Afya ya akili ni hali ya mtu kuwa na akili timamu kiroho,kimwili ,na Kwa mazingira yake yote yaliyomzunguka na anaweza kuamua kitu akiwa katika ukamilifu, zifuatazo ni sababu za kuwa na Afya ya akili.
Tunapaswa kujifunza kuhusu afya ya akili kwa sababu nyingi muhimu kupitia kufahamu afya ya akili tunaweza kuishi vizuri pia kuweza kukubaliwa katika jamii,Kwa hiyo zifuatazo ni baadhi ya sababu za kujifunza afya ya akili.
1. Kuweza kutambua lipi la kufanya na Kwa wakati maalumu_tunapofahamu vizuri afya yetu ya akili hasa pale tunapokuwa na akili timamu tunaweza kutambua lipi la kufanya na Kwa wakati maaalumu,kuacha ambayo yasiyofaa kwenye jamii na kufanya yanayokubalika katika jamiii husika,hiyo ndio sifa mojawapo inayotutenganisha na vichaa na watu wenye afya njema ya akili.
2.Kuelewa nafsi zetu – kutusaidia kujitambua, kudhibiti hisia na kushughulika na changamoto za maisha, mtu akishakuwa na afya nzuri ya akili ana uwezo wa kujitambua yeye ni nani,ana uwezo wa kudhibiti hisia zake mfano wa hisia za kupenda,kuchukia na mambo mbali mbali ana uwezo wa kutawala Kila aina ya hisia na pia uwezo wa kupambana na hali halisi ya maisha, katika umakini anaweza kupambana katika kupata mahitaji anaweza kuridhika na Kila hali hasa pale anapokumbana na hali isiyo ya kawaida mtu mwenye afya ya akili anaweza kuona Cha kufanya.
3. Kuzuia matatizo – tukijua dalili na ishara za matatizo ya akili mapema, tunaweza kuyadhibiti kabla hayajawa makubwa,hali hii ya kuzuia matatizo mbali mbali ni ishara kwamba mtu ana afya ya akili,ni kweli sio Kila aina ya matatizo inawezekana kuzuiwa ila kama afya yako ya akili unafanya kazi vizuri Kuna baadhi ya ishara unaweza kuziona na kutabiri Kuna kitu au Kuna ishara inaweza kuleta matatizo na kuwa macho ili kuzuia hilo tatizo.mfano ukiwa na mtoto mvivu usipotambua ishara hiyo haraka na ukamsaidia mtoto kufanya kazi na kumwambia madhara ya uvivu unakuwa hauna afya nzuri ya akili,ila ukitambua mapema na ukamsaidia ni ishara mojawapo ya kuona ishara na ukazuia tatizo.
4.Kupunguza unyanyapaa – elimu ya afya ya akili hutusaidia kuelewa kuwa matatizo ya akili ni hali za kiafya kama magonjwa mengine, na siyo aibu.ni kweli mtu akitambua kwamba ana afya nzuri ya akili anao uwezo wa kutambua kwamba Kuna watu wengine wanahitaji msaada au uwezo wa kutambua kwamba binadamu wote hatuko sawa Kuna wengine wanahitaji msaada na Kuna wengine afya zao za akili haziko sawa na wapo tayari kuwasaidia na kuwajali wengine hali inayosababisha kuondoa unyanyasaji au kunyanyapaa wengine katika jamii.
5. Kuboresha mahusiano – mtu mwenye afya nzuri ya akili hushirikiana vyema na familia, marafiki na jamii.Afya ya akili ni kipau mbele katika kuleta mahusiano kwenye jamii Kwa sababu jamii kubwa ya watu ukiwa vizuri kwenye upande wa afya ya akili ni kitu kinacholeta mahusiano katika jamii Kwa sababu Kuna kujaliana na kuonyesha utu na kushirikiana vyema na kuwa sawa katika jamii hali inayoleta usawa katika jamii na mahusiano mema.
6.Kuongeza tija – afya njema ya akili inachangia mtu kufanya kazi vizuri, kusoma kwa bidii na kutumia uwezo wake ipasavyo.kwa sababu mtu akiwa na afya ya akili anakuwa vizuri kisaikolojia,kiafya,kibaiologia na sehemu zote zinazomzunguka mtu,hali hii umefanya mtu afanye kazi vizuri Kwa kutumia akili yake Kwa sababu Kila sehemu oliyomzunguka ipo vizuri na pia kama ni mwanafunzi atasoma vizuri na kufaulu masomo yake.
7. Kujenga jamii yenye mshikamano – jamii yenye uelewa wa afya ya akili husaidiana, hulinda wanaopitia changamoto, na hupunguza matatizo ya kijamii kama vurugu, uraibu na msongo.
Kwa kifupi, kujifunza kuhusu afya ya akili kunatusaidia kuishi maisha bora, yenye furaha na yenye tija binafsi na kijamii na pia kutasaidia kuweza kutambua lililojema na kutenda yaliyo mazuri.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu dalili za figo.figo husawazisha maji mwilini pamoja na kuchuja mkojo.
Soma Zaidi...Hawa huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenda maeneo mengine nyeti sana ya mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Soma Zaidi...Mie ni kijana wa kiume umri 33, nna tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nna minyoo lakini hata nikinywa dawa sioni afadhali, niliona labda ni pombe nikapumzika kunywa tatizo lipo pale pale japo nisipokunywa haliwi kwa ukubwa ule ila lipo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kushindwa kushuka kwa makende kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye skolatumu(scrotum).
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini
Soma Zaidi...Post hii inazungumzia zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindu.kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu anaitwa vibrio cholera.mdudu huyu hushambulia utumbo mdogo na kusababisha madhara mengi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za ugonjwa wa Dondakoo,hali hii utokea iwapo ugonjwa haukutibiwa mapema au umetibiwa lakini bado Kuna matokea hasi ambayo yanaweza kujitokeza kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisichokuwa na damu
Soma Zaidi...