VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao.
VYNZO VYA MINYOO
Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Hapa ninakwenda kukuorodheshea kwa ufupi vyanzo hivi vya minyoo kwa ujumla wao na makundi yao:
1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama. Wakati mwingine kuosha tu haitoshelezi, maana unaweza kuosha kwa maji ambayo yana vimelea vya minyoo, hivyo unajikuta hukufanya kitu. Kwani minyoo wanaishi ardhini, kwenye majani na kwenye maji.
2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama. Maji machafu yanaweza kuwa na mayai ama lava wa minyoo hii. Maji ambayo yamechanganyika na choo kikubwa yanakuwa na mazalia ya minyoo hii. Ni vyema kuchemsha maji hata yachemke, yapozwe na yahifadhiwe vyema kwa matumizi ya nyumbani na hata biashara.
3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi. Upikaji wa nyama yeyote unatakiwa uwe wa makini sana. Kuhakikisha kuwa nyama imewiva vyema. Kuna baadhi ya nyama zinashauriwa kuwa makini sana katika kuzipika kama nyama ya ngurue na ya punda. Pia kuna aiana za samaki nao wanahitajika kuwapika vyema kama samaki aina ya kaa.
4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo. Minyoo huweza kuishi kwenye udongo, na ikitokea my akatembea bila ya viatu katika eneo hili, minyoo hawa wanaweza kupenya kwenye ngozi yake na kuingia mwilini.
5.Kula udongo, tunaona sana mara nyingi watu wanakula udongo, ukweli ni kuwa sio kila udongo unakuwa na minyoo. Kama utakuwa umeandaliwa vyema unaweza kuwa hauna minyoo. Lakini kula udongo kunaweza kusababisha minyoo. Pia kuna madhara makubwa sana ya kiafya katika kula udongo.
6.Kinyesi cha wanyama na binadamu. Hivi ni vyanzo vizuri sana vya minyoo. Kwani minyoo wanaweza kuishi kwenye kinyesi vyema na kwa muda mrefu zaidi kuliko maeneo mengine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Tina ya vidonda vya tumbo na dawa zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Hepatitis C ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoshambulia ini na kusababisha kuvimba. Watu wengi walioambukizwa na virusi vya Hepatitis C (HCV) hawana dalili. Kwa kweli, watu wengi hawajui kuwa wana maambukizi ya Hepatitis C hadi uharibifu wa ini
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya makunfi ya watu walio hatarini kupata UTI
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea njia za kujilinda na kujikinga na UTI
Soma Zaidi...VIPIMO VYA MINYOO Haitoshelezi kuwa na dalili pekee ukathibitisha kuwa una minyoo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu fangasi wa sehemu za Siri
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo.
Soma Zaidi...