Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya maradhi haya ya ukimwi, dalili zake, tiba na kinga zake na mengineyo zaidi.
YANAYOKUPASA KUYAJUWA KUHUSU UKIMWI,DALILI ZAKE, MATIBABU YAKE NA CHANZO CHAKE
Ukimwi ni katika moja ya maradhi ambayo yanaweza kumuathiri mtu kimwili na kiakili. Pia inaweza kumuathiri mtu kijamii, na hii ndio maana watu wengi wamekuwa wakiogopa kupata ukimwi zaidi kuliko maradhi mengine yaliyo hatari. Ukweli ni kuwa ukimwi ni hatari kwa sababu unamuuwa mtu kidogokidogo kwa muda wa miaka mingi, lakini yapo maradhi hatari zaidi kuliko UKIMW. Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya maradhi haya ya ukimwi, dalili zake, tiba na kinga zake na mengineyo zaidi.
Ni nini maana ya Ukimwi?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno "upungufu wa kinga mwilini" ni hali sugu, inayoweza kutishia maisha inayosababishwa na virusi vya Ukimwi (VVU). Kwa kuharibu mfumo wako wa kinga, VVU huingilia uwezo wa mwili wako kupambana na viumbe vinavyosababisha magonjwa. Viumbe hivyo ni kama bakteria, virusi, protozoa, fangasi na vinginevyo.
Nini maana ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)?
VVU ni ufupisho wa maneno Virusi Vya Ukimwi, ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini. Hudhoofisha mwili uwezo wake kujilinda dhidi ya vijidudu vya maradhi. Neon hili kwa lugha ya kiingereza hufupishwa kama HIV.
VVU ni maambukizo ya zinaa. Yanayoweza pia kuenezwa kwa kuongezewa damu iliyoambukizwa au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kunyonyesha. Inaweza kuchukua miaka mimngi huwenda 5 mpaka 10 kabla ya VVU kudhoofisha kinga yako ya mwili hadi kufikia ukimwi.
HATUWA ZA MAAMBUKIZO YA VVU
1. Hatua ya kwanza ya maambukizi (Primary infection)
Watu wengi walioambukizwa na VVU hupata ugonjwa unaofanana na Homa ndani ya mwezi mmoja au miwili baada ya virusi kuingia mwilini. Hivyo kutengeneza dalili za awali za VVU na UKIMWI. Dalili hizi si lazima zimpate kila mtu, wapp wengine hawazipati kabisa. Sana dalili hizi hutokea wiki mbili toka kupata maambukizi mpaka wiki nne kisha hupotea. Kwa baadhi ya watu zinaweza kuanzia wiki ya kwanza, na wengine kuishia wiki ya sita. Dalili hizo ni:-
1.Kupatwa na homa.
2.Maumivu ya kichwa yasiyo na sababu
3.Maumivu ya misuli
4.Kuota upele
5.Kupatwa na baridi ama kuhisi baridi.
6.Kukauka na koo ama kupatwa na vidonda kooni.
7.Kupatwa na Vidonda vya kinywa au sehemu za siri
8.Kuvimba kwa Tezi za limfu kwenye mapaja, makwapa na haswa kwenye shingo
9.Mwili kuwa na Maumivu bila ya sababu maalumu.
10.Kutokwa na Jasho la usiku
11.Kuharisha
2. Hatuwa ya pili Toka kuambukizwa.
Kama tulivyoona dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza. Sasa hutokea kwa baadhi ya watu kuwa tezi za limfu zisivimbe wakati wa hatuwa ya kwanza, ila zikavimba katika hatuwa hii ya pili. Tofauti na hili hakuna dalili nyingine maalumu ya VVU katika hatuwa hii ya pili. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka miaka 10. Kwa watu wengi ni kati ya miaka 4 mpaka 10 ila wengine mara chache hutokea ikawa chini ya hapo.
Kuendelea kwa UKIMWI
Ikiwa hautapata matibabu maalumu ya ART na kutumia ARV mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuthibiti maambukizo yako ya VVU, ugonjwa huendelea hadi kufikia kuwa UKIMWI kwa takriban miaka 10. Wakati huu ukiwa na UKIMWI unakua, mfumo wako wa kinga umeharibiwa sana, na hivyo kukufanya uweze kuambukizwa na magonjwa nyemelezi - Mgonjwa nyemelezi ni magonjwa ambayo hayangemsumbua mtu aliye na kinga nzuri.
SASA UKIMWI UNATOKEAJE?
Seli ndio matofali yaliyojengea miili yetu. Ndani ya miili yetu kuna aina nyingi za seli, na seli za damu. Ndani ya damu pekee kuna aina zisizopunguwa tatu za seli. Kuna seli hai nyekundu, nyeupe na seli sahani. Kila seli kati ya hizi ina kazi zake. Sasa hii seli hai nyeupe yenyewe ndio inakazi ya kupigana na vijidudu vya maradhi vinapoingia katika miili yetu. Vijidudu hivyo vinaweza kuwa bakteria, virusi ama fangasi. Seli hizi ndizo ambazo ambazo huitwa CD4.
