Post hii unahusu mtu mwenye ugonjwa wa akili ambao huitwa ugonjwa wa wasiwasi Kwa kitaalamu huitwa anxiety,ni pale mtu anapokuwa na wasiwasi Kwa vitu nafasi mbali mbali kama tutakavoona.
Dalili za mtu mwenye wasiwasi Kwa kitaalamu huitwa anxiety ni kama zifuatazo
1.kuwepo Kwa mawazo mda wote
Mtu mwenye wasiwasi anaweza kuwa na mawazo yanayozunguka kichwani mwake mara kwa mara, bila uwezo wa kuyaacha mara nyingi mawazo hayo yanaweza kusababisha huzuni na kushindwa kula au kufanya mambo mengine ya muhimu Kwa hiyo uendeleee kuwaza hata kuwaza mambo ambayo hayapo.
2.kuwepo Kwa hofu za mara Kwa mara
; inaweza kuwa na uhusiano na matukio ya kila siku au matukio yaliyopita au Kwa sababu ya kuwaza mambo ambayo hayapo na yaliyo makubwa ambayo humjengea hofu na mara nyingi mgonjwa huanza kuogopa watu na vitu vidogo hasa ambavyo havina maaana Kwa mfano unaweza kukuta mtu mzima anamwogopa mtoto wadudu na vitu vidogo vya aina hiyo.
.3.Moyo Kufanya Kazi kwa Kasi:
Mtu anaweza kuhisi mapigo ya moyo kuwa ya haraka au kuwa na mtikisiko wa mwili, hali hii inawezekana kabisa kusababishwa na pointi ya juu yake Kwa sababu mtu anapokuwa na hofu na kuogopa kila kitu pamoja na wasiwasi na mwili Kwa ujumla unareact ambapo mapigo ya moyo yanaenda mbio Kwa sababu ya woga na wasiwasi wa mgonjwa.
.4.Kukosa usingizi.
Wasiwasi unaweza kusababisha mtu kuwa na ugumu wa kuingia au kubaki katika usingizi,Kwa sababu ya kuwaza vitu ambavyo havipo pamoja na wasiwasi kusababisha mtu kukosa Usingizi Kwa sababu uwepo wa usingizi utegemea na Amani ,Kwa hiyo mtu anapoendelea kuwaza mambo ambayo hayapo hasa makubwa anashutuka kutoka Usingizini,Kwa mfano mtu anawaza kwamba Kuna watu wanakuja kumuua hawezi kulala Kwa sababu anaona anakuja kuuliwa na pengine anaweza kukimbia bila sababu,ndio maana unaweza kumwona mwehu anakimbia pasipokuwepo na sababu yoyote ya kukimbia.
.5.kutokuwa na Hamasa
Mtu mwenye wasiwasi anaweza kukosa hamasa ya kufanya mambo aliyokuwa akiyapenda mara nyingi,Kwa sababu haoni umuhimu wa kufanya jambo hilo na pia Huwa na wasiwasi kama kitu anachokifanya ni Cha ukweli au amekosea unaweza kukuta mtu anatengeneza kitu anakiharibu au pengine anakuja kutengeneza anasema Kuna watu watakuja kuharibu hali ya kuwaza na kutojiamini, kuwaza na kutowaamini wengine kusababisha mgonjwa wa aina hii kutokuwa na hamasa ya kufanya kitu chochote.Au pengine akitaka kufanya kitu mpaka anawaza matokeo hasi.
6.Kutokuwepo na umakini katika utendaji
Wasiwasi unaweza kufanya mtu awe mgumu wa kuzingatia vitu hivyo kushindwa kufikia malengo,Kwa sababu Kila anachokifanya anakifanya akiwa na wasiwasi na kutojiamini hali ambayo kusababisha kutokuwepo na umakini katika utendaji.
Mabadiliko katika Hamu ya Chakula
Watu wenye wasiwasi wanaweza kula zaidi au kupunguza kula kulingana na hali Kwa sababu yeye anawaza labda atakufa,anawaza labda anayoyafanya hayaeleweki Kwa watu,Hana Amani Kwa hiyo hata na wakati wa kula hali vizuri kitu ambacho kupelekea kupungua uzito na Kukonda Kwa sababu ya kutokuwepo hamu ya chakula.
Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi tunapaswa kutambua kwamba huu ni ugonjwa Kwa hiyo tuwatendee kama ndugu zetu na Kwa upande,Kuna watu wengine wanakoswa msaada jamii inawatenga hali ambayo kusababisha wenyewe kujitenga na jamii hatimaye wengine wanaamua maamuzi magumu na kujiua.kwa hiyo jamii inaapaswa kuonyesha ushirikiano na kuwapeleka kwenye vituo vya afya Kwa sababu huu ni ugonjwa na una chanzo chake pia unatibika.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.
Soma Zaidi...Kuziba kwa utumbo ni kuziba kwa chakula au kimiminika kisipite kwenye utumbo mwembamba au utumbo mpana (colon). Kuziba kwa matumbo kunaweza kusababishwa na mikanda ya nyuzi kwenye fumbatio ambayo huunda baada ya upasuaji, mifuko iliyovimba au iliyoambuk
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata homa ya ini,kwa sababu ya hali zao mbalimbali wanaweza kupata ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini
Soma Zaidi...Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi visababishi vya maambukizi kwenye milija na, ni mambo yanayosababisha maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na tatizo la kukosa nguvu, kuchoka ama kuhisi viungi vinelegea. Endelea na post hii.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kisukari hurejelea kundi la magonjwa yanayoathiri jinsi mwili wako unavyotumia sukari kwenye damu (glucose). Glucose ni muhimu kwa afya yako kwa sababu ni chanzo muhimu cha nishati kwa seli zinazounda misuli na tishu zako. Pia ndio chanzo ki
Soma Zaidi...