kukojoa wacha kubana mkojo kwa muda mrefu. Hizi ni baadhi tu ya njia ambazo zitakusaidia kulinda figo zako dhini ya maradhi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Je kwa mfano mimi nmeupata ukimwi leo na sihitaji kwenda kupima yaaan uanza kujionyesha baada ya muda gani
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa ukimwi huonekana baada ya muda gani toka kuathirika?
Soma Zaidi...Walio katika hatari ya kupata homa ya inni
Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata homa ya ini,kwa sababu ya hali zao mbalimbali wanaweza kupata ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Nini husababisha maumivu ya tumbo chini ya kitomvu kwa wanawake na wanaumr?
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu. Ni katika maumivu amaboyo kwa wanaume mara nyingi huhusishwa an ngiri na kwa upande wa wanawake huhusishwa na chango hasa pale wanapokaribia kuingia katika siku zao. Ma
Soma Zaidi...Nini kinasababisha kizunguzungu?
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za kizunguzungu zinazotekea katika mwili wa binadamu
Soma Zaidi...Kiungulia, dawa yake na namna ya kuzuia kiungulia
Tambuwa kiungulia, sababu zake, dawa za kiungulia na namna ya kupambana na kiungulia
Soma Zaidi...Matibabu ya vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.
Soma Zaidi...