image

NJIA YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA VIRUSI VYA VYA UKIMWI NA ATHARI ZAKE

Posti hii inahusisha maambukizi ya virusi vya ukimwi .pia  tutangalia  njia za kujikinga na  ugonjwa wa UKIMWI

 

        NJia za kujikinga na ugonjwa wa ukimwi.

  1. Kulingana na  ilivyoelezwa apo mwanzo  kwamba  tutangalia njia za maambukizi ya virusi vya ukimwi.hivyo hivyo mtu mwenye virusi vya ukimwi au mtu yoyote hambaye hana ni marufuku kutotumia miswaki mmoja.
  2. Kuacha kabisa kufanya ngono umri mdogo chini ya miaka 18.pia ata hivyo kuna njia nyingi za maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.njia ya ngono ndo njia inayongoza kuwa na maambukizi mengi sana . Pia ukiangalia sahivi watu wanaoishi katika kundi ili wengi ni vijana walio na umri wa miaka hiyo .hivyo ukiacha ngono utakuwa umejiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa njia ya ngono.
  3. Kuepuka kishirikiana vifaa vyenye ncha kali kama  wembe, sindano ,mikasi ,na vifaa vya kutobolea masikio,pamoja na vifaa vya kunyolea nywele.
  4. Kuepuka kuchangia nguo za ndani na taulo.Nguo hizi zinaweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI .
  5. Kutumia glavu unapokuwa unamuhudumia mgonjwa wa virusi kama atakuwa ametokwa na maji au damu
  6. Kuhakikisha kuwa wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wanapata ushauri wa daktari
  7. Kuhakikisha kuwa wenye maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi wanapata matibabu sahii.
  8. Mama mjamzito na mume wake kuhudhuria kiliniki mapema ili wachunguzwe kama wana maambukizi ya virusi vya ukimwi wakigundulika wapate tiba sahii .pia  mama lazima apate dawa ya kuzuia maambukizi kwa mtoto aliyetumboni mwake.

9.Mama mjamzito anashauriwa kujifungulia hospitalini ili kama mtoto ameathirika apate matibabu ya haraka iwezekanavyo.   

    

        Athari za maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

  1. KUtokana na hivyo tulivyoeleza kuhusu maambukizi ya  mgonjwa anashauriwa kuwahi hospitalini ili kuangalia hali yake
  2. Athari nyingine unafhoofika kwa mwili na kupungua kwa kinga ya mwili .pia huweza kusababisha magonjwa nyemelezi na hatimaye kifo.
  3. Kuharisha mara kwa mara.hii ni mojawapo ya athari ya virusi vya ukimwi.mtu kuharisha inatokana na virusi vya ukimwi kuwa vina nguvu nyingi kwenye mwili.
  4. Kukosa nguvu na kuchoka
  5. Kupata magonjwa ya ngozi kama chunusi sugu na mabakamabaka.
  6. Kupata homa mara kwa mara

        7.kukohoa mara kwa mara.

 

                Kulingana hayo kuna mambo pia ya kuzingatia kwa mtu anayeishi na virusi vya ukimwi.

1.usafi.mtu anayeishi na virusi vya ukimwi na ukimwi anatakiwa kuzingatia usafi wa mwili,nguo na mazingira yanayomzunguka.Anatakiwa kuoza na kuvaaa nguo safi.mgonjwa wa UKIMWI anaweza kushindwa kufanya usafi binafsi na sehemu za kulala.hivyo ni muhimu kumsaidia kufanya usafi wa mwili kama vile kukata kucha ,nywele na kumwogesha .nguo za kuvaaa zinapaswa kuwa safi mda wowote .pia ni muhimu kumfulia nguo zake za kuvaaa na matandikio .Ni vizuri kuchukua tahadhari wakati wa kumhudumia mgonjwa ili kuepuka kuambukizwa virusi.

