picha

Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa.

Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

RPESHA YA KUSHUKA (HYPOTENION)


Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa. Kama ilivyo presha ya kushuka presha ya kupanda unaweza kuizuia ana kujilinda nayo kwa kula vyakula salama.



VYAKULA MUJARABU KWA MWENYE PRESHA YA KUSHUKA


1.Tumia chumvi zaidi; wataalamu wa afya wanahimiza sana kutumia chumvi zaidi kwani madini ya sodium yaliyomo kwenye chumvi husaidia katika kupandisha presha. Ila tambua kuwa kwa wazee kuzidi kula chumvu kunaweza kusababisha moyo kujashinwa kufanya kazi vyema.
2.Kunywa maji mengi ya kutosha: maji husaidia katika kuongeza hali ya umajimaji kwenye miili. Hii husaidia kukabilia na upungufu wa maji mwilini (dehydration) hali hizi ni muhimu kwa kukabiliana na presha ya kushuka.
3.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kwa zaidi. Kwa mfano viazi mbatata, mchele na mikate
4.Kunywa chai yenye caffein;



DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA


1.Kushundwa kuona vyema
2.Kuchanganyikiwa
3.Kizunguzungu
4.Kuzimia
5.Uchovu wa hali ya juu.
6.Kuhisi baridi
7.Kushindwa kufikiri kwa kina
8.Kichefuchefu
9.Kushindwa kuhema vyema
10.Kutokwa na jasho




NJIA ZA KUKABILIANA NA MRESHA YA KUSHUKA


1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa muda wa dakika 30 mpka 60
2.Kunywa maji mengi na ya kutosha
3.Unapokaa usikae mkao wa kukunja miguu
4.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kama viazi mbatata, mchele na mikate
5.Punguza ama wach kabisa uvutaji wa sigara
6.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe.




HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA


1.Lala chini kwenye kitu kilicho flati.
2.Kunywa maji mengi
3.Tumia chumvi, unaweza kuilamba unaweza pia kukoroga chumvi kwenye kikombe na kunywa.
4.Kama hali inaendelea kuwa mbaya zaidi ni vyema kuwasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 10535

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 web hosting    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Dalilili za kidole tumbo (appendicitis)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa Kidole ambao kitaalamu hujulikana Kama Appendicitis. Kidole tumbo husababisha maumivu kwenye tumbo la chini la kulia. Hata hivyo, kwa watu wengi, maumivu huanza karibu na kitovu na kisha kusonga. Kadiri uvi

Soma Zaidi...
Nini chanzo cha malaria

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria

Soma Zaidi...
Dalili na madhara ya Kiungulia

post hii inaelezea kuhusiana na dalili au ishara na madhara ya Kiungulia ni maumivu ya moto kwenye kifua chako, nyuma ya mfupa wako wa kifua. Maumivu huwa mabaya zaidi wakati wa kulala au kuinama

Soma Zaidi...
Dalili za Kufunga kwa ulimi (tongue tie)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kufunga kwa ulimi (Tongue-tie) kuanzia Mtoto anavyo zalia mpaka navyokua ni hali inayotokea wakati wa kuzaliwa ambayo kitaalamu hujulikana kama ankyloglossia.

Soma Zaidi...
Aina mbalimbali za michubuko

Post hii inahusu zaidi aina mbalimbali za michubuko,kwa Sababu michubuko utokea sehemu tofauti tofauti na pia Kuna aina mbalimbali kama tutakavyoona hapo mbeleni.

Soma Zaidi...
Kushambuliwa kwa moyo na kupumua

Post hii inahusu zaidi kuhusu kushambuliwa kwa moyo na kupumua, kushambuliwa kwa moyo na kupumua kwa kitaala huitwa (cardiopulmonary Arrest) ni kitendo Cha kusimama ghafla kwa moyo na kupumua.

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa macho.

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa macho, ugonjwa huu kwa kawaida una dalili kuu tano kadri ya maambukizi yanavyoongezeka na madhara yake kwa hiyo tunapaswa kujua dalili hizo Kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Je pumu inaweza kusababishwa na virusi ama bakteria?

Hapa utakwenda kujifunza jinsi ambavyo pumu inaweza kuwa na mahusiano kwa kuwepo kwa aina flani ya bakteria ama virusi.

Soma Zaidi...
Namna ya kumsaidia mtoto mwenye UTI

Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.

Soma Zaidi...
Dalili za Maambukizi kwenye mifupa

Posti hii inahusu zaidi dalili za Maambukizi kwenye mifupa, ni dalili ambazo ukionyesha kwa mtu mwenye Maambukizi kwenye mifupa.

Soma Zaidi...