Sasa virusi vya VVU vinapoingia mwilini vinaanza kuharibi hizi seli ambazo zinalinda mwili. Kawaida mtu anaweza kuwa na seli hizi 500 mapa 1500 katika kipimo kimoja. Sasa VVU vinaanza kuziharibu hizi na kupunguza idadi yake. Na kila seli hizi zikipunguwa ndipo mfumo wa kinga unavyoendelea kuharibika na ndivyo maradhi yanapozidi kupata nafasi ya kuingia mwilini.
Sasa endapo zimeharibiwa na kufika idadi ya 200 katika kipimo kimoja hapa mtu huyu ataambiwa ana Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI. Katika hatuwa hii mtu atakuwa akinyemelewa na maradhi nyemelezi kama fangasi, kifuwa kikuu, na mengineyo.
NINI CHANZO CHA VV NA UKIMWI?
Mpaka sasa chanzo halisi cha VVU bado ni mada tatizi. Ijap[okuwa wengi wanakubaliana na nadharia kuwa VVU asili yake ni masokwe, na ni huko Afrika huhusani maeneo ya Misitu ya Kongo. Yaani eti hapo zamani Waafrika wa maeneo hayo walikuwa wakiwinda masokwe kwa ajili ya kula nyama. Kumbe masokwe hayo yalikuwa na VVU. Hivyo kuingiliano huu ukapelekea watu kupata VVU. Kisha vikaanza kusafiri kutoka hapo, utandawazi na ukoloni, ukimbizi na miingiliano ya kibiahsara ilipelekea kuenea kwa kasi virusi hivi.
Dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza
1.Homa
2.Kuhisi baridi ama kutetemeka
3.Uota upele
4.Kutokwa na jasho wakatio wa usiku
5.Maumivu ya misuli
6.Kupata vidonda vya koo, ama kuwasha kwa koo.
7.Uchovu mkali usio elezeka
8.Kuvimba kwa tezi node za lymph yaani kuvimba tezi za mtoki mapajani, kwapa na shingoni.
9.Kupata vidonda kwenye mdomo
Dalili za Ukiwmi:-
1.Kupunguwa uzito kwa haraka bila ya sababu maalumu ijulikanayo
2.Kupata homa kali za mara kwa mara na kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku.
3.Kuchovu mkali sana usiojulikana sababu.
4.Kuendelea kuvimba kwa tezi za mtoki, kwapa na shingo
5.Kuharisha kunakoendelea zaidi ya wiki moja
6.Kutokwa na vidonda kwenye mdomo, ulimi, mkundu na sehemu za siri.
7.Kubana kwa pumzi
8.Kupoteza kumbukumbu, kukasirika mara kwa mara, ama kupoteza uwezo wa kuthibiti akili (kuchanganyikiwa)
9.Kuota mapele, majipu, mabumbuza kwenye ngozi, kope, pua na mdomoni.
VIPIMO VYA VVU:
VVU vinaweza kuonekana mapema sana kulingana na aina ya vipimo. Vipo vipimo ambavyo vinaweza kugunduwa virusi mapema sana hata ndani ya wiki. Hivi hutumiaka sana maabara na si rahisi kuvipata. Hapo chini nitataja baadhi ya vipimo ambavyo hupatikana karibia maeneo mengi
Kuna aina nyingi za vipimo vya VVU. Hapa nitataja baadhi tu ya aina za vipimo hivyo:-
1. Kipimo kinachohuisisha Muunganiko wa HIV antibody na antigen. Chenyewe kinaweza tu kupima damu ya mtu. Hivi vinatumika kugunduwa antigeni ijulikanayo kama p24. antigeni p24 ni chembechembe inayozalishwa mwilini baada ya kupata maambukizi, hivyo kama itakuwepo kwenye damu inamaana mtu atakuwa ameathirika. Kipimo hiki kinaweza kugunduwa virusi mwilini kuanzia wiki 2 mpaka 6 toka kuambukizwa. Yaani kuanzia wiki 2 mpaka mweni mmoja na nusu.
2.kipimo cha HIV antibody testing. Kipimo hiki kinaweza kupimwa kwa kuchukuwa damu ya mtu ama majimajinya wili wake. Chenyewe kinapima VVU mwilini kuanzia wiki ya 3 mpaka wiki ya 12 yaani wiki tatu mapaka miezi mitatu.
3.Kipimo kuangalia viral load; huu ni upimaji wa kiasi cha virusi kwenye kipimo cha damu. Ni kuwa kama kiasi cha virusi kwenye damu yako ni kikubwa sana unaweza kuwa dhaifu kuliko ambaye kiasi chake ni kidogo.
4.Kipimo cha kuangalia drugs resistance. Hapa ni kuangalia uwezo wa mwili kama utakuwa msugu kutumia aina flani ya ART.
