Zijuwe sababu kuu zinazokufanya ukahisi maumivu makali ya tumbo kwa chini upande wa kushoto
MAUMIVU YA TUMBO KWA CHINI UPANDE WA KUSHOTO
Sehemu ya kushoto ya tumbo lako kwa chini hupatikana mwishilizo wa utumbo mkubwa. Pia kwa upande wa wanawake sehemu hii hupatikana ovari ya kushoto. Katika hali za kawaida maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto sio jambo la kuogopesha sana. Kwani maumivu haya yanaweza kuondoka yenyewe bila ya kuhitaji uangalizi wa kidaktari.
Je na wewe ni mmoja kati ya wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa shini upande wa kushoto? Je una muda gani na tatizo hili?. makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakwenda kukujuza sababu za maumivu ya tumbo sehemu ya chini upand wa kushoto.
Kama nilivyotangulia kukuijuza kuwa maumivu haya si jambo la kuogopesha. Basi ni vyema kwa haraka ukamuona daktari endapo utaona dalili zifuatazo:-
A.Homa
B.Sehemu husika kuwa na ugumu na maumivu
C.Kuvimba kwa tumbo
D.Kuona damu kwenye kinyesi
E.Kuendelea kuwa na kichefuchefu na kutapika kwa masik kadhaa
F.Kupungua uzito
G.Ngozi kuwa na njano.
Sababu za maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto
1.Kuwa na shida kwenye utumbo mkubwa.
Hii hutikea pale kwenye utumbo mkubwa kunapoota kama vijifuko vijidogo. Hivi sio jambo la kuogopa sana kiafya maana mara nyingi havina madhara na hupotea vyenyewe. Hali hii huwapata sana wenye umri zaidi ya miaka 40. sasa ikitokea vijifuko hivi vimeshambuliwa na vijidudu huvimba na kuleta maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto. Dalili zake ni kama:-
A.Homa
B.Kichefuchefu
C.Kutapika
D.Tumbo kujaa na kuiwa gumu
E.Kuharisha
F.Kukosa choo
2.Gesi tumboni.
Sababu nyingine ni kujaa gesi tumboni. Gesi tumboni inaweza kusababishwa na:-
A.Kumeza hewa sana
B.Kula kupitiliza
C.Kuvuta sigara
D.Kutafuna bigjii
E.Chakula kutokumeng’enywa vyema
F.Kula vyakula vyenye gesi
G.Kuwa na bakteria kwenye utumbo mkubwa.
3.Kuvimbiwa ama chakula kutokumeng’enywa vyema tumboni. Hali hii huplekea maumivu ya tumbo kwa juu. Maumivu haya wakati mwingine husambaa na kuathiri chini ya tumbo upande wa kushoto. Mtu pia ataona dalili kama:-
A.Kiungulia
B.Kuhisi kishiba na tumbo kujaa
C.Kucheua gesi
D.kichefuchefu
4.Ngiri henia; henia ina dalili kama:-
A.Kuongezeka uvimbe maeneo ya tumboni (si kila henia)
B.Maumivu kuongezeka
C.Maumivu wakati unaponyanyua kitu
D.Kujihisi umeshiba
5. kuwa na vijiwe kwenye figo
Vijiwe vya kwenye vigo vinatokana na mkusanyiko wa madini ya chumvi. Vijiwe hivi vinaweza kutokea kwenye figo, kibofu ama maeneo mengine kwenye mfumo wa mkojo. Vijijiwe hvi vinaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto. Pia vinaweza kusababisha maumivu ya mgongo upande mmoja na nyuma pia na kwenye mbavu. Tofauti na dalili hizi pia mgonjwa anaweza kupata dalili zifuatazo:-
A.Mkojo wenye rangi ya kahawiya, nyekundu ama mawingu mawingu na haruu kali
B.Mkojo wenye maumivu makali unaotokea mra kwa mara
C.Kichefuchefu
D.Vomiting
E.Homa
Maumivu ya tumbo kwa chini uapande wa kulia kwa wanawake, husababishwa na yafuatayo:-
A.Tumbo la chango
B.Kuota tishu za tumbo la uzazi maeneo mengine
C.Kuwa na shida kwenye ovari
D.Kuwa na ujauzito uliotungia nje
E.Kuwa na ugonjwa wa PID
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa kuziba kwa Njia ya machozi yaani kukosa machozi ambayo husababishwa na maambukizi.
Soma Zaidi...Hivi badovunasumbuliwa na fangasi kwenye mdomo ama ulimi. Ni dawa gani umeshatumia bila mafanikio?.
Soma Zaidi...maambukizi ya kawaida ya zinaa (STI), Hujulikana Kama Chlamydia. Huenda usijue una Ugonjwa huu kwa sababu watu wengi hawapati dalili au ishara, kama vile maumivu ya sehemu za siri na kutokwa na uchafu kutoka kwa uke au uume. Maambukizi haya huathiri
Soma Zaidi...Bipolar disorder ni hali ya afya ya akili inayohusisha mabadiliko makubwa katika hisia, nishati, na shughuli za kila siku za mtu. Dalili za bipolar disorder zinaweza kuwa kwenye kipindi cha mania na kipindi cha unyogovu, zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa bipolar.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Ugonjwa wa mdomo unaoungua ni neno la kimatibabu kwa ajili ya kuwaka moto mara kwa mara mdomoni bila sababu dhahiri. Usumbufu huo unaweza kuathiri ulimi wako, ufizi, midomo, ndani ya mashavu yako, paa la mdomo wako au maeneo yaliyoenea ya mdomo wako wot
Soma Zaidi...VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukutajia baadhi tu ya sababu zinazopelekea kuumwa na tumbo. Hali hizi zinawweza kuwapata watu wa jinsia zote katika umri wowote ule. Ijapokuwa nyingine si kwa wote ni kwa baadhi ya watu. hapa nitakuletea sababu 5 tu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea sababu za maumivu ya tumbo kitovu i
Soma Zaidi...