image

JE?WAJUA NJIA SAFI NA KANUNI ZA KUWEKA MWILI WAKO KWENYE AFYA NZURI?

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa usafi katika maisha ya mwanadamu au mwili wa binadamu.

Tukiangalia katika maisha yetu ya iipa siku tunaona kwamba watu hawaweki mazingira yao katika hali ya usafi.usafi utusaidia kuwa salama na kuondokana na vimelea vya magonjwa.pia ukioga kunakuondolea harufu mbaya unasababishwa na jasho linalotolewa mwilini kwa njia ya ngozi.vilevile,kuoga husaidia kuzibua vitundu vya jasho,ambavyo huziba kutokana na uchafu .Aidha ,kuoga kuoga huifanya ngozi kuonekana nyororo na dhaifu.

 

ZIFUATAZO NI KANUNI ZA AFYA  AMBAZO ZINAWEKA MWILI KATIKA NZURI YA AFYA.

  1. LIshe bora,kutokana na apo mwanzo tulivyoeleza kuhusu afya ya mwili ni muhimu .lishe bora au chakula ni muhimu kwa afya zetu .pia lishe bora ni chakula chenye mchanganyiko wa virutubisho vyote muhimu ambavyo vina protini,vitamin,wanga na sukari,mafuta na madini.pia maji safi na salama ni muhimu kwa afya zetu ,protini hujenga na kukuza mwili .wanga na sukari utia mwili nguvu.mafuta uleta nguvu na joto mwilini.vitamini hupinda mwili ili usipatwe na magonjwa.madini husaidia kuimarisha mifumo na mifupa ya mwili.maji husaidia kumeng'enya chakula.pia maji husaidia kuondoa uchafu wa sumu mwilini  na kurekebisha joto la mwili .hio ni mojawapo ya kanuni nzuri ya kuweka afya ya mwili .pia ukiweza kutumia hivyo vyakula utapata afya nzuri sana

 

  1. safi wa mazingira,kutoka na apo awali tulivyoona jinsi ya kuweka afya  zetu vizuri. Usafi wa mazingira tunayoishi ni lazima yawe katika hali ya usafi.pia ni muhimu kufanya usafi wa mazingira ya nyumbani au mazingira yote yanayotuzunguka.pia kama kuna sehemu kuna mazingira machafu huvutia sana wadudu ambao ubeba vimelea vya magonjwa.vimelea hivyo huweza kusababisha magonjwa kama vile kuharisha ,kipindupindu,malaria na ugonjwa wa ngozi.inatubidi tuwe tunafanya usafi kila siku katika mazingira yetu ili tusiweze kupata magonjwa hayo.pia tukifanya hivyo tunakuwa tunalinda afya zetu .uchafu ni adui wa maendeleo.

 

  1. kutumia maji safi na salama,ili kuwa na afya bora tunatakiwa kutumia maji safi na salama.kabla ya kunywa maji hakikisha maji yamechemshwa na kuchujwa vizuri kwa kitambaa cheupe na kisafi .maji ya kunywa yachemshwe na yahifadhiwe vizuri kwenye vyombo visafi vyenye mifuniko.ni vizuri kuwa na chombo mahalumu cha kuchotea maji ya kunywa na kumiminina kwenye chombo cha kunywea maji .havitakiwi kutumia chombo hichohicho kuchotea maji na kunywa .hio ilikuwa ni kanuni jinsi gani  tunaweza kuweka mwili wetu katika hali ya usafi na afya njema.

 

  1. kupumzika na kupata usingizi,watu wengi hawajui kama kupumzika na kupata usingizi kama ni njia mojawapo  ya kuweka mwili katika hali ya afya.kupumzika niuhimu kwa afya zetu.watu inabidi watenge muda ili kupumzisha akili na kupata chakula bora.ili kuweka mwili katika hali ya afya .pia ata hivyo inatubidi usiku kulala na kupata usingizi kwa muda wa kutosha .usipolala kwa muda wa kutosha mwili hudhoofika na hatimaye kukosa nguvu.                                                                     Pia ,unaweza kupumzika kwa kujibirudisha kwa kuangalia runinga au kusikiliza radio na kusoma vitabu au magazeti.unapopumzika ,unapata nguvu mpya ya kuendelea na kazi yako,kusoma au kucheza kwa ufanisi au kufanya kazi yako.kupumzika ni muhimu kwa akili ya usalama wako na afya yako .pia inashauri angalau kwa siku moja ulale masaa name (8).ili kuweka wako safi.