MATIBABU YA VVU NA UKIMWI
Kama ijulikanavyo kuwa hakuna dawa ya kutibu kabisa IKIMWI ila zipo dawa za kusaidia kuishi nyema kama kawaida bila ya kupata usumbufu wowote. Dawa hizi husuia yharibifu wa mfumo wa kinga usiendelee. Kwa ufupi matibabu haya kuzuia ukuaji na uongezekaji wa VVU mwilini. Matibabu haya hujulikana kama ART. Yaani Anti Retroviral Theraphy, na dawa zake hujulikana kama ARV yaani Anti Retroviral Virus. Dawa hizi zimegawanyika katika makundi kama:-
1.Reverse transcriptase (RT) inhibitor. Hizi huzuia virusi kujizalisha na kuongezeka.
2.Protease inhibitors. Hufanya virusi vishindwe kufanya kazi vyema.
3.Fusion inhibitors. Hivi huzuia virusi kuingia mwilini
4.Integrase inhibitors. Hizi huzuia HIV kujizalisha
5.Multidrug combination. Huu ni muunganiko wa dawa hizi zaidi ya moja.
Kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI
Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-
A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendo
B.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6
C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.
Kwa nini ni muhimu kutumia ARV?
Kwa kuwa sasa umeshajuwa kuwa usipotumia dawa unaweza kuishi zaidi ya miaka 10.sasa nikujuze faida za kutumia dawa hizi:-
1.Kuzuia uzalishaji wa virusi vya UKIMWi
2.Kuongeza umathubuti wa kinga ya mwili na kurefusha muda wa kuishi
3.Kupunguza uwezekano wa kuambukiza watu wengine.
Je naweza kufanya ngono na aliyeathirika na nisiathirike?
Ndio inawezekana kabisa kwa sababu zifuatazo:-
1.Kama umetumia kinga (kondomu)
2.Kama hakukutokea muchubuko wakati wa tendo la ndoa
3.Kama mgonjwa ametumia ARV kwa muda mrefu angalau kwa miezi 6 na kutumi na hali hiyo kwa muda zaidi hata akafikia kiasi idadi ya virusi haionekani kwenye kipimo.
Dawa ya kuzuia kuathirika kwa walio hatarini zaidi.
Kuna watu wapo hatarini sana kuathirika. Kwa mfano madaktari na wakunga, muda wowote wanaweza kuathirika. Shuikrani ziwaendee wataalamu wa dawa, wametuletea dawa inayotambulikwa kwa PrEP au kwa kirefu pre-exposure prophylaxis. Hii ji dawa inayotumika kwa dharura endapo umepatwa na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukupelekea kuathirika. Dawa hii inafanya kazi ndani ya masaa 72 baada ya kupata virusi. Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii ni bora kwa asilimia 80 inaweza kuzuia kmaambukizi ya muda mfupi.
Utaratibu wa maisha kwa aliyeathirika
1.Jilinde na maambukizi
2.Punguza misongo ya mawazo
3.Tumia kondomu wakati wa kushiriki ngono
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Kula mlo kamili
6.Wacha kuvuta sigara
7.Wacha ama punguza kutumia vilevi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1905
Sponsored links
๐1
kitabu cha Simulizi
๐2
Kitau cha Fiqh
๐3
Simulizi za Hadithi Audio
๐4
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
๐5
Madrasa kiganjani
๐6
Kitabu cha Afya
Sababu za ugonjwa wa mkojo kuwa na damu
Posti hii inaelezea sababu zinazosababisha mkojo kuwa na damu. Soma Zaidi...
Namna Maambukizi kwenye milija na ovari yanavyotokea
Post hii inahusu zaidi namna Maambukizi kwenye milija na ovari ambayo yanatokea,Mara nyingi usababisha na bakteria wanaoweza kuingia kupitia sehemu mbalimbali. Soma Zaidi...
Je kwa mfano mimi nmeupata ukimwi leo na sihitaji kwenda kupima yaaan uanza kujionyesha baada ya muda gani
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa ukimwi huonekana baada ya muda gani toka kuathirika? Soma Zaidi...
Sababu za vidonda sugu vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za vidonda vya tumbo sugu Soma Zaidi...
Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo
Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa. Soma Zaidi...
Ni Nini husababisha kinjwaa kutoa harufu mbaya?
Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya? Soma Zaidi...
Dalili za Ugonjwa wa Ebola.
Virusi vya Ebola ni virusi vinavyohusiana vinavyosababisha Homa zaรย hemorrhagic magonjwa yanayoambatana na kutokwa na damu nyingi (kuvuja damu), viungo kushindwa kufanya kazi na, mara nyingi, kifo. Virusi vya Ebola na virusi huishi kwa wanyama, na wanad Soma Zaidi...
Je ugonjwa wa pumu uneweza kusababisha kifo, na nini kifanyike kupunguza madhara?
Ugojwa wa pumu ni hatari na unaweza kutokea ghafla. Lakini je unaweza kusababisha kifo, makalahii itakwend akujibu swali hili Soma Zaidi...
Sababu za Maumivu ya shingo
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maumivu ya shingo na ndani yake kunasababu zinazopelekea shingo kupata maumivu. Soma Zaidi...
Ugonjwa wa macho
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa macho, ni ugonjwa ambao ushambulia zaidi sehemu za nje za macho ambazo kwa kawaida uitwa conjunctiva na cornea hizi sehemu zikipata maambukizi zisipotibiwa mapema uweza kusababisha upofu kwa mgonjwa. Soma Zaidi...