Chanzo cha kiungulia

Post hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa kiungulia, kiungulia ni kitendo cha kupanda kwa gesi kutoka kwenye tumbo mpaka kwenye mdomo,hali uwasumbua wengi na kusababisha hali isiyo rafiki.

Vyanzo vya kiungulia.

1. Kudhoofika kwa utendaji kazi wa kizuizi cha juu cha tumbo kwa kitaalamu huitwa (lower esophagus sphincter) sehemu hii uhakikishe kuwa kila kitu ambacho kinaenda mwilini hakirudi ila sehemu hii ikiharibika usababisha kurudi kwa vyakula na vitu vingine kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye mdomo.

 

2. Mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula .

Kwa sababu ya kuwepo kwa vyakula mbalimbali ambavyo uleta shida kwenye mmeng'enyo wa chakula kama vyakula vya mafuta, sukari, vyakula vya caffeine, chocolate na vyakula vya aina hiyo Usababisha mmeng'enyo wa chakula kutoenda sawa na hatimaye kusababisha kiungulia.

 

3. Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tindikali kwenye mmeng'enyo wa chakula,

Kwa kawaida tindikali ni lazima kwenye mmeng'enyo wa chakula ila ikizidi inaleta kiungulia aina hii ya tindikali ambayo ukaa tumboni kwa kitaalamu huitwa hydrocholic asidi, ikiwa nyingi upanda mpaka kwenye mdomo na kusababisha kiungulia.

 

4. Kuwepo kwa baadhi ya madini kwenye mwili .

Kwa sababu kwenye mwili wa binadamu kuna madini mbalimbali na kila aina ya madini ufanya kazi tofautitofauti na yakikosa  usababisha matatizo mengi mwilini . Kwa mfano ukosefu wa madini ya magnesium na potassium, yakikosa usababisha kuongezeka kwa kiungulia.

 

5. Kuwepo kwa uzito mkubwa na kitambi.

Kwa kawaida uzito mkubwa ni chanzo cha magonjwa mengi kwa sababu kuna watu wanene na hawafanyi mazoezi usababisha na wanaopenda kula sana usababisha chakula kupanda juu na kusababisha kiungulia.

 

6. Wamama wajawazito na wenye umri mkubwa.

Kuna wakati mwingine wamama wajawazito wanakuwa na kiungulia kwa sababu ya hali zao na wengine wenye umri mkubwa kwa sababu ya kushuka kwa immunity upate kiungulia.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/14/Thursday - 09:41:44 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1396


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-