 

2.lishe bora,.tumeangalia apo mwanzo kwamba virusi vya ukimwi husababisha kupungua kwa kinga mwilini.lishe bora huongeza kinga ya mwili .watu wanaoishi na virusi vya ukimwi huitaji lishe bora ili kiongozi kinga ya mwilini.

 

3.usalama wa lishe,.watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wako katika hatari ya kuambukizwa maradhi mengine kwa urahisi .hii inatokana na kupungua kwa kinga mwilini.chakula kinaweza kuwa miongoni mwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kama hakitandaliwa kwa kuzingatia usafi.ili chakula kiwe safi na salama ni muhimu kuzingatia usafi wa mara kwa mara wakati wa kuandaa chakula.unatakiwa uzumie vyombo safi wakati wa kuandaa kula chakula vyombo vinatakiwa kuishiwa vizuri kwa sabuni na maji safi na salama.vyombo lazima vianikwe au vipanguswe na kitambaa safi. 

   

Mtu anayeishi na virusi vya ukimwi anapaswa kula mlo kamili kila siku.chakula kinatakiwa kiwe safi na salama .chakula kifunikwe kwa kutumia mfuniko safi ili kuzuia vumbi na wadudu.mtu anayeishi na virusi vya ukimwi anatakiwa kula chakula cha moto .matunda na mboga mboga hasa zile zinazoliwa bila kupikwa zioshwe kwa maji safi na salama.

 

Pia mtu anayeishi na virusi vya ukimwi anatakiwa kuepuka vyakula viliyosindikwa .vyakula hivi mara nyingi husindikwa kwa kemikali ambazo zinaweza kuleta madhara kwa mgonjwa.vilevile ,haishauriwi kula chakula kilichokaa zaidi ya saa mbili bahada ya kupikwa kinatakiwa kipashwe moto mpaka kichemke kabla ya kula.

Kama ilivyo kwa watu wengine ,mtu anayeishi na virusi anatakiwa kunywa maji safi na salama ,maji ya kunywa yatunzwe katika chombo safi chenye mfuniko na kuweka mahali safi.

 

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3270


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Walio kwenye hatari ya kupata UTI
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata UTI, ni watu ambao wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa UTI kwa sababu ya mazingira mbalimbali kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Sababu kuu za maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, Tumbo la ngiri na chango
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake Soma Zaidi...

Madhara ya fangasi.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya fangasi za ukeni kwa kawaida tunajua kubwa fangasi zikiingia kwenye uke usababisha madhara mbalimbali ambayo mengine yanaweza ya kudumu na mengine ya mda kama yametibiwa mapema. Soma Zaidi...

Je mtu akapima ukimwi na kile kipimo kidogo .je kina usahihi au la ..na pia kama inaonyesha mistari miwili.
Hivi umeshawahi kuwazakuwa jekipimo cha HIV ni sahihi kwa kiasi gani. Unadhani huwa kinakoseaga kutoa majibu? Soma Zaidi...

Dalili za ukosefu wa misuli.
Posti hii inahusu dalili za ukosefu wa misuli. ukosefu wa udhibiti wa misuli wakati wa harakati za hiari, kama vile kutembea au kuokota vitu. Ishara ya hali ya msingi, Ataxia inaweza kuathiri harakati, hotuba, harakati za jicho na kumeza. Soma Zaidi...

Sababu za mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu.
Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine. Soma Zaidi...

Fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Dalili za kwanza za HIV na UKIMWI kuanzia wiki ya kwanza toka kuathirika
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Soma Zaidi...

Aina za fangasi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya aina za fangasi Soma Zaidi...

Matatizo ya mapigo ya moyo
posti hii inazungumzia kuhusiana na matatizo ya mapigo ya moyo.Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, unaodunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza k Soma Zaidi...

Sababu za kunyonyoka kwa nywele
Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya mapafu
Saratani ya Mapafu ni aina ya Kansa inayoanzia kwenye mapafu. Mapafu yako ni viungo viwili vya sponji kwenye kifua chako ambavyo huchukua oksijeni unapovuta na kutoa kaboni dioksidi unapotoa nje. Soma Zaidi...