Tatizo la tezi koo

Posti hii inahusu zaidi tatizo la tezi koo, ni tatizo ambalo uwapata watu mbalimbali ambapo Usababisha koo kuvimba na mgonjwa huwa na maumivu mbalimbali na pengine mgonjwa upata kikohozi kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo.

Tatizo la tezi kwenye koo.

1. Kama tulivyokwisha tangulia kusema kwamba tatizo hili uwapata watu mbalimbali, na hasa uwapata sana watu wanaoishi sehemu zenye mikusanyiko mbalimbali na kuna wataalam mbalimbali ambazo wameweza kutoa takwimu kwamba ugonjwa huu uwapata watu wa kwenye machimbo kwa sababu ya matumizi ya vyakula vya kwenye mifuko ya nailoni ila sio hawa tu na wengine wanaweza kupata kwa sababu zifuatazo.

 

2. Kuna sababu ambazo utokea kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ya virus, kwa kawaida tunafahamu kwamba ugonjwa ambao usababishwa na virus ni vigumu kupona inawezekana ugonjwa ukaisha wenyewe au kwa wakati mwingine tunatibu dalili kama vile homa , kikohozi na miwasho kwenye koo kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi.

 

3. Sababu nyingine ni pamoja na Maambukizi ya bakteria, kwa kawaida pengine kuvimba au Maambukizi kwenye koo usababishwa na kuwepo kwa Maambukizi ya bakteria, kwa kawaida kama Maambukizi yametokana na bakteria uponyaji ni rahisi kwa hiyo pamoja na kutibu dalili kama vile kutuliza homa, kutuliza maumivu, miwasho na kikohozi vile vile na antibiotics zinaweza kutumika na mtu akaomba kabisa na kuendelea na shughuli zake za kawaida.

 

4. Sababu nyingine ni pamoja na upungufu wa vitamini mbalimbali kwenye mwili.

Kwa kawaida tunafahamu matumizi ya vitamini kwenye mwili kwa hiyo kama vitamini vinakosa usababisha kuwepo kwa magonjwa kwenye koo, kwa hiyo ni vizuri kabisa kutumia mboga mboga za majani,matunda na matumizi ya mlo kamili kwa kufanya hivyo tunaweza kuepuka kuwepo kwa maambukizi kwenye koo.

 

5. Upungufu wa kinga mwilini.

Kwa kawaida watu wenye upungufu wa kinga mwilini ushambuliaji na magonjwa mbalimbali kwa hiyo ni vizuri kabisa kutumia vidonge au dawa ili kuweza kuongeza kinga na kuzuia magonjwa kama ya koo.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/02/Tuesday - 09:37:26 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1159


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-