Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni.
Maumivu ya tumbo kitomvuni
Maumivu ya tumbo kwenye kitomvu, yanaweza kuwa ni ishara ya maradhi mengi. Mara nyingi maumivu haya yanaweza kuondoka yenyewe baada ya muda. Ila wakati mwingine yanaweza kuwa ni ishara ya shida za kiafya ambazo huhitaji uangalizi wa daktari kwa haraka. Kwa wanaume huwa henia ikisumbuwa sana eneo hili.
Je na wewe ni mwene kusumbuliwa na maumivu ya tumbo kwenye kitomvu? Makala hii ji kwa ajili yako. Hapa tunakwenda kuona sababu za maumivu ya tumbo kwenye kitomvu, dalili na maradhi yanayohusiana na maumivu ya tumbo kitomvuni. Unaweza kutuachia maoni yako hapo chini.
Eneo hili la kitomvuni kitaalamu hufahamika kama umblical region. Eneo hili la tumbo linahusisha viungo kama tumbo la chakula, utumbo mdogo, utumbo mkubwa na kongosho. Hivi ni katika viungo muhimu sana katika mmengenyo wa chakula, na afya ya mtu kwa ujumla.
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI NA DALILI ZAKE
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
Dalili zake
Tofauti na kuwa mgonjwa atakuwa anaumwa na tumbo kwenye kitomvu, lakini tumbo hili litafungamana na dalili zifuatazo:-
1.Kuharisha
2.Kichefuchefu
3.Kutapika
4.Homa
5.Kutokwa na jasho sana
2.Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili. Tofauti na kuwepo kwa maumivu haya pia mgonjwa ataona dalili flani.
Dalili za ugonjwa wa appendix
1.Kujaa kwa tumbo na kukaza kama mtu aliye vimbiwa
2.Kichefuchefu
3.Kutapika
4.Kuhisi maumivu ambayo huwa yakiongezeka kila unapokohoa ama unapojongea.
5.Mvurugiko wa tumbo kama kukosa choo au kuharisha
6.Homa
7.Kukosa hamu ya kula.
Ugonjwa huu ni katika magonjwa ambayo yanahitajika kutibiwa mapema na haraka sana. Endapo mgo jwa atachelewa kutibiwa appendix inaweza kupasuka, na endapo itapasuka inaweza kuhatarisha maisha.
3.Vidonda vya tumbo
Yes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum. Tofauti na maumivu ya tumbo kwenye kitomvu pia mgonjwa ataona dalili zifuatazo
Dalili za vidonda vya tumbo:
1.mvurugiko wa tumbo
2.Kuhisi tumbo kujaa na kucheua
3.Kichefuchefu
4.Kutapika
5.Kukosa hamu ya kula
6.Kutoa hewa kwa mdomoni kwa sauti
4.Matatizo kwenye kongosho
Huu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali. Pia zinapoonyesha dalili zake huwa ni kama:-
Dalili za maradhi ya kongosho
1.Kichefuchefu
2.Kutapika
3.Homa
4.Mapigo ya moyo kuongezeka
5.Kuwa na ngriri ya henia
Ugonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-
1.Mashambulizi ya bakteria
2.Henia
3.Uvimbe
4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
Dalili
1.Kichefuchefu
2.Kutapika
3.Tumbo kujaa
4.Kupunguwa maji
5.Kukosa hamu ya kula
6.Kukoa choo
7.Homa
8.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
Dalili nyingine:-
1.Kupata pumzi kwa tabu
2.Kushuka kwa presha ya damu
3.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
4.Kuzimia
5.Udhoifu wa ghafla upande mmoja wa mwili
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-
1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
2.Kuona damu kwenye choo
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi sababu za uti wa mgongo, ni ugonjwa unaotokana na kuwa na maumivu kwenye uti wa mgongo, hasa hasa ugonjwa huu ushambulia watu kuanzia miaka ishilini mpaka kwenye arobaini hivi, zifuatazo ni sababu za maumivu katika uti wa mgongo.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za fangasi Mdomoni kwa watoto, vijana, watu wazima na mama wanaonyonyeshwa.
Soma Zaidi...Hivi umeshawahikujiuliza kuhusu tezi dume. Wacha nikujuze kitu kimoja, ni kuwa tezi dume huwapata watu kuanziamiaka 40 na kuendelea. Na ifahamike kuwa tezi dume sio busha ama ngiri maji. Pia itambulikekuwa rozi dumehutibika.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yatokanayo na fangasi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dengue, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ila unasambazwa na mbu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbu anayasambaza Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa Aedes mosquito .
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kama mtu hajatibiwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe au puto katika mshipa wa damu kwenye ubongo. Uvimbe kwenye Ubongo unaweza kuvuja au kupasuka, na kusababisha kuvuja damu kwenye ubongo. Mara nyingi, kupasuka kwa Uvimbe wa Ubongo hutokea katika nafasi kati
Soma Zaidi...Seli ni chembechembe hai ambazo zimo ndani ya mwili wa binadamu na hufanya kazi mbalimbali kwenye mwili, binadamu hawezi kuishi bila seli.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya watu walio hatarini kupata fangasi
Soma Zaidi...Post inahusu zaidi athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa wajawazito au ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri.ugonjwa huu uleta madhara kwa wajawazito kama tutakavyoona
Soma Zaidi...