Dalili za ugonjwa wa kaswende
Post hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kaswende kwa wajawazito, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa watu wote, kwa sababu ugonjwa huu una dalili ambazo upitia kwa hatua mbalimbali kama tutakavyoona.
Dalili za ugonjwa wa kaswende.
1. Kwa kuwa tangu mwanzoni nimejaribu kueleza kwamba ugonjwa huu upitia kwenye hatua mbalimbali,kwa hiyo tutaanza na hatua ya kwanza ambayo kwa kitaalamu huitwa primary symptoms, kwenye hatua hii mgonjwa anakuwa na vipele ambazo havina maumivu kwa kitaalamu huitwa chancres hivi vidonda hivyo ujitokeza baada ya wiki tatu baada ya maambukizi, hivi vidonda mara nyingi utokea sehemu ambayo sex imefanyiwa kama ni mdomoni vitajitokeza hapo kama ni kwa njia ya haja kubwa vitajitokeza hapo au kama ni kwa njia ya kawaida na penyewe vitajitokeza hapo, kwa hiyo vidonda hivyo kama havijapata matibabu utoweka ndani ya wiki tatu mpaka sita.
2. Kwa hiyo kama ikitokea mtu akapatwa na tatizo kama hili na anajua kabisa alifanya ngono bila kinga ni vizuri kabisa kupata matibabu mapema ili kuondoa tatizo kubwa kubwa zaidi, changamoto ni kwamba vidonda hivi mara nyingi huwa haviumi ndio maana watu wengi hawajishughulishi kupima badala yake ni kupotezea na ukizingatia havina maumivu yoyote, madhara ya kutotibu mapema usababisha hali ambayo sio nzuri kama tutakavyoona hapo baadaye.
3. Hatua ya pili utokea pale ambapo vidonda vya hatua ya kwaza kutotibiwa , hatua hiyo kwa kitaalamu huitwa primary symptoms,hivi vidonda ambavyo vilikuwepo vinatudi tena sio kwenye sehemu ambayo sex ilifanyika tu bali ni katika sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye mikono hasa hasa kwenye sehemu ya viganja, kwenye miguu hasa kwenye ukanyagio,pia na rangi yake inakuwa kama ya nyekundu ila sio nyekundu iliyokaza, na pia vidonda hivi vinaweza kuwa hata mdomoni, hali hiyo utokea kwa sababu ya ugonjwa kueneza kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
4. Katika hatua hii mgonjwa anaweza kushindwa kutembea kwa sababu ya kuwepo kwa vidonda kwenye nyayo za miguu na wakati mwingine hatua hii uambatana na homa, mwili mzima kuchoka,Madonda kwenye koo, kuvimba kwa lymph nodes kwa sababu ya maambukizi, pengine nywele kwenye kichwa unyonyoka , maumivu makali ya kichwa, kupungua uzito, na pia mwili kuishiwa nguvu.
Pengine watu uchanganya dalili hizi na mgonjwa wa HIV kwa sababu dalili za mgonjwa wa HIV hatua ya nne na tatu huwa na dalili kama hizi, mtu kuja kufikia hatua hiyo ni kwamba ugonjwa huu unakuwa umemaliza miaka kama kumi na tano mwilini na ndipo dalili za hapo juu zinaweza kutokea.
5 . Kwa hiyo jamii inapaswa kuelezwa wazi kuhusu ugonjwa huu kwa sababu kuna wakati watu wanaenda kupima baada ya kuona dalili kama hizi wakidhani ni maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, na baadae unakuta mtua anapewa majbu kwamba hana maambukizi ya ukimwi na ni kweli anakuwa hana ila shida watu wengi hawapimi kaswende na yenyewe kama haijatibiwa inaweza kumfikisha mtu sehemu mbaya , kwa hiyo kupima kaswende ni lazima ili kuweza kuepukana na matatizo mbalimbali.
6. Pia hatua ya mwisho ni hatua ya tatu ambayo kwa kitaalamu huitwa latent phase, ni hatua ya mwisho utokea mara nyingi kama hatua ya pili haijatibiwa na kama matibabu hayajafikiwa mgonjwa anaweza kupoteza maisha, kwa hiyo kupima kaswende ni lazima ili kuweza kuepukana na vifo vya akina mama na watoto wao, twende hospitali dawa ipo na watu wengi wanapona.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π2 Madrasa kiganjani π3 Bongolite - Game zone - Play free game π4 kitabu cha Simulizi π5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Dalili za mimba ya mtoto wa kiume
βPost hii inachunguza mada maarufu ya dalili za ujauzito zinazohusishwa na kubeba mtoto wa kiume. Tutatofautisha kati ya ngano za jadi na ukweli wa kisayansi, huku tukitoa mwongozo wa jinsi ya kupata majibu sahihi kuhusu jinsia ya mtoto wako.
Soma Zaidi...Sababu za maambukizi kwenye nephoni
Posti hii inahusu zaidi sababu za maambukizi kwenye nephroni, ni vitu vinavyosababisha mabukizi kwenye nephroni.
Soma Zaidi...Sababu za homa kwa watoto wachanga
Muhtasari (Executive Summary) βHoma kwa mtoto mchanga si ugonjwa wenyewe, bali ni ishara kwamba mfumo wa kinga ya mwili unapambana na kitu kigeni. Ingawa homa inaweza kuwatia hofu wazazi wengi, mara nyingi husababishwa na maambukizi ya virusi, bakteria, mabadiliko ya mwili kama kuota meno, au matokeo ya kawaida ya chanjo. Makala haya yanachambua sababu hizi kwa kina na kutoa mwongozo wa lini unapaswa kukimbilia hospitali haraka.
Soma Zaidi...MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik.
Soma Zaidi...Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu
Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo.
Soma Zaidi...Dalili za mtoto Mwenye UTI
Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Soma Zaidi...