MINYOO NI NINI?
MINYOO NI NINI?
Minyoo ni katika vimelea ama wadudu wanaoishi ndani ya kiumbe aliye hai. Wanaweza kuishi kwenye wanyama kama ngo’ombe, ngurue na mbuzi, pia wanaweza kuishi ndani ya binadamu. Wanajipatia mahitaji humo kama chakula, hewa na kila wanachohitaji. Wakiwa wanaishi ndani ya mwili wa kiumbe hai wanaweza kusababisha madhara makubwa sana katika afya ya mtu. Wadudu hawa kitaalamu wanatambulika kama parasitic worm.
Katika makala hii tutakwenda kujifunza, dalili, sababu, matibabu na njia za kupambana na minyoo katika mazingira yetu. Pia tutaona madhara ya kiafya yanayoletwa na kuishi na minyoo mwilini. Endelea kuwa nasi upate faida hii
Hatari ya kupata minyoo ni kubwa sana maeneo ya vijijini ama katika maeneo ambayo hali ya usafi sionzuri. Nchi zinazoendelea kama nchi za afrika ni katika maeneo ambayo yanakabil;iwa sana na minyoo kuliko nchi zilizo endelea.
Wataalamu wanatueleza kuwa kuna aina zaidi ya 300,000 (laki tatu) za minyoo. Na katika aina hizi kuna aina 300 (mia tatu) za minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu na kumuathiri kwa namna moja ama nyingine.
Minyoo wanazaliana kwa kutaga mayai, na mayai yao yanatofautiana ukubwa, kuna ambayo yanaonekana kwa macho na mengine ni madogo zaidi kwa kuonekana kwa macho. Kuna aina za minyoo hutaga mayai bila ya kuhitaji kuwepo kwa dume, kwani kuna minyoo ambayo ina jinsia zote kwa pamoja (hermaphroditc).
Minyoo huweza kutaga mayai zaidi ya mara sita kwa siku. Na idadi ya mayai yao ni kati ya mayai 3000, mpaka 700000. na mayai yao yanaweza kudumu kwa miezi mingi biala ya kufa, na yanaweza kuvumialia hali mbalimbali za joto.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni huduma maalumu ambayo utolewa kwa mtu ambaye ana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo. Zifuatazo ni huduma maalumu kwa mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito, kaswende inaweza kukaa kwa mtu zaidi ya miaka mingi bila kuleta madhara ya moja kwa moja lakini kadiri ya siku zinavyokwenda madhara utokea hasa wakati wa ujauzito, madhara hayo umwadhiri mtot
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisichokuwa na damu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster. Kwa hiyo ili kugundua kubwa mtu ana Ugonjwa huu Dalili kama hizi zifuatazo zinaweza kutokea kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...Saratani ya Utumbo ni Saratani ya utumbo mpana (koloni), sehemu ya chini ya mfumo wako wa usagaji chakula. Kwa pamoja, mara nyingi hujulikana kama Saratani ya utumbo mpana. Visa vingi vya Saratani ya utumbo mpana huanza
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.
Soma Zaidi...