 

  1. KUfanya mazoezi ya viungo vya mwili,watu wengi kufanya mazoezi hawafamyi sababu wanaona ni huharibifu wa mda.lakini usichokijua mazoezi ni muhimu sana ili kuweza kuweka mwili sawa.pia inabidi mazoezi yafanyike mara kwa mara.ili kuimarisha afya ya mwili.mazoezi kama.kuruka kamba,kukumbuka,gwaride,.pia mazoezi haya hutusaidia kuwa na utayari wa kufanya kitu .ndo maana uaga tunashuhudia bahadhi ya shure wanakimbia mchaka mchaka.hii uaga inawataka kuwaweka tayari wa kujifunza kwa ufanisi darasani.na kuijenga misuli.pia mchezo huleta burudani ,kwa hiyo ni muhimu kucheza mara kwa mara ili kudumisha afya ya mwili.mtu aliyezoea kucheza hashambuliwi naagonjwa mara kwa mara.ata hivyo ni muhimu kudumisha usafi na kufuata kanuni za afya ili mwili huweze kuwa na afya bora.pia kanuni za afya  kuonekana nadhifu na msafi wakati wote .kuongezeka kwa umri wa kuishi,kutoshambuliwa na maradhi ya mara kwa mara ,kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutenda mambo mbalimbali kwa ufanisi,wepesi na umakini ,na kuokoa gharama ambazo zingetumika kwenye matibabu.             





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1986


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Senene
Soma Zaidi...

Dalili za minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo Soma Zaidi...

Dalili za Ugonjwa wa mapigo ya moyo
Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, Kupepesuka au kudunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza kuwa ya kutisha, kwa kawaida hayana madhara. Katik Soma Zaidi...

Maambukizi ya tezi za mate
Psti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi ya tezi za mate ambao hujulikana Kama MABUSHA (mumps) ni maambukizi ya virusi ambayo kimsingi huathiri tezi mojawapo ya jozi tatu za tezi za mate zinazotoa mate, zilizo chini na mbele ya masikio Soma Zaidi...

Dalili za saratani (cancer)
Posti hii inahusu zaidi dalili za kansa, ni dalili ambazo utokea kwa mtu Mwenye tatizo la ugonjwa wa Kansa ingawa sio lazima dalili hizi kutokea tukadhani kuwa ni Kansa Ila zilizonyingi huwa ni kweli dalili za kansa. Soma Zaidi...

Magonjwa yanayowashambulia watoto wachanga
Watoto wachanga ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, watoto hawa hushambulia na maginjwa mara kwa mara na kusababisha ukuaji wao kuwa dunk, Soma Zaidi...

Dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, ni dalili ambazo zinaweza kujitokeza Kwa mgonjwa,Kwa hiyo baada ya kuona dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospital mara moja Kwa ajili ya matibabu. Soma Zaidi...

Athari za kutokutibu minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya athari zinazoweza kutokea endapo minyoo haitotibiwa Soma Zaidi...

Magonjwa ya kuambukiza.
Posti hii inahusu zaidi Magonjwa ya kuambukiza, ni magonjwa ambayo yanaweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kuweza kusababisha madhara yale yale kwa mtu aliyeambukizwa au anayeambukiza kwa hiyo Maambukizi yanaweza kuwa ya moja kwa moja au yasi Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa hepatitis C
Hepatitis C ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoshambulia ini na kusababisha kuvimba. Watu wengi walioambukizwa na virusi vya Hepatitis C (HCV) hawana dalili. Kwa kweli, watu wengi hawajui kuwa wana maambukizi ya Hepatitis C hadi uharibifu wa ini Soma Zaidi...

Vyanzo vya sumu mwilini.
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa sumu mwilini, kwa sababu kuna wakati mwingine tunapata magonjwa na matatizo mbalimbali ya ki afya tunaangaika huku na huko kumbe sababu kubwa ni kuwepo kwa sumu mwilini na vyanzo vya sumu hiyo ni kama ifuatavy Soma Zaidi...

Jinsi ya kujikinga na mafua (common cold)
Posti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi. Soma Zaidi...