picha

Dalili za uti kwa wanaume na wanawake

tambuwa chanzo na dalili za UTI na tiba yake, pamoja na njia za kupambana na UTI

Dalili za uti kwa wanaume na wanawake

UGONJWA WA UTI
Ugonjwa wa UTI ni kifupisho cha Urinary Track infections. Haya ni maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo. Mashambulizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria aina ya E.Coil. Bakteria hawa huishi kwenye utumbo (gastrointestinal track). Pia UTI inaweza kusababishwa na fangasi na virusi kwa kiasi kidogo sana. UTI inasumbuwa sana watu, inakadiriwa kuwa kati ya kila watu watano mmoja ana UTI. Wanawake wapo hatarini zaidi kupata UTI kuiko wanaume



UTI inaambukizwa vipi?
Maambukizi mengi ya UTI yana tokea choon wakati wa kujisafisha. Bakteria hawa wanatoka kwenye utumbo kuja nje kupitia haja kubwa. Sasa ikitokea mtu amejisafisha vibaya anaweza kuwachukuwa bakteria hawa na kuwapa njia kuingia kwenye njia ya mkojo na kusababisha mashambulizi. Pia wakati wa kushiriki tendo la ndoa (ngono). hii inaweza kusababisha UTI kuhama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Pia kushirikiana vifaa vya ngono, kutumia vifaa vya uzazi wa mpango na njia nyinginezo.



Dalili za UTI
1.Kukojoa mara kwa mara
2.Kuhisi kuunguwa ama umoto wakati wa kukojoa
3.Kutoa mikojo kwa uchache
4.Mkojo kuwa mchafu, kama mawingu ama mwekundu uliopauka
5.Harufu kali ya mkojo
6.Maumivu ya kwenye njonga kwa wanawake
7.Maumivu ya mkundu na puru kwa wanaume.



Dalili za UTI zinaweza pia kuwa tofauti na hizo hapo juu. Dalili hizi hutofautiana kwa kulingana na aina ya UTI. Kama unataka kuzijuwa dalili zaidi za UTI endelea kusoma makala hii mpaka mwisho.



Aina za UTI na dalili zake.
Ugonjwa wa UTI umegawanyika katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni kama:-
1.UTI ya kwenye figo (acute pyelonephritis). UTI hii huathiri figo, na kusababisha dalili kama:-
1.Maumivu ya mgongo kwa juu
2.Homa kali
3.Kuhisi baridi na kutetemeka
4.Kichefuchefu
5.Kutapika.



2.UTI ya kwenye kibofu (cystitis). hii ni aina ya UTI ambayo huathiri kibofu cha mkojo. Dalili zake ni:-
1.Maumivu ya nyonga
2.Maumivu ya tumbo kwa chini ya kitovu ama mvurugiko wa tumbo kwa chini
3.Kukojoa mara kwa mara huku ukiwa na maumivu.
4.Kukojoa damu, ama mkojo wenye rangi nyekundu ya kupauka.



3.UTI ya kwenye mrija wa mkojo (urethritis). mrija wa mkojo kitaalamu unaitwa urethra. Huu ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu na kuuleta nje. Dalili za UTI hii ni kuhisi kuunguwa wakati wa kukojoa.



Dalili za UTI kwa upande wa wanawake.
Kwa upande wa wanawake dalili za UTI zinaweza kuwa zaidi ya tulizotaja hapo juu. Kwa wanawake UTI inaweza kuathiri mfumo mzima wa uzazi kwa mwanmke. Kwa mfano mwanamke anaweza kupata dalili za mimba kumbe ni UTI. Kuvimba kwa matiti, kuuma kwa tumbo, kubadilika hedhi, kukojoa mara kwa mara. Kwa ufupi kwa wanawake uti inaweza kusumbuwa sana kwani inadhaniwa ni maradhi mengine.



Dalili za UTI kwa wanaume.
Kwa wanaume dalili za UTI ni kama ambazo tumetangulia kuzitaja hapo juu. Kwa wanaume hawana dalili maalumu kama wanawake. Hata hivyo maumivu ya kwenye puru na mkundu hutokea kwa wanaume na si kwa wanawake.



Watu hawa wapo hatarini kupatwa na UTI.



1.Kuwa mwanamke. Wanawake wapo hatarini kwa sababu ya maumbile yao. Njia yao ya mkojo ipo karibu sana na njia ya hajakubwa. Hata hivyo njia yao ya mkojo ni fupi kukifikia kibofu kuliko wanaume.
2.Kuwa ni mwenye kushiriki ngoni.
3.Kama unatumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama spermicidal agent
4.Kama mwanamke hapati tena hedhi, yaani amefikia kikomo cha kupata hedhi
5.Kama una matatizo kwenye mfumo wa mkojo.
6.Kama njia ya mkojo imeziba kwa mfano kama unavijiwe kwenye figo na vikaziba njia ya mkojo.
7.Kama unatumia matibabu ya kuongezea kinga ya mwili nguvu kama vile wenye kisukari
8.Kama unatumia mpira wa kukojolea.



NJIA ZA KUJILINDA NA KUIJIKINGA NA UTI
1.Kunjwa maji mengi sana
2.Nenda ukakojoe punde baada ya kufanya ngono
3.Kwa mwanamke jisafishe kuelekea nyuima na si kutokea nyuma kuelekea mbele
4.Safisha vyema choo baada ya kujisaidia
5.Nenda ukakojpoa punde tu unapohisi unataka kukojoa
6.Vaa nguo za ndani zilizo kavu na zisizo bana.
7.Jisafishe vyema sehemu za siri kabla na baada ya kufanya ngono.





                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 5851

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰2 web hosting     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰5 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Madhara ya fangasi.

Posti hii inahusu zaidi madhara ya fangasi za ukeni kwa kawaida tunajua kubwa fangasi zikiingia kwenye uke usababisha madhara mbalimbali ambayo mengine yanaweza ya kudumu na mengine ya mda kama yametibiwa mapema.

Soma Zaidi...
MJUE MBU, NA YAJUWE MARADHI MAKUU MATANO (5) HATARI YANAYOAMBUKIZWA NA MBU, malaria kukamata namba moja kwenye maradhi hayo)

Mbu ni katika wadudu ambao husababisja vifo vya maelfu kila mwaka, na mamilioni ya watu wanaathirika na maradhi yaletwayo na mbu.

Soma Zaidi...
Njia salama za kusafisha sehemu za siri

Afya ya sehemu za siri ni nguzo muhimu ya afya ya mwili mzima, lakini kuna potofu nyingi zinazozunguka namna gani ya kuzihudumia. Makala haya yanajadili njia salama na za kitaalamu za kusafisha sehemu za siri (kwa wanawake na wanaume), makosa ya kuepuka kama vile matumizi ya sabuni zenye marashi na mtindo wa douching, na jinsi ya kulinda bakteria walio salama (normal flora) ili kuzuia maambukizi kama UTI na fangasi.

Soma Zaidi...
Madhara ya Tiba kemikali kwa wagonjwa wa saratani

Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba kemikali, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wa saratani, madhara haya yanayoweza kuwa ni kwa Sababu mbalimbali kama vile kuaribika kwa seli zinazoendelea kufanya kazi kwenye mwili.

Soma Zaidi...
Saratani ya tishu zinazounda Damu mwilini (leukemia)

Post hii inaelezea kuhusiana naร‚ย Sarataniร‚ย ya tishu zinazounda damu mwilini, ikijumuisha uboho na mfumo wa limfu.ugonjwa huu kitaalamu huitwa leukemia.

Soma Zaidi...
Njia za kusambaa kwa ugonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine

Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Soma Zaidi...