image

Dalili za ukimwi siku za mwanzo

Makala hii inakwenda kukupa majibu ya maswali mengi kuhusu VVU na UKIMWI. tutakwenda kuona kwa ufupi historian a chanzo cha VVU na UKIMWI. hatuwa za maambukizi ya VVU na ukimwi na dalili zake za kuonekana toka kupata maambukizi. Pia hapa utajifunza namna

Dalili za ukimwi siku za mwanzo

DALILI ZA UKIMWI SIKU ZA MWANZO
Bila shaka umeshawahi kujiuliza kuhusu dalili za mwanzo za VVU na ukimwi. Makala hii itakwenda kujibu baadhi ya maswali yako mengine ambayo ulikuwa ukijiuliza kama, ni zipi dalili za mwanzo za vvu na ukimwi, je ukimwi unaingiaje, ni nini kitatokea baada ya kupata virusi vya ukimwi na mengineyo zaidi. Makala hii ni moja ya makala zetu za kutoa elimu ya afya ili kuendelea kuelimusha jamii.



Je nini maana ya UKIMWI?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno Upungufu Wa Kinga Mwilini. Ukimw husababishwa na aina ya virusi inayojulikana kwa jina la VVU yaani Virusi vya ukimwi. Historia ya Ukimwi imeanza zamani sana toka miakaya 1950. Kuna nadharia nyingi sana kuhusu chanzo na asili ya ukimwi. Kisayansi nadharia inayokubalika ni kuwa chanzo cha ukimwi ni masokwe. Miaka ya 1980 ukimwi ndipo ulipoanza kujulikana rasmi.


Hatua za maambukizi ya VVU na UKIMWI
Mara tu baada ya mtu kupata maambukizi mapya, atapitia hatuwa kuu tatu kabla ya kuambiwa ana ukimwi. hatuwa hizi hutofautiana kwa dalili zake. Kutoka kuambukizwa virusi mpaka kuambiwa mtu ana ukimwi inaweza kuchukuwa miaka mitano hadi kumi. Wapo baadhi ya watu wakawa pungufu ya hapo ama Zaidi ya hapo. Hebu saa tuzione hatuwa hizi na dalili zake.



A. Hatuwa ya kwanza baada ya maambukizi mapya:
Hatuwa hii hupatikana mwanzoni mwa wiki za mwanzo kabisa baada tu ya kupata maambukizi mapya. Katika hatuwa hii mtu hawzi kupima akaonekana kuwa ana maambukizi. Katika hatuwa hii virusi vinakuwa ni vingi sana kwenye damu, na huzaliana kwa kasi sana. Na hapa mtu anaweza kuonyesha baadhi ya dalili. Kuonyesha dalili hizi inachukuwa wiki 2 hadi sita. Baada ya hapo hatoweza kuona dalili tena. Dalili za maambukizi ya VVU katika hatuwa hii ni kama:-

1. Kupata mafuwa
2. Vidonda vya koo
3. Uchovu
4. Homa
5. Maumivu ya kichwa
6. Kutokwana upele
7. Kuvimba na kuuma kwa tezi za shingo na mapajani.



B. Hatuwa ya pili baada ya baambukizi mapya
Hatuwa hii ni katika hatuwa hatari sana. Katika kipindi hiki kiwango cha virusi kwenye damu hupunguwa na virusi kuelekea maeneo mengine ya mwili na kuathiri seli hai nyeupe zinazojulikana kama VD4. Katika hatuwa hii mtu akipima ataonekana kama ameathirika, lakini hakuna dalili yeyote itakayoonekana kwa muathirika katika kipindi hiki chote. Hatuwa hii inaweza kudumu kwa muda wa miaka mitano hadi 10. Katika wakati huu wote virusi vitaendelea kuathiri na kuharibu seli za CD4 mabzo ndio mlinzi wa mwili.


Seli za CD4 ni nini na ni zipi kazi zake?
Kabla hatujaona hatuwa ya tatu kwanza tuone kwa ufupi ni nini seli za CD4. Katika damu kuna seli aina kuu tatu ambazo ni seli hai nyeupe, seli hai nyekundu na seli sahani. Kila moja kati ya hizi ina kazi yake maalumu. Kwa mfano:-



1. Kazi za seli hai nyekundu ni kusafirisha hewaa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu na kupeleka kwenye moyo ambapo husambazwa kuelekea maeneo mengine ya mwili. Seli hai nyekundu ndizo ambazo nyingi kwenye damu na ndio maana damu ni nyekundu. Pia kazi nyingine ni kusafirisha hewa ya kabonidaiyoksaidi kutoka kwenye seli kupeleka kwenye mapafu kupitia kweye moyo.



2. Kazi za seli sahani ni kusaidia katika kuganda kwa damu na kupona kwa vidonda. Endapo utakuwa umejikata na jeraha likawa linatoa damu, seli sahani hiletwa kwa wing eneolile ili kusaidia damu kutoendelea kutoka na kuganda eneo lile. Uponaji wa vidonda na majeraha pia huhitaji seli hizi.


3. Seli hai nyeupe kazi zake ni kulinda mwili zidi ya vijidudu vya maradhi kama bakteria, fangasi, virusi na protozoa. Kwa ufupi seli hizi ni kama ndio walinzi wa mwili endapo zitapunguwa mwili utakuwa hatarini. Seli hizi hutafuta vijidudu hivi popote vilipo na kuviuwa kwa kuvimwagia kemikalia mbazo zitavifanya vife. Seli hai yeupe ndizo huitwa cd4. Kwa hiyo kazi kuu ya seli za CD4 ni kupambana na vijidudu shambulizi ndaniya mwili.



Sasa virusi vya ukimwi (VVU) vinapoingia mwilini moja kwa moja hutafuta seli za CD4, Huziingia ndani yake na kuanza kuzaliana humo. Baada ya kuwa virusi bni vingi ndani ya sli hiyo hupasuka na kumwaga virusi nje, na seli ile hufa kabia. Maelfu ya virusi hivi vilivyitoka kwenye seli moja huvamia seli nyingine na mhakato hujirudia. Baada ya muda wa miaka kadhaa mtu huyu atakuwa na upungufu wa kinga mwilini na hapo ndipo huambiwa ana ukimwi.



C. Hatuwa ya tatu (ukimwi).
Kikawaida mtu mwenye afya aha seli za cd4 500 mpaka 1500 kwenye kipimo kimoja. Sasa kama ana VVU huanza kuharibu seli hizi hadi hupunguwa chini ya kiwango hiko. Zikipunguwa kutoka 500 hadi 200 hapa huambiwa mtu huy ana upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI. tafiti zinaonyesha kuwa baada ya kufikia hatuwa hii ya cd4 200 kama mtu huyu hataanza matibabu maalumu itachukuwa mikaa mitatu hadi kufariki. Hatuwa hii mgonjwa ataanza kuona dalili za ukimwi ambazo ni:-

1. Kupunguwa uzito kwa asilimia 10 bila ya sababu maalumu
2. Kuharisha mfululizo
3. Kuota upele kuzungukia maeneo mbalimbali ya mwili hadi sehemu za siri
4. Kuota majipu
5. Kusumbuliwa na fangasi mara kwa mara
6. Kuwa na homa za mara kwa mara
7. Kukonda sana bila ya sababu maalumu
8. Kuwa na uchovu wa mara kwa mara
9. Kupata maradhi nyemelezi kama kifua kikuu, kisukari, saratani, mkanda wa jeshi na mengineyo.



Nini mtu afanye baada ya kugundulika kuwa ni muathirika?
Vyema kwanza kupata ushauri kutoka kwa mtoa huduma ya ushauri nasaha. Hii itasaidia kumuweza mtu vyema kiakili, na kumuandaa kukabiliana na changamoto. Pia itamsaidia kujifunza Zaidi kuhusu namna ya kuishi na virusi vya ukimwi. pia atatakiwa kuanza matibabu haraka iwezekanavyo. Matibabu haya yatamsaidia ku:-

1. Kupunguza uzalishaji wa virusi vipya ndani ya mwili
2. Kuzuia virusi vya ukimwi visiharibu seli nyingine za mwili
3. Kumfanya mtu asifike kwenye hatuwa ya tatu ya kuambiwa ana ukimwi
4. Kupunguza uwezo wa mtu kumuambukiza mwingine.



Ni muda gani virusi huonekana kwenye kipimo?
Vipimo vya VVU vipo katika makundi kadhaa. Vipo ambavyo hipima kwa kutumia damu, vipo kwa kutumia mate. Tukiacha mbali hayo yote ni kuwa virusi vya ukimwi huanza kuonekana baada ya wiki tatu jhadi miezi mitatu kwa ajili ya uthibitisho Zaidi. Pia vipo vipimo ambavyo kuweza kuonyesha mapema Zaidi ila mara nyingi hivi havipatikani kwa urahiri.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1202


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Namna ya kuangalia Maambukizi kwenye mifupa.
Posti hii inahusu zaidi njia zinazotumika ili kuangalia Maambukizi kwenye mifupa. Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfupa
posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfupa ambao kitaalamu hujulikana Kama Soma Zaidi...

Dalili za Mgonjwa wa kisukari
Post hii inahusu dalili za mtu Mwenye ugonjwa wa kisukari, dalili hizi zinaweza kujitokeza Moja kwa Moja mtu akagundua kuwa ana Ugonjwa wa kisukari.zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kisukari. Soma Zaidi...

Dalili za za kuwepo kwa maambukizi chini ya kitovu
Posti hii inahusu zaidi dalili za kuonyesha kuwa Kuna maambukizi kwenye kitovu hasa hasa chini ya kitovu. Soma Zaidi...

Magonjwa ya moyo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu magonjwa ya moyo Soma Zaidi...

Dalili, chanzo, sababu na vmambo hatari kuhusu kifua kikuu
Katika makala hii utajifunza kuhusu kifua kikuu, dalili zake, sababu zake, chanzo chake na mambo hatari kwa mgonjwa. Soma Zaidi...

Mzio (aleji) na Dalili zake
Posti hii inahusu zaidi mzio na Dalili zake ni Dalili ambazo ujitokeza kwa mtu mwenye mzio, kuna wakati watu wengine ushindwa kutambua kuwa ni mzio au la, lakini leo tunaenda kujua Dalili za mzio kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Dalili kuu za minyoo
Minyoo ni katika viume wanyonyaji, wanaoishi katika miili ya viumbe hai na kujipatia chakula humo. Minyoo wanaweza kuishi kwenye maeneo yenye majimaji kama kwenye maji, ndani ya viumembe hai kama mtu, ngombe, ngure na paka. Minyoo pia wanaweza kuishi kwen Soma Zaidi...

Dalili za kifua kikuu kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kifua kikuu kwa watoto,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto pindi wanapopata Maambukizi ya kifua kikuu. Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa kisukari aina ya 1 (type 1)
Kisukari cha Aina ya 1, ambacho wakati mmoja kilijulikana kama Kisukari cha changa au Kisukari kitegemeacho insulini, ni hali sugu ambapo kongosho hutoa insulini kidogo au haitoi kabisa, homoni inayohitajika kuruhusu sukari (glucose) iingie kwenye se Soma Zaidi...

MARADHI MAKUU HATARI MATANO (5) YANAYOENEZWA KWA KUNG'ATWA NA MBU (malaria ndio inachukua nafasi ya kwanza)
1. Soma Zaidi...

Uwepo wa asidi nyingi mwilini
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kuwepo kwa asidi nyingi mwilini hali uwasumbua watu wengi na kufikia kiasi cha kusababisha madhara mengine mawilini ikiwamo pamoja na kansa ya koo, ili kujua kama una wingi wa asildi mwilini unapaswa kujua dalili kama ifu Soma Zaidi...