Dalili za gonorrhea - gonoria
Jifunze dalili za gonorrhea na namna inavyoambukiza, zipi athari za gonori kwa wanawae na wanaume
Dalilii za gonorrhea
Gonorrhea au gonoria ni moja kati ya magonjwa yanayoenezwa kupitia ngono. Huweza kusababishwa na bakteria na kuathiri wanaume na wanawake. Kuweza kuathiri mdomo, koo, mkundu na sehemu za siri kwa wanaume na wanawake. Huweza kuambukizwa kwa kupitia ngono ya mdomo, ngono ya ukeni ama kwenye mkundu. Kwa watoto huweza kuathiri macho. Gonorrhea (gonoria) huambukizwa kutoka kwa mama kuja kwa mtoto wakati wa kujifunguwa.
Dalili za gonoria (gonorrhea) zinaweza kuchelewa kuonekana kwa wanawake kuliko kwa wanaume. Wapo wengine hawaonyeshi dalili yeyote ile hadi hali itakapokuwa ni mbaya zaidi. Kwa mara nyingi dalili za gonoria (gonorrhea) huonekana kuanzia siku 2 mpaka 7 baada ya kuambukizwa. Na kwa wanawake inaweza kuchelewa zaidi hadi mwezi.
Ni zipi dalili za gonoria (gonorrhea)?
Dalili za gonoria (gonorrhea) unaweza kuwa na dalili tofautitofauti kulingana na jinsia. Dalili kwa wanawae na kwa wanaume zinaweza kutofautiana kulingana na maumbile ya jinsia hizi. Muda wa kutokea dalili hizi pia hutofautiana. Pia huweza kuahiri maeneo mengi mwilini.
Dalili za gonorrhea kwa wanaume:-
1.Maumivu wakati wa kukojoa
2.Kutokwa na majimaji kama usaha kwenye uume.
3.Kuvimba pamoja na maumivu ya korodani.
Dalili za gonorrhea kwa wanawake
1.Kutokwa na uchafu sehemu za siri
2.Maumivu makali ya maeneo ya nyonga
3.Maumivu makali wakati wa kukojoa
4.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
Dalili za gonoria (gonorrhea) katika maeneo mengine ya mwili:
1.Maumivu ya mkundu, na kutokwa na kama kinyesi pamoja na maumivu ya tumbo na mvurugiko.
2.Maumivu ya macho, kushindwa kuvumilia mwanga mkali, na macho kutoa kama usaha
3.Vidonga vya koo na kuvimba kwa tezi na lumph kwenye shingo
4.Maumivu ya viungio pamoja na kuwa na joto.
Ni nini chanzo na sababu ya gonoria (gonorrhea)
Kama nilivyotangulia kukuambia hapo juu kuwa gonoria huambukizwa na bakteria. Bakteria hawa hufahamika kwa jina la bacterium Neisseria gonorrhoeae. Na huenezwa kwa njia ya kufanya ngono ya mdomo, mkundu ama ukeni.
Waliohatarini kupata gonorrhea (gonoria)
Watu wa umri wowote wanaweza kupata ugonjwa huu. Hata hivyo kuna ambao wapo hatarini zaidi. Kwa wanawake walio zaidi ya miaka 25 wapo hatarini zaidi. Na wanaume ambao wanashiriki ngono ya mkundu wapo hatarini zaidi. Pia wafuatao wanaweza kuwa hatarini kupata gonorrhea:-
1.Kuanza mahusiano na mpenzi mpya
2.Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja (michepuko)
3.Kuwa na penzi ambayo ana wapenzi wengine (michepuko zaidi)
4.Kuwa na maambukizi ya goniria hapo nyuma ama kuwa na maambukizi mengine ya magonjwa ya ngono.
MADHARA YA GONORIA (GONORRHEA) ENDAPO HAITATIBIWA
Endapo gonoria itachelewa kutibiwa inaweza kuleta madhaya mengi ndani ya mwili kuanzia ugumba, kudhoofu mwili, maumivu na mengineye. Yafuatayo ni madhara ya kuchelewa kutibu gonoria:-
1.Ugumba kwa wanawake. Ugonjwa huu kwa mwanamke unakula via vya uzazi kwa fujo sana. Unaathiri mirija ya falopia ambayo nduo inayohusika kubeba yai na utungaji mzima wa mimba na kusababisha PID yaani Pelvic Inflamatory Deseases. Hivyo mwanamke anahitajika atibiwe mapema kabla madhara hayajakuwa makubwa.
2.Ugumba kwa wanaume. Kwa wanaume gonoria huathiri vimirija vijidogo vilivyopo kwenye korodani. Mirija hii hujulikana kama epididymis. Hali hii hupelekea kuharibika kwa mirija hii hivyo kushindwa kubeba mbegu za kiume kuzitoa nje. Ugonjwa unaosababishwa na uharibifu huu hujullukana kama epididymitis.
3.Mashambukizi ya viungo vingine vya mwili na kuleta homa, upele, vidonda, maimivu ya viungo, kukaza na kuvimba kwa viungio.
4.Huongeza hatari zaidi kwa mwenye VVU na UKIMWI. Watu wenye VVU na UKIMWI ni rahisi kueneza gonoria kwenda kwa mwingine.
5.Kwa watoto waliop[ata gonoria wakati wa lujifunguwa wanaweza kupata upofu na madhara mengine kati afya zao.
NJIA ZA KUPAMBANA NA KUKABILIANA NA GONORIA (GONORRHEA)
1.Kuwa mwaminifu katika mahusiano wacha kuchepuka
2.Hakikisha mwenza wako yupo salama
3.Usishiriki ngono na mtu aliyeathiriwa na magonjwa ya ngono bila kinga
4.Tumia kondomu
5.Pima mara kwa mara gonoria.
.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 ai web app π2 web hosting π3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π4 Kitau cha Fiqh π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Dalili za Ugonjwa wa ini
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Dalili za ugonjwa wa upele
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa upele, ni dalili au mwonekano wa mgonjwa wa upele.
Soma Zaidi...Homa ya manjano, dalili za homa ya manjano na namna ya kujikinga na homa ya manjano
HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.
Soma Zaidi...Dalili za ngozi kuwasha.
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa kuhusiana na dalili za ngozi kuwashwa.
Soma Zaidi...Sababu za Hedhi Kuchelewa Bila Mimba
βKuchelewa kwa hedhi ni jambo linaloweza kuleta hofu na wasiwasi, hasa kwa wanawake wanaohisi kuwa mimba ndiyo sababu pekee. Hata hivyo, kuna sababu nyingi za kibiolojia na mtindo wa maisha zinazoweza kusababisha mzunguko wa hedhi kuvurugika. Post hii inachunguza visababishi hivi na kutoa mwongozo wa wakati mwafaka wa kuona daktari.
Soma Zaidi...Ni zipi dalili za Ukimwi na ni zipi dalili za VVU
Ijuwe historia ya VVu, Dalili zake, tiba na vipimo vyake pia njia za kueneza VVU na UKIMWI
Soma Zaidi...