picha

Sababu za maumivu ya viungo na viungo kuwaka moto nini sababu zake

Sababu za maumivu ya viungo na viungo kuwaka moto nini sababu zake


MAUMIVU YA VIUNGO NA VIUNGO KUWAKA MOTO.

Viungio ni sehemu za mwili ambapo mifupa hukutana. Viungio ndio ambavyo huruhusu mifupa kujongea. Miongoni mwa viungio ni kama mabega, hips, viwiko, magotini, shingoni, voganjani na maeneo mengineyo. Maumivu ya viungio ni hali ya kutokuwa sawa ama kuuma ama kupata jaoto kwa viungio. Tatizo la kuuma kwa viungio ni la kawaida sana na mara nyingi halihitaji dawa. Mtu anaweza kuhisi kama viungo vinawaka moto hali hii pia ni katika hali zinazotambulika kama maumivu ya viungo.



Ila hutokea maumivu ya viungo yakawa ni mtokeo ya maradhi ama majeraha na ajali. Maumivu ya viungo mara nyingi sababu kuu ni ugonjwa unaoitwa arthrist. Hata hivyo zio zaidi ya sababu 20 za maumivu ya viungo.



Je na wewe unasumbuliwa na maumivi ya viungio?. makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakwenda kunagalia sababu za maumivu ya viungo. Makala hii ni moja kati ya juhudi zetu za kuelemisha jamii juu ya yale ambayo yanatokea mara kwa mara kwa watu.


Nini husababisha maumivu ya viungo na viungo kuwaka moto?


1.Kuwa na infection (mashambulizi ya bakteria na virusi) kwa mfano virusi vya influenza, hepatitis


2.Kuwa na uvimbe kwenye viungio kitaalamu hutambulika kama inflamation


3.Mfumo wa kinga mwilini (autoimmune diseases) kushambulia maeneo ya viungo na kupelekea inflamation ama kuuwa seli. Hakuna sababu maalumu inayojulikana kusababisha jambo hili


4.Kukusanyika kwa asidi ya uric kwenye viungo (uric acid) mara nyingi hii huathiri miguu na utahisi kama miguu inawaka moto. Kutokunywa maji kwa wingi kunaweza kuwa m,oja ya sababu ya hambo hili. Kama una maradhi ya figo, ama shida kwenye tezi ya thyroid ama una maradhi ya kurithi inaweza kuleta shida hii kwa kiasi kikubwa. Watu wengine walio hatarini ni wenye kunywa pombe, wenye shinikizo la juula damu (presha ya kupanda, marahi ya ini kisukari na shida kwenye tezi ya thyroid



Sababu nyingine za maumivu ya viungo
5.Kulainika na kuvunjika kwa mfupa laini (cartilage) w kwenye magoti.
6.Kuwa na majeraha
7.Kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu
8.Kuwa na saratani
9.Kumung’unyika na kuvunjika kwa mifupa kutokana na ugonjwa unaojulikana kama osteoporosis
10.Udhaifu wa mifupa na matege



NJIA ZA KUZUIA MAUMIVU YA VIUNGO NA VIUNGO KUWAKA MOTO
1.Tumia dawa za kukata maumivu
2.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
3.Kabla ya kufanya mazoezi jikunyuekunjue kwanza (stretch) ili kuvipa moto viungo
4.Kunywa maji mengi na ya kutosha
5.Punguza uzito wa mwili wako kama upo juu sana.
6.Hakikisha unakula mlo kamili
7.Kama mtoto anasumbuliwa na hali hii hakikisha anakunywa maji mengi, pia vitamini D vya kutosha.




                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 4318

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

MAMBO HATARI KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

MAMBO HATARI KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO Tukiachia mbali kuchukua dawa aina ya NSAIDs, unaweza kuwa na hatari ya kuongezeka kwa vidonda vya tumbo ikiwa: Utakuwa ni mvutaji wa sigara.

Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia Ugonjwa wa kaswende

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia Ugonjwa wa kaswende, tunajua wazi kuwa Ugonjwa huu unasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kufanya ngono zembe na njia nyingine kwa hiyo tunaweza kuzuia kusambaa na kuenea kwa ugonjwa huu kwa n

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia Ugonjwa wa tauni.

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka Ugonjwa wa raundi.

Soma Zaidi...
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu.

Soma Zaidi...
Dalili za uvimbe kwenye kinywa

Post hii inahusu dalili za uvimbe kwenye kinywa ambapo kitaalamu hujulikana Kama oral candidiasis Uvimbe kwenye kinywa husababisha vidonda vyeupe, kwa kawaida kwenye ulimi au mashavu ya ndani. Wakati mwingine uvimbe kwenye kinywa huweza ku

Soma Zaidi...
Yajue mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi (cellulitis)

Mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi hujitokeza sehemu yenye jeraha pia huonyesha wekundu wenye upele,Uvimbe na malengelenge.

Soma Zaidi...
Dalili za UTI kwa wanaume

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za UTI upande wa wanaume

Soma Zaidi...
Dalili za macho makavu.

Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Nini husababisha Fangasi sehemu za Siri

Katika somo hili tutaeleza sababu kuu zinazopelekea kupata fangasi sehemu za siri, mazingira yanayochochea kuongezeka kwa fangasi, pamoja na vitu vinavyochangia maambukizi na kurudia-rudia kwa tatizo.

Soma Zaidi...