IJUE HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV) DALILI ZAKE, TIBA YAKE, CHANJO YAKE, NA MBU ANAYESAMBAZA HOMA HII

Haya ni maradhi ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kwa kupitia mbu.

IJUE HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV) DALILI ZAKE, TIBA YAKE, CHANJO YAKE, NA MBU ANAYESAMBAZA HOMA HII

3. HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV)

Haya ni maradhi ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kwa kupitia mbu. Mbu aina ya Aedes aegypti ndiye ambaye anatuhumiwa kwa kusambaza maradhi haya. Homa hii kwa mara ya kwanza iligundulika mwaka 1952 Tanzania.

 

Dalili za maradhi haya zinaweza kutokea siku 3 mpaka 7 baada ya kung'atwa na mbu huyu. Dalili za malaria ni sawa na zile za dengue ila utofauti ni kuwa homa hii haipelekei kutokwa na damu. Dalili hizo ni kama homa, maumivu ya viungio, baridi, kutapika na kichefuchefu, maumivu ya mgongo pamoja na miwasho.

 

Neno 'chikungunya' ni neno la kabila ya kimakonde, kabila linalopatikana kusini mwa Tanzania. Neno hili linamaana ya "kunyumbulisha viungo katika hali isiyo ya kawaida". Nenohili lilimaanisha maumivu ya viungo anayoyapata mgonjwa. bado homa hii pia haina dawa ila zipo dawa za kupunguza athari ya dalili za homa hii.

                    Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 155